CHADEMA wasaliti - CUF

Kwa kweli, hali yao ni mbaya. Kumbe CUF wanatafuta ushindi wa pili au wa tatu?
 
Kwa namna hii siasa zetu bado. Bora CDM wako serious. They mean business.
 
 
cdm haipo tena wafuasi wake waliokipa kura wamerudi kwenye chama chao ccm, na siku za chadema katika ramani ya siasa za tanzania zinahesabika.
<br />
<br />
ONGEZA ZA KWAKO KIDOGO! SIKU NYINGENE USIKARIRI MASABURI WE!
 
Yaani chadema inapandishwa chati kila uchao. Mtu akihisi wananchi hawamwelewi-ni chadema, akifilisika kisiasa-chadema, wanandoa wasipoelewana-chadema, akidhani atakosa ubunge-chadema. Chadema, chadema, chadema... Pimaneni kwa hoja bana tunawasikia. Mtatiro unataka sub kabla ya game kuanza? Acha hizo.
 
Hivi CCM na CUF si wana ndoa ya Mkeka? au mimi ndio sielewi? au Ndiyo yaleyale ya Mh Tundu Lissu kuwa ya Pwani yabaki Pwani na Bara yabaki Bara? sasa mbona walikuwa wanampinga tena?
 
Mtatiro amejibu hoja za wengi. Sasa mleta hoja hii aliipata wapi? Nini chanzo chake?
 

Huyo ndiye mratibu wa kampeni CUF (Naibu Katibu Mkuu-Bara), hayo makubwa. Yaani tayari ameshakubali kushindwa akimaanisha kuwa wenyewe CUF watakuwa wa pili nyuma ya CCM but mbele ya CHADEMA. Zijabadilisha maneno hapa, angalia mpangilio wa maneno yake hapo kwenye nyekundu.Hafai kuendesha kampeni kama tayari anakiri kuwa watakuwa wa pili.
 

Kama usaliti maana yake ni kugawa kura za chama pinzani basi kimsingi kila chama kinasaliti vyama vingine na ndio maana ya demokrasia kama sikosei. CCM inavisaliti CHADEMA na CUF; CUF inavisaliti CCM na CHADEMA; na CHADEMA inavisaliti CCM na CUF. Kwa hiyo wote ngoma droo kilichobaki ni kila chama kuuza sera zake tu ili mgombea wao akubalike na kuchaguliwa na wananchi.
 
waseme tu kwa sasa ndio kajitokeza mpinzani yaani chadema, coz ccm n cuf ni kitu kimoja
 

Mbona hili halina uhusiano na hoja ya awali ambayo ilihusu uchaguzi wa Igunga?
 
mwanzo wa kushindwa ni malalamiko na kelele ndo kinachoonekana kwa cuf iliyopoteza matumaini na muelekeo wa kisiasa.
 


aligombea ubungo akashindwa vibaya mno. msameheni bado ana maumivu.
 
Kwani
CUF na CDM wana Mahusiano gani hadi huyu Jamaa adai kwamba CDM wanawasaliti?
 
Bora tuwe wakweli Vyama vya siasa havitafika mbali kama havitokuwa na tabia ya kuachiana majimbo. Kama kweli CUF ina nguvu zaidi ya CDM basi CDM waiachie CUF Igunga vinginevyo ni kuwapa CCM ubwete wa kushinda.

Wakuti pole sana maana wewe ni mgeni hapa .Hebu soma kwanza upate kuelewa hoja nyingi kabla hujaanza na lawama kuona kama CUF wana nguvu .CUF ina nguvu Pemba si bara kaka .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…