Kabewa
Senior Member
- Oct 30, 2009
- 136
- 56
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekwepa kumwekea pingamizi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kama kilivyoahidi na badala yake kimepeleka malalamiko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya ahadi kadhaa za mgombea huyo.
Aidha, tofauti na ahadi ya chama hicho kwamba kada wake aliyejipatia umaarufu hivi karibuni, Mabere Marando, ambaye ni wakili mashuhuri ndiye angepeleka pingamizi hilo, jana malalamiko hayo yaliwasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika.
Akizungumza wakati akiwasilisha malalamiko hayo, Mnyika ambaye pia anagombea ubunge Ubungo, alisema wameamua kuwasilisha barua ya malalamiko ili Msajili John Tendwa, ingawa hawamuamini, amwekee pingamizi Kikwete, baada ya kubaini kuwa hawana uwezo huo tofauti na walivyoahidi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake Jumamosi.
Kwa mujibu wa Mnyika, Chadema ambayo licha ya Marando pia kina mwanasheria mwingine Tundu Lisu, kilibaini kuwa mwenye uwezo kisheria kumwekea pingamizi mgombea urais si chama cha siasa bali Msajili.
Mnyika ambaye aliwasilisha barua hiyo kwa kofia tatu kama mpigakura, Kaimu Katibu Mkuu na kwa niaba ya Chadema, alidai mgombea wa CCM alitoa maneno na kufanya vitendo vilivyokatazwa chini ya kifungu cha 21 (1) (a) na (e) ya sheria namba 6 ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.
Alidai mgombea huyo alitumia nafasi yake ya urais wakati wa kampeni, kushawishi wapiga kura wamchague kwa kutoa ahadi kadhaa.
Ahadi zinazodaiwa kutolewa wakati wa kampeni ni ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kupandisha kima cha chini kutoka Sh 135,000 hadi Sh 235,000 na barua hiyo ya malalamiko imewasilisha pia nakala ya gazeti kama ushahidi.
Hata hivyo, habari hiyo ya gazeti hili yenye kichwa JK: Ni matusi kudai sijali wafanyakazi, inaonesha kima cha chini kupandishwa kutoka Sh 104,000 hadi Sh 135,000 na si Sh 235,000.
Fedha hizo za nyongeza hazikuidhinishwa na Bunge na amezitoa kwenye OC (matumizi mengine) hiyo ni hongo na rushwa kitendo hicho kilikuwa na nia ya kuwashawishi wafanyakazi kama wapiga kura, kumpigia kura Kikwete kutokana na nyongeza hiyo ya mishahara, alidai.
Mgombea huyo pia analalamikiwa kutumia nafasi yake ya urais wakati wa kampeni kuahidi kukilipa Chama cha Ushirika cha Nyanza, Sh bilioni tano, ili kilipe madeni yake ambayo kinadaiwa na kuahidi Serikali kuchukua madeni yote ya vyama vya ushirika.
Hata hivyo, uchukuaji wa madeni ya vyama vya ushirika vilivyokufa, ulianza kufanyika kwa vyama mbalimbali vilivyokuwa na madeni tangu mwanzoni mwa Serikali ya Awamu ya Nne, kwa nia ya kuviwezesha kununua mazao ya wakulima, ambayo yalikuwa yakilanguliwa na wafanyabiashara kwa bei ya chini.
Malalamiko mengine ni kutumia nafasi yake ya urais kuahidi watu wa mkoa wa Kagera kununua meli mpya ya kisasa itakayotumiwa na wananchi wa mkoa huo kusafiri kati ya Bukoba na Mwanza.
Alidai kwamba ahadi hizo zina lengo za kushawishi wananchi wa Kagera na Mwanza wanaotumia usafiri wa meli na wanaohudumiwa na chama cha ushirika cha Nyanza, kumpigia kura.
Nyongeza ya mshahara, ahadi ya Sh bilioni tano na ahadi ya mali imetumika kama hongo kwa hao wote wahusika ili wampigie kura Kikwete, ilisema sehemu ya barua hiyo yenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/MSJ/04/32.
Katika uzinduzi wake na kwenmye Ilani yake Chadema imeahidi wananchi kutoa elimu ya msingi mpaka chuo kikuu bure na ahadi za vyama vingine ambazo zimekuwa zikitolewa kwa nia ya kushawishi wagombea wao wapigiwe kura.
Alipotakiwa kutoa ushahidi wa jinsi Rais Kikwete alivyotumia nafasi yake ya urais kushawishi wapiga kura kumpigia kura, alisema wametumia ushahidi wa vyanzo vya umma, ambavyo ni vyombo vya habari na kuwasilisha nakala ya magazeti matatu na kanda za video.
Kutokana na malalamiko hayo, chama hicho kimemwomba Msajili baada ya kuridhika kuwa Rais Kikwete amefanya vitendo vilivyokatazwa na sheria na kupoteza sifa za kushiriki mchakato wa uchaguzi, jina lake liondolewe.
Barua hiyo ilisisitiza: jina lake liondolewe chini ya kifungu 24(1) cha Sheria ya Gharama ya Uchaguzi ya mwaka 2010, kinachosema mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelezwa katika sehemu hii, atakuwa amepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi na uchaguzi.
Hata hivyo, Mnyika alisema amewasilisha malalamiko hayo huku akiwa na imani yenye shaka, kwa sababu Msajili ameteuliwa na Rais ambaye wanamlalamikia.
Tumempa Msajili malalamiko, wakati tukijua ameteuliwa na Rais na hiki ni kipimo kwake kama atasimamia sheria kwa uhuru, akishindwa tutaeleza kwa wananchi hatua tutakazochukua, alisema
Alipoulizwa Tendwa uamuzi wake baada ya kupokea malalamiko hayo Katibu Muhtasi wake, alisema: Msajili amesema hawezi kuzungumza nanyi leo (jana) ila mje kesho (leo) asubuhi atatoa majibu ya malalamiko haya.
Source Habari Leo