Chadema washindwa kumzuia kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema washindwa kumzuia kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kabewa, Aug 31, 2010.

 1. Kabewa

  Kabewa Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 98
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekwepa kumwekea pingamizi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, kama kilivyoahidi na badala yake kimepeleka malalamiko kwa Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya ahadi kadhaa za mgombea huyo.

  Aidha, tofauti na ahadi ya chama hicho kwamba kada wake aliyejipatia umaarufu hivi karibuni, Mabere Marando, ambaye ni wakili mashuhuri ndiye angepeleka pingamizi hilo, jana malalamiko hayo yaliwasilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika.

  Akizungumza wakati akiwasilisha malalamiko hayo, Mnyika ambaye pia anagombea ubunge Ubungo, alisema wameamua kuwasilisha barua ya malalamiko ili Msajili John Tendwa, ingawa hawamuamini, amwekee pingamizi Kikwete, baada ya kubaini kuwa hawana uwezo huo tofauti na walivyoahidi wakati wa uzinduzi wa kampeni zake Jumamosi.

  Kwa mujibu wa Mnyika, Chadema ambayo licha ya Marando pia kina mwanasheria mwingine Tundu Lisu, kilibaini kuwa mwenye uwezo kisheria kumwekea pingamizi mgombea urais si chama cha siasa bali Msajili.

  Mnyika ambaye aliwasilisha barua hiyo kwa kofia tatu kama mpigakura, Kaimu Katibu Mkuu na kwa niaba ya Chadema, alidai mgombea wa CCM alitoa maneno na kufanya vitendo vilivyokatazwa chini ya kifungu cha 21 (1) (a) na (e) ya sheria namba 6 ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.

  Alidai mgombea huyo alitumia nafasi yake ya urais wakati wa kampeni, kushawishi wapiga kura wamchague kwa kutoa ahadi kadhaa.

  Ahadi zinazodaiwa kutolewa wakati wa kampeni ni ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kupandisha kima cha chini kutoka Sh 135,000 hadi Sh 235,000 na barua hiyo ya malalamiko imewasilisha pia nakala ya gazeti kama ushahidi.

  Hata hivyo, habari hiyo ya gazeti hili yenye kichwa ‘JK: Ni matusi kudai sijali wafanyakazi’, inaonesha kima cha chini kupandishwa kutoka Sh 104,000 hadi Sh 135,000 na si Sh 235,000.

  “Fedha hizo za nyongeza hazikuidhinishwa na Bunge na amezitoa kwenye OC (matumizi mengine) hiyo ni hongo na rushwa … kitendo hicho kilikuwa na nia ya kuwashawishi wafanyakazi kama wapiga kura, kumpigia kura Kikwete kutokana na nyongeza hiyo ya mishahara,” alidai.

  Mgombea huyo pia analalamikiwa kutumia nafasi yake ya urais wakati wa kampeni kuahidi kukilipa Chama cha Ushirika cha Nyanza, Sh bilioni tano, ili kilipe madeni yake ambayo kinadaiwa na kuahidi Serikali kuchukua madeni yote ya vyama vya ushirika.

  Hata hivyo, uchukuaji wa madeni ya vyama vya ushirika vilivyokufa, ulianza kufanyika kwa vyama mbalimbali vilivyokuwa na madeni tangu mwanzoni mwa Serikali ya Awamu ya Nne, kwa nia ya kuviwezesha kununua mazao ya wakulima, ambayo yalikuwa yakilanguliwa na wafanyabiashara kwa bei ya chini.

  Malalamiko mengine ni kutumia nafasi yake ya urais kuahidi watu wa mkoa wa Kagera kununua meli mpya ya kisasa itakayotumiwa na wananchi wa mkoa huo kusafiri kati ya Bukoba na Mwanza.

  Alidai kwamba ahadi hizo zina lengo za kushawishi wananchi wa Kagera na Mwanza wanaotumia usafiri wa meli na wanaohudumiwa na chama cha ushirika cha Nyanza, kumpigia kura.

  “Nyongeza ya mshahara, ahadi ya Sh bilioni tano na ahadi ya mali imetumika kama hongo kwa hao wote wahusika ili wampigie kura Kikwete,” ilisema sehemu ya barua hiyo yenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/MSJ/04/32.

  Katika uzinduzi wake na kwenmye Ilani yake Chadema imeahidi wananchi kutoa elimu ya msingi mpaka chuo kikuu bure na ahadi za vyama vingine ambazo zimekuwa zikitolewa kwa nia ya kushawishi wagombea wao wapigiwe kura.

  Alipotakiwa kutoa ushahidi wa jinsi Rais Kikwete alivyotumia nafasi yake ya urais kushawishi wapiga kura kumpigia kura, alisema wametumia ushahidi wa vyanzo vya umma, ambavyo ni vyombo vya habari na kuwasilisha nakala ya magazeti matatu na kanda za video.

  Kutokana na malalamiko hayo, chama hicho kimemwomba Msajili baada ya kuridhika kuwa Rais Kikwete amefanya vitendo vilivyokatazwa na sheria na kupoteza sifa za kushiriki mchakato wa uchaguzi, jina lake liondolewe.

  Barua hiyo ilisisitiza: “jina lake liondolewe chini ya kifungu 24(1) cha Sheria ya Gharama ya Uchaguzi ya mwaka 2010, kinachosema mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelezwa katika sehemu hii, atakuwa amepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi na uchaguzi”.

  Hata hivyo, Mnyika alisema amewasilisha malalamiko hayo huku akiwa na imani yenye shaka, kwa sababu Msajili ameteuliwa na Rais ambaye wanamlalamikia.

  “Tumempa Msajili malalamiko, wakati tukijua ameteuliwa na Rais na hiki ni kipimo kwake kama atasimamia sheria kwa uhuru, akishindwa tutaeleza kwa wananchi hatua tutakazochukua,” alisema

  Alipoulizwa Tendwa uamuzi wake baada ya kupokea malalamiko hayo Katibu Muhtasi wake, alisema: “Msajili amesema hawezi kuzungumza nanyi leo (jana) ila mje kesho (leo) asubuhi atatoa majibu ya malalamiko haya”.

  Source Habari Leo
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhhhhhh
   
 3. L

  Luiza Gama Senior Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hawa sisi tulisema ni watwanga maji hawana lao, hivi mlipokuwa mkizungumza na kusema majukwaani mlikuwa hamujui kuwa hamna uwezo huo kisheria?


  sasa hamjaingii ikulu mnashindwa kufanya utafiti mambo madogo kama haya jee tukikupeni nchi si mtakuwa bomu kuliko hawa mnaowakosoa?
   
 5. L

  Luiza Gama Senior Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 21, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chadema msipoteze muda.Muda hauwezi kuwasubiri na mnachotakiwa kukifanya kwa kipaumbele ni kukutana na wananchi na kunadi sera zenu kwenye majukwaa.Mkianza kuuliza juu ya ahadi za Kikwete kununua meli mnajipaka matope kwa wapiga kura wa mikoa ya ziwa.Mnapohoji kuongezeka kwa mishahara ya wafanyakazi wafanyakazi hao hao watajiuliza maswali mengi ya kulikoni.

  Kwenye majukwaa nyinyi mgedai kuwa ni kutoka na shinikizo lenu kama Chadema haya mafanikio yasingekuwapo,lakini kinyume cha hayo mnajimaliza wenyewe.
   
 7. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mapungufu ya katiba yetu,ni dhahiri kuwa msajili wa Vyama vya siasa ataipendelea CCM kwani mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye rais ndiye mwenye kumteua msajili. Je,hapo haki itatendeka?
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mpo wengi...!!!

  Au ndo mkutano wa intelijensia na watawala?
   
 9. k

  kandambili2 Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa alikuwa ni mtumishi wa Mungu hapo kale, bila shaka anajua au kukumbuka lile andiko la kibanzi na boriti. Kwamba huwezi kutoa kibanzi kilicho ktk jicho la mwenzio hadi hapo utakapotoa boriti lililo ktk jicho lako.Yeye amekuwa akito ahadi kemkem ooo mara elimu bure,mara nitawapa wafanyakazi kima cha chini cha 350,000. mara kilimo bora.unadhani hizo hazifanani na za JK. Amefilisika kisiasa
   
 10. M

  MWANASHERIA Member

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani nisikilizeni mimi, mimi si ndio mwanasheria? Ni kwamba chini ya sheria ya gharama za uchaguzi, pingamizi za namna hii zinawekwa na msajili wa vyama vya siasa, either kwa yeye mwenyewe kumove au kwa kupelekewa malalamiko na msajili wa vyama vya siasa, lakini kama chadema wangekaa kimya msajili asingelazimika kuweka pingamizi yeye mwenyewe, ila kwa sababu amepelekewa malalamiko, ni lazima ayafanyie kazi. So to say, chadema wamepeleka pingamizi kwa msajili ili yeye alipeleka tume ya uchaguzi.

  suala la msingi ni kwamba, je msajili atapeleka hilo pingamizi, au anatafuta bla blaah za kutudanganya? Sababu anateuliwa na raisi mwenyewe, na hata akipeleka, je tume ya uchaguzi utamtoa kikwete kwenye kinyang'anyiro, coz mwenyekiti wa tume na wasaidizi wake wote wanateuliwa na raisi.
   
 11. m

  mob JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  nimekuja gundua kuwa anachofanya raisi ni kutafsiri bajeti kwa mtazamo mwingine akitoa ahadi kuwa zitafanyika lakini ni wapi anatoa.

  this man is very clever. angalia jana kasema kuwa watanunua bajaji 400. hizi ziko kwenye bajeti ya afya ya mwaka 2010/11 hivyo itakuwa rahisi yeye kushinda mapingamizi yote maana hii imeshatamkwa na kupitishwa na bunge na slaa,zitto wakiwa ndani yake

  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2009/10, katika mkakati wa kupunguza vifo
  vinavyotokana na uzazi, Wizara ilikamilisha taratibu za ununuzi wa pikipiki maalum 400
  kwa ajili ya wajawazito wanapopata rufaa. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau
  ilinunua radio call 40 na magari 12 ya kubebea wagonjwa na kusambaza katika
  Halmashauri za Karagwe, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Nachingwea, Kisarawe, Liwale,
  Ngara, Rufiji, Chunya, Ileje na Sumbawanga.​
  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Wizara itanunua pikipiki 400 kwa
  ajili ya kubebea wagonjwa ili kutekeleza Mpango wa Afya ya Mama na Mtoto. Aidha,
  Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
  Mitaa, itanunua mtambo wa kujenga Zahanati kwa gharama nafuu ​
  (Ultimate Building
  Machine – UBM)

  nawatakia kampeni njeme kwa maendeleo ya taifa yetu.amani na upendo uwe pamoja nanyi

   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hawa wanajigamba ni watu wa utafiti, na si wakurupukaji.


  ila inonyesha wazi kuwa ni wakupukaji na wahuni na ushahidi ni huu, kazi kupepetua midomo tu na wakiujua ukweli huwa kimya.

  ni chama cha wajuaji au wajuvi na si wajuzi
   
 13. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,846
  Likes Received: 11,965
  Trophy Points: 280
  Hebu waeleze wao wanasoma kichwa cha habari na kurukia kujibu bila kuelewa. Kwanza mwandishi kajiuma uma Chadema wameshindwa halafu mwisho kasema anayeweka si Chadema ni Msajili.

  Pingamizi haliwekwi na Chadema wao Chadema wanapeleka malalamiko kwa Msajili ambaye ndiye anauwezo wa kuweka pingamizi na hata Msajili akiweka pingamizi yeye hana uwezo wa kulitolea maamuzi atalipeleka NEC huo ndio utaratibu. Sasa nyie baada ya kuona heading ambayo nayo iko bias basi nyote mnaongozana kama kondoo mtoni bila kudadisi.
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,115
  Trophy Points: 280
  Tbc wazime jf kwa kuruhusu maneno kama haya kwani kwao ni dhambi kubwa...........
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Hapo kwenye red ni kuonyesha hana wazo jipya wala mbinu mpya amezoea kudesa (copy and paste) aangalie asicopy na jina la mtu akadhani nilake....achanganye na zake....
   
 16. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  CHADEMA walisema watamuwekea pingamizi mgombea Urais kwa tiketi ya CCM na sio kumfungulia mashitaka.
  Pingamizi la uchaguzi hupelekwa kwa msajili wa vyama ambae ni Tendwa na mashitaka hufungulia mahakamani ambapo kwenye hii kesi ya CHADEMA sidhani kama kuna suala la kwenda mahakamani.

  Kesi zote za uchaguzi zinaanzia kwa msajili wa vyama na zinaishia kwa msimamizi wa uchaguzi ambako yupo Jaji Lewis Makame. Kesi kama hii ni ngumu sana kuipeleka mahakamani, uchaguzi utasimamishwa hata miaka 3 kama itafika huko.
   
 17. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  unachoongea ni sahihi lakini kama ulikuwepo kwenye kampeni siku ya jmosi ni kwamba ilitamkwa kuwa CHADEMA inaweka pingamizi period. sasa kama walidanganya ni suala lingine.
  lakini naona kuna tatizo hapa, JK katoa ahadi ya meli Bukoba Slaa katoa ahadi ya elimu bure msingi hadi chuo kikuu tofauti ni nini hadi kuwepo na malalamiko??? hata suala la mishahara si lilizungumzwa bungeni?? au ahadi hiyo hiyo inakuwa ok kwa Slaa, na rushwa kwa JK???
  mie bado sijaona mantiki ya malalamiko hayo

  CHADEMA muda unapotea kwa haya malalamiko chanjeni mbuga
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hao mabwege wa HABARILEO wamekurupuka tu na hiyo habari au uelewa mdogo wa mwandishi na mhariri wake ambaye ni mawakala wa JK na ndiye aliyemuweka hapo akitokea Majira. Hata Chadema kwenye mkutano wao walisema watapeleka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye baada ya kupitia ndipo anaweza kuiwasilisha rasmi kwenye Tume ya uchaguzi
   
 19. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Imagine pingamizi la Chadema limepelekwa NEC na tume ikampiga chini JK..:confused2:
   
 20. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli wanasheria wa chadema ni imara na ndio maana wamemuingiza mkeke bwana mdogo John apeleke malalamiko ambayo yapo wazi kabisa kwani hata vyama vingine vinatoa ahadi ya kushughulikia mafisadi na pia kupunguza mishahara ya wabunge na rais,sasa hiyo nini nini?
  Jamani siku zote najua akili ni nywele kwahiyo pale chadema kuna baadhi ya watu wana nywele pungufu au hawana nywele baadhi ya sehemu na ndio maana wamepungukiwa ufahamu wa ahadi za kampeni.Itawabidi warudi shuleni ili kuelimika na si kumaliza madarasa tuu kama walivyofanya.(Ongera bwana Lisu na Marando kwa kulijua hilo!)
   
Loading...