CHADEMA wanuna Zitto kwenda CUF

CHADEMA wanuna Zitto kwenda CUF

wanafiki wanashindwa kuelewa kwamba CUF,NCCR ,NA CHADEMA ni kitu kimoja ndo maana ya UKAWA.Sasa zitto kwenda CUF siyo kweli ni umbea gazeti la kufungia maandalizi hilo.
 
Wanachokifanya chadema ni kama mwanaume aliyemwacha mkewe then anaanza kumuonea wivu baada ya kuolewa na mume mwingine. Pia inaweza kuwa kinyume chake
CUF wapo ndani ya UKAWA tunajenga nyumba moja hizi porojo za wivu zipo ccm.
 
CHADEMA wana wivu wa kike.
ccm ndo wivu wa kike mnashindwa kuelewa Zitto akienda CUF bado yupo ndani ya UKAWA kazi ya FUTA DELETE CCM NCHI NZIMA inaendelea.
 
CHADEMA wamsamehe Zitto tusiwe na chuki kiasi hiki, tumsamehe bure tu kama baba amrudiavyo mwanawe. Hata kama kakosa vipi lakini bado ni mwanetu wala tusiruhus aendelee kuaibika mitaani.
The guy is our son lets forgv him.

#GOODMORNING
 
Last edited by a moderator:
Huu ni upuuzi ni Vizuri kupuuza gazeti umma. Cdm wana mambo mengi muhimu ya kufanya Chama makini hakiwezi kuhangaika na mtu kama Zitto na walishasema habari ya Zitto imefungwa CDM
 
Mbona hamukuipigia debe habari hii?
? ? ? ?

Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza.

“Kiongozi wa Upinzani Bungeni (Mbowe) ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa bomba la gesi. Pale atakapohitaji msaada wetu tutamsaidia, tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezekana kabisa kuwa zaidi ya Dola ya Marekani 600 milioni (zaidi ya Sh1 trilioni) zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia China mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa kwa uwezo wa Mola,” alisema Zitto.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya kitaifa baada ya kugunduliwa kwa gesi na wao (wananchi) wameonyesha kwamba wakiamua wanaweza kupigania masilahi ya Taifa.

“Mmesimama kidete kuhakikisha utajiri huu hauporwi na haturudii makosa yaliyofanyika Kanda ya Ziwa pale tuliporuhusu madini kuporwa na mabeberu wa kimagharibi,” alisema.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwahutubia wakazi hao, aliwataka viongozi wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa kuongoza kwa misingi ya chama ya haki sawa kwa wote.

“Profesa Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter) hana uwezo wa kuendelea kuwapo madarakani na hapaswi kufumbiwa macho, wote waliohusika na sakata hili lazima wachukuliwe hatua,” alisema.

Kuhusu uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura alisema, “watakapokuja kuwaandikisha jitokezeni hiyo ndiyo njia pekee ya kutafuta ukombozi wa pili wa Taifa hili lakini msipofanya hivyo hatutawaondoa hawa CCM.”
 
kweli chadema wamekosa hoja sasa acha wahangaike na mchawi wao.
 
Kama ambavyo imetabiliwa ktk maandiko, "nyakati za mwisho patatokea manabii wa uongo", hali kadhalika nyakati za kuelekea uchaguzi mkuu (ktk nchi nyingi za kiafrika) hujitokeza vyombo vya habari bandia. OLE WENU ENYI WAANDISHI kwani hakika hamtaikwepa hukumu, ima "The Hegue" au ktk mahakama za "gachacha".
 
This is what we call cheap politics!

CHADEMA na CUF wako kwenye Umoja wa UKAWA.
Watanzania tumeshuhudia jinsi umoja huu ulivyowatikisa CCM kwenye Chaguzi za Serikali za Mitaa. Sasa weye unayetumabia eti CHADEMA wamenuna unataka kutumabia nini kama siyo unafiki na kutaka kuchonganisha watu???

Kufukuzwa kwa ZZK toka CDM hakujakiasili chama hata kidogo. Ijulikane kwamba Zitto Kabwe ndiye anayetamani kurudi CHADEMA baada ya kufukuzwa kwa usaliti. CHADEMA walishasema hawawezi kufanya kazi na mtu kigeugeu, mnafiki, msaliti na ndumila kuwili.

Hii hoja imeletwa na wana CCM ili kutaka kuweka mazingira ya kuwagonganisha CUF na CDM ili waanza kufarakana na pengine kuvunja umoja huu ili CCM waweze kupeta kwenye Uchaguzi Mkuu 2015.

Nawasihi viongozi wa UKAWA msikubali kuingia kwene mtego huu wa kibaradhuli wa kutaka kuanzisha mvurugano ili kupunguza kasi ya UKAWA kuelekea Ikulu 2015.
 
Weka picha ya CDM wakinuna...
 
Wanachokifanya chadema ni kama mwanaume aliyemwacha mkewe then anaanza kumuonea wivu baada ya kuolewa na mume mwingine. Pia inaweza kuwa kinyume chake

CDM wamefanyaje?
 
Hahahaha!
Chanzo: Uhuru

No comment!
 
kwani hapo tatizo ni liko wapi zito ni MP opposition hata kama wana kesi mahakamani. lipumba hakufanya kosa kumwalika na aliamini kumsaidia to clarify some issues ili watu waelewe. mimi nawashauri CDM musihesabu makosa mnayo ona zitto kafanya. kumbukeni wakati wa buzwagi scandal jinsi zitto alivyo fanya kazi ya kujenga chama na marq ngapi zitto aloweka rehani uhai wake kwa maslahi ya chama. Namwamini sana mbowe kuwa ni mtu mwenye hekima sana na ndo maana CDM mmefika hapo mlipo namshauri mbowe atafute namna yq kimaliza mgogoro huu kumfukuza zitto siyo solution hata kidogo

Kwani nini maana ya makubaliano yaani
 
Back
Top Bottom