CHADEMA Washington DC, Marekani yapata uongozi mpya

CHADEMA Washington DC, Marekani yapata uongozi mpya

Kila linapotajwa jina la Leticia Nyerere, natamani niwaite FBI wamchunguze huyu mama. CDM inajidhalilisha sana kumtumia huyu opportunist

Duh!ebwabaee,Eti fitinamwiko!kumbe mnafiki wal mnafikuna!
 
TAARIFA KWA UMMA
CHADEMA WASHINGTON DC, MAREKANI YAPATA UONGOZI MPYA
Kikao cha Viongozi wa Tawi la Chadema Washington DC, Marekani, tarehe 27 July 2013 kimemteua Ndugu Kalley Ammy Pandukizi kuwa Mwenyekiti wa Tawi kuchukua nafasi ya Ndugu Cosmas Wambura. Awali Ndugu Kalley Pandukizi alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tawi la Chadema DMV linalobeba majimbo matatu ya Washington DC, Maryland na Virginia. Baadae alikuwa Afisa wa Habari wa Tawi na nafasi yake kuchukuliwa na Cosmas Wambura. Viongozi wengine na nafasi zao ni Katibu wa Tawi ni Libearatus Mwang'ombe aliyekuwa katibu wa kwanza wa Tawi, aliyechukua nafasi ya Isidory Lyamuya. Katibu Mwenezi ni Ndugu Hussein Kauzela na Mweka hazina ni Ndugu Ludigo Mhagama. Mwenyekiti wa Baraza la wanawake ni Ndugu Baybe Mgaza na Katibu wa Baraza la wanawake ni Mariam Khamis. Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Ndugu Amri Maliyatabu na katibu wa baraza la vijana ni Ndugu Stephen Msungu. Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee ni Amos Cherehani na Katibu wa baraza la wazee ni Elias Mshana. Nafasi ya Mwisho ni ya Baraza la Washauri linaloongozwa na Prof Nicolas Boaz na Emmanuel Muganda.
Akizungumza baada ya Uteuzi huo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley, Amewashukuru Viongozi wote kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuwaahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa Tawi na kuwaunganisha wanachama kuwa wamoja. Pia ameahidi kushirikiana na Jumuia nyingine ikiwemo Jumuia ya Watanzania DMV, Ofisi ya Ubalozi Wa Tanzania Marekani, Jumuia ya Waislam waishio Washington DC (TAMKO) na Uongozi wa CCM DMV ili kujenga Tanzania Moja yenye mshikamano.
Pia Ndugu Kalley amesema baada ya kurudi kwenye nafasi hiyo kipaumbele cha kwanza kitakuwa kuvalia njuga mambo makuu mawili ambayo ni Suala la mchakato wa Katiba unaoendelea ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba nzuri iliyoridhiwa na Watanzania wote bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa nia mbaya. Pili amesema atavalia njuga suala la upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi Ujao wa Mwaka 2015 uwe huru na Haki.
Aidha Katika mkutano huo Ndugu Kalley ameelezea kusikitishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa Sheria vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia wasio na hatia na hata matukio ya mauaji wanayotuhumiwa baadhi ya Askari Polisi. Ndugu Kalley amesema atapambana vikali kuhakikisha matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za raia yanayofanywa na baadhi ya askari Polisi yanakomeshwa, kwani hakuna sheria inayoruhusu askari Polisi kujichukulia sheria mkononi wakati Mahakama ndizo zilizopewa Mamlaka hiyo.
Tawi la Chadema Washington DC lilianzishwa rasmi tarehe 26 Aprili 2012 chini ya usimamizi wa Mbunge wa viti maalum Mh Leticia Nyerere na Kufunguliwa rasmi tarehe 27 Mei 2012 na Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu katibu mkuu wa Chadema Mh Zitto Kabwe. Sherehe hizo za Ufunguzi ziliudhuriwa Pia na Mbunge wa Iringa mjini Mh Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari, Mbunge wa Viti Maalum Kwimba Mh Leticia Nyerere na Mbunge wa Viti maalum Kutoka Zanzibar Mh Mariam Msabaha.
Sina imani na Kalley Ammy Pandukizi. Kwanza hata kidato cha nne hajafika. Hii ni kusema kuwa hana elimumya kutosha kutekeleza hayo aliyoahidi. Namshauri arudi darasani na ajiendeleze kwenye taaluma yake ya IT nadhani ni bora zaidi kuliko majukwaa anayovamia
 
Hongera Uongozi Mpya USA.Tuko pamoja 24 Hrs.Diaspora ni engine ya mabadiliko . Akina Kwame Nkrumah ni product ya Diaspora iliyokua instrumental katika kupigania uhuru wa Ghana uliokua inspiration kwa wapigania uhuru wa Afrika.Tunapigania uhuru wa pili.It's our moment!
Chadema mnachekesha sana. Yaani huyu mkongoman kalley ndo mmemwamini na kumpa nafasi hiyo? Ana uzalendo gani na Tanzania?
 
Duh!ebwabaee,Eti fitinamwiko!kumbe mnafiki wal mnafikuna!
Unafiki upo wapi? kupenda CDM na ku over look viongozi wake? Google Leticia Nyerere uone jinsi maisha yake yanavyosakamwa na misukosuko ya sheria za Maryland. Love makes blind
 
Unafiki upo wapi? kupenda CDM na ku over look viongozi wake? Google Leticia Nyerere uone jinsi maisha yake yanavyosakamwa na misukosuko ya sheria za Maryland. Love makes blind
Mkuu, leticia nyerere maisha yake yamejaa utata na utapeli. Haaminiki hata kidogo.
 
Hongera uongozi mpya. Kila la heri katikakuwajibika na kulitumikia Taifa hili ktk nafasi mlizonazo.
Tunahitaji kila aina ya mchango, hivyo bandugu songeni mbele.
 
Sina imani na Kalley Ammy Pandukizi. Kwanza hata kidato cha nne hajafika. Hii ni kusema kuwa hana elimumya kutosha kutekeleza hayo aliyoahidi. Namshauri arudi darasani na ajiendeleze kwenye taaluma yake ya IT nadhani ni bora zaidi kuliko majukwaa anayovamia

Unaongea kama mnafki au una wivu usio na maendeleo. Unasema hajasoma, hajafika kidato cha nne,Halafu unashauri ajiendeleza na taaluma yake ya IT so kumbe ni msomi? ana taaluma ya IT? sasa yeye akienda majukwaani kinachokuuma nini? anakuzuia wewe kupata riziki yako ya kila siku? Kuelimika si wingi wa vidato.
 
Mbona mnafaidika na pesa za hao wasio kuwa na makaratasi wanaoishi nje?Kila siku hao wasio na makaratasi wanatuma dola kuja huko Tanzania.Na serikali inatoa madafu na sio dolla.angalia sana .ethiopia wamenufaika na hao wasiokuwa na makaratasi na wenye makaratasi kwa pamoja.na wamejenga dam kubwa kuliko yoyote barani africa.kwa michango tu kutoka kwa kila mhiethiopia anaye ishi nje.Tanzania viongozi wamekalia roho mbaya tu.wanawanyima watu passport bure tu eti unakwenda nje kufanya nini?.sasa hivi mnaona watoto wa wakubwa ndio wauza ngano wazuri sana.Nafurahi sana nikimwona mtoto wa mlala hoi huku nje kuliko yule wa kigogo.
 
Kalley Pandukizi namjua vizuri sana, Amezaliwa Ocean Road Hospital Miaka ya sabini. Baba yake ni Mdoe wa Bagamoyo lakini si ndugu na Kikwete. Mama yake ni Mzigua wa Turiani. Ameishi magomeni makuti tangu akiwa mdogo, nyuma ya kanisa katoliki mtaa wa Mlandizi, Baadae akaishi mtaa wa Ufipa Kinondoni Nyumba ya tano kutoka makao makuu ya Chadema, Ndio maana amekuwa mfuasi wa Chadema maana alikuwa anaishi karibu na makao makuu ya Chadema mtaa wa Ufipa. Hata ukimuuliza fundi cherehani anayeshona magwanda ya chadema mtaa wa Ufipa yule mpare atakwambia anaijua familia yake. Kalley ninayemjua mimi ni mtaalamu wa Lugha ya Kifaransa. Amesoma elimu hiyo Alliance Francaise kwa miaka mitatu mapaka alipohitimu Diplome Superiera au High Diplome, baadae akawa mwalimu wa Lugha hiyo kwa miaka mitatu. Pia alisoma taaluma ya Computer kwa miaka mitatu na kuhitimu. Na pia hivi tunavyozungumza anatarajia kuhitimu taaluma ya lugha ya Kispanish. Sasa Kalley Unayemzungumzia wewe ni yupi?
 
Back
Top Bottom