CHADEMA wanatumia msemo wa Kiingereza "If you can’t convince them, confuse them"

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Hadi dakika za mwisho za kujiuzulu kwa Ndugai wana CCM wengi hawakujua wawe upande upi wa Spika au wa Rais. Ndio maana hadi sasa wabunge wengi wa CCM bado wapo kimya. Kwa upande wa upinzani hasa Chadema wao walichokuwa wanafanya ni kuchochea kuni, kuna waliokuwa wanampaka mafuta Ndugai kwa unafiki na kuna waliokuwa wanataka Rais amfukuze Ndugai. Zitto ndio kabisaa hajatia neno.

Nitazungumzia misemo miwili ya kiingereza inayotumiwa sana na wanasiasa nikiihusisha na vyama vyetu vya siasa vya CCM, CHADEMA na ACT-Wazalendo. Misemo hiyo ni;

“If you can’t fight them join them.” na
“If you can’t convince them confuse them.”

Msemo wa kwanza unakihusu chama cha ACT Wazalendo. Hiki chama ni kichanga hakina mtaji wa wanachama wala resources za kutosha kuweza kumshinda mpinzani wake mkuu ambaye ni ‘chama tawala’ CCM, kikaona heri lawama kuliko fedheha njia ya mkato ni kuungana na mwenye nguvu. Huko Zanzibar kimeungana na serikali na kuunda serikali ya umoja SUK, pia tumeona kinavyoshirikiana na CCM katika mambo mengi likiwemo hili la Maridhiano. Hii inadhihilisha huo msemo wa “If you can’t fight them join them.”

Kwa upande wa CHADEMA ambacho ni chama kikuu cha upinzani chenye wanachama wengi na umri mrefu kulinganisha na ACT, chenyewe kimekataa kuungana na mtesi wao, kimeamua ku fight kwa kuwachanganya CCM wapigane wao kwa wao.

CHADEMA wameanzisha mchakato wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kwa makusudi, leo ndani ya CCM wamegawanyika wengine wanataka Katiba mpya wengine tuanze na Tume Huru, hoja ambazo ilikuwa haramu kuzisikia ndani ya CCM na naona kama Chadema wanafanikiwa kwa kiasi fulani. Kwa mfano Chadema wali fight sana kumtaka Spika ajiuzulu walishindwa kwa sababu CCM walikuwa wamoja lkn baada ya kuwaachia CCM bunge peke yao Ndugai ametoka kwa urahisi sana wakisaidiwa na UVCCM, kwa hoja ya (Mikopo) iliyotakiwa kuwasilishwa na kambi ya upinzani bungeni.

Kwangu binafsi kwa faida ya muda mrefu CHADEMA wamechagua njia sahihi kuliko ACT ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea hisani ya aliyeungana naye. If you can’t convince them confuse them ili baadae wapatikane wa kuwaunga mkono miongoni mwao.
 
CCM imekufa na inasubiri mazishi tu, mazezeta ya CCM yanaiona CCM ni mungu asiyekufa. Samia anadhani nguvu za Dola zitamsaidia kubakia madarakani.

Hajui Kama kuna Mungu,amesahau kilichomkuta mwenzake.
 
Back
Top Bottom