GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

GE2025 CHADEMA wataka anayedhaniwa kuwa Polisi atolewe nje ya Mahakama

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao

Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili



Chanzo: Mwananchi
 
Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam wakiomba kutolewa nje mtu mmoja aliyedhaniwa ni askari ambaye ameenda kukaa katika benchi la wafuasi hao.

Leo Septemba 8, 2025 Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anapandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali (preliminary hearing) wa kesi ya uhaini inayomkabili.

Source Mwananchi
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
 
Hivi polisi akiwa off, hana haki ya kwenda kusikiliza kesi mahakamani kama raia wengine? Au mtu akiwa polisi anapoteza haki nyingine zote?

Chadema msijekuwa mnafukuza malaika mkidhani ni shetani!
Kwa mambo iliyotengenezwa na watawala hamna kuaminiana, wapo sahihi kwa madhira wanayofanyiwa.
 
Hivi ni kwa nini hawa askari wanapenda sana kuleta taharuki ktk matukio kama haya halafu wanawasingizia chadema kwamba ndio wanafanya fujo... Yaani mpenzi wa Yanga akakae kwenye benchi la mashabiki wa simba.. lazima watamgawana tu.
 
Chadema waache mambo ya kizamani. Hata ikiwa ni polisi ndio iweje? Kwani wakitaka kukushikeni wote mliopo hapo watashindwa??!!!
Acheni vurugu zisizo na msingi.
Kuweni waungwana.
 
Back
Top Bottom