CHADEMA wanatufunza Uzalendo

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,288
9,923
Chadema wanatufunza "uzalendo".

Tafsiri ya uzalendo inaendana na uwezo wa kiakili. Huwezi kuwa mzalendo kama akili haipo sawasawa, uzalendo ni kukipenda kitu chako bila mipaka, bila kujali utachukuliwaje na watu wengine na bila kujali utatafsiriwa vipi na wengine.

Kuna somo wanatufundisha CHADEMA, ukiwaangalia Chadema wa mwaka 2011 kwenye lile vuguvugu la mabadiliko ni walewale hadi leo. Wanaipenda mikakati yao na kuiishi. Hawajawahi kutenganisha uhalifu na Chadema bila kujali chama chao kinatafsiriwa vipi na WANANCHI amabo wanawaomba ridhaa ya kuwaongoza.

Chadema wamepitia mengi mno ya kukatisha tamaa na pengine hata wangeweza kuweka mpira kwapani, lakini hawajawahi kufanya hivyo. Angalia trend ya maisha yao na namna wanavyoweza kuuishi uhalisia wao.

Mwaka 2010 baada ya uchaguzi wa Jimbo la Arusha ambalo lilimweka Godbless Lema madarakani ilikuwa mwanzo wa Chadema kupitia majaribuni, Lema alihudhuria kesi ya kupinga ushindi wake mara nyingi zaidi kuliko alivyohudguria vikao vya Bunge, wanachadema na viongozi wao waliungana nae hadi akashinda. Uchaguzi huo ulimfanya Batilda Buriani kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya baada ya kushindwa kura na Lema. Huo ukawa mwanzo wa mengi kwa Lema.

Sambamba na kupingwa ushindi wake, Lema na wenzake wakiwemo akina Dr Wilbroad Slaa, mkewe Slaa walipitia magumu mengi, unamkumbuka mchumba wa Dr Slaa aliyepasuliwa kichwani katika vurugu za Arusha?

Siku zote Chadema wakutana na mikono ya Polisi kuliko walivyoshambuliana na vyama vya kisiasa. Yaani Chadema na Polisi ilifikia kipindi wakaonana kama Paka na PANYA. Waliwindana, Polisi wakipinga namna Chadema wanavyoendesha siasa zao, lakini Chadema muda wote walisimamia msimamo wao kwamba Polisi wanafanya kazi za CCM na sio za Kipolisi, mwisho Wananchi na wafuasi wao waliendelea kuwaamini. Hamkubuki Polisi walibatizwa jina la Poli_CCM?

Hiyo yote waliiweza kwa sababu ya ushirikiano wao. Unazikumbuka kesi za baada ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni mwaka 2018 uliomrudisha Bwana Mtulia madarakani kupitia CCM? Mbowe, Mashinji, Peter Msigwa, Bulaya, Halima Mdee na wengineo walisota mahakamani na hata kuhukumiwa kulipa faini milioni 350, unakumbuka baada ya kuhukumiwa kulipa faini, wanachama walifanyaje? Waliwachangia, milioni 350 ndani ya saa 72, kila mtu alitoka gerezani.

Achana na hilo, unakumbuka issue ya aliyekuwa Mbunge wa kilombero, Peter Lijualikali, Hadi hukumu yake inasomwa, viongozi wote wa Chadema walikesha mahakamani na michango walichangishana. Unajua kilitokea nini? Mahakama ilimhukumu kifungo Cha chini ya miezi sita. Kuna mambo mengi hufanyika kuhusu hizi kesi za viongozi, moja ni kulinda nafasi yake kama ikitokea atahitaji kuendelea kuongoza, kikatiba ukihukumiwa hukumu ya makosa ya kijinai inayozidi miezi sita unakosa sifa ya kuendelea kuwa kiongozi. Chadema hucheza na hizi hukumu, ndani na nje ya Mahakama ili kulinda "status" za watu wao wenye influence kubwa kwa Wananchi.

Hebu fikiria hili, viongozi wa Chadema waliohukumiwa kulipa faini ya milioni 350 kwa pamoja, ukiangalia kwenye kila kiongozi alihukumiwa kulipa faini ya isyopungua milioni 10 au jela miezi mitano. Linganisha kosa la kulipa faini ya milioni 10 au kwenda jela miezi mitano, inawezekanaje? Ulipe milioni 10 au kwenda jela miezi 5. Kwanini sio miaka kadhaa. Ukigombana na mwenzako mkapigana, ukamtoa damu, utahukumiwa kulipa faini laki moja au jela miezi 12. Angalia hiyo faini fanya relation na matukio ya viongozi wa Chadema ya maandamano yaliyosababisha kifo Cha mwanafunzi aitwae Akwilina. Inaingia akilini?

Chadema wapo smart sana linapokuja suala la ushirikiano. Tofauti na CCM. Chadema mtu wao hawawezi kumuacha mwenyewe, hata kama anaouwezo kifedha, hawamuachi mwenyewe, watashikamana nae hadi mwisho.

Leo Mahakama ya Mbeya imemuachia huru Mdude Nyagali, kabla ya hukumu ya leo, juma lililopita wakati anafikishwa mahakamani kusomewa hukumu, wanachama wa Chadema na viongozi wa juu kabisa katika chama chake, akiwemo Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe alikuwepo mahakamani, just imagine, Mwenyekiti taifa anasafiri kutoka Dar es salaam anaenda Mbeya kusikiliza hukumu ya mwanachama wake, hata kama Mdude angehukumiwa kwenda jela, bado moyoni angesema Chadema ni Bora katika maisha yake na asingejutia maisha ya jela kujihusisha na Chadema, they fought to the maximum.

Leo Mdude Nyagali ameachiliwa Huru, amebebwa kutoka Mahakama ya Mbeya mjini wamezunguka nae mitaani wakiwa wamembeba juu kwa juu. Wakati anaendelea kubebwa juu kwa juu kuna zoezi linaendelea la kumchangia fedha za kuja kuanza maisha baada ya kukaa mahabusi kipindi kirefu, challenge inayoendelea ni ya kumkusanyia walau 10 milioni kupitia ukurasa wa Kaka yangu Malisa GJ, Kuna magroup ya Chaso na ya mpambanaji mwenzao mwingine anaeitwa Masonga.

Hebu fikiria hili Kisha jiulize ni Nani wa CCM amewahi kuchangiwa katika mambo magumu anayoyapitia. Ukiachana na send off, michango ya harusi na kipaimara au birthday, mtu pekee aliyewahi kuchangiwa kupitia CCM ni Hayati Baba wa Taifa kipindi anapigania Uhuru baada ya kupatikana na hatia kipindi Cha utawala wa Waingereza nchini, harambee iliyoendeshwa na akina Bibi Titi Mohammed, hiyo ikiwa ni TANU, kabla hata ya Uhuru wa Tanzania. Inawezekana wenye huo ujasiri walikuja kuzaliwa wakiwa Wapinzani wa CCM, usishangae ndo hao Chadema ya leo.

Wana CCM tutambue kuwa viongozi wetu watokanao na CCM wakifikishwa kwenye vyombo vya dola, watu wa kuwasemea na kuwasaidia ni sisi wenyewe, dola haina Chama. Suala la kesi kuwa mahakamani haimaanishi mtuhumiwa tayari anayo makosa, ni Jambo la kumpigania kwa hali na mali.

Tulijitolea mimi na ndugu yangu Pio Pius kuchangisha chochote kitu tumpambanie mwenzetu, lakini mwitikio ni mdogo mno, haijalishi mwenzetu LENGAI Ole Sabaya anao uwezo wa kuweka wakili ama lah, sisi kama sehemu ya watu wake tumemsaidiaje? Yeye hawezi kufanya mpango wowote kulingana na mazingira aliyopo muda huu, tulio nje ndo watu pekee wa kumpigania, kuna mambo mengi ya kufanya nje ya kumtafutia mawakili, lakini hata kwenye issue ya kumtafutia mawakili tungeunisha nguvu tungeweza kumtafutia wenyewe, yaani wakili ambae anaetafutwa na familia yake angepata Msaidizi wake. Huo ndo upendo ninaoutaka uwepo kwenye Chama chetu.

Kwenye masuala ya kisheria, mawakili hawaendi kutetea tabia ya Sabaya, wanaenda kusimamia vifungu vya kisheria alivyoshtakiwa navyo Sabaya na wenzake, mawakili wanaoenda kusimamia hiyo kesi hiyo wanaenda kusimamia dhidi ya Serikali. Ni battle of interest.

Kama Chadema waliweza kusimama na MDUDE aliyekamatwa na madawa ya kulevya, wakiwa na vizibiti, wameshindwa mahakamani kuthibitisha ikiwa hayo madawa ni ya Mdude au sio yake. Itashindikana nini kwa Mkuu wa Wilaya kuambiwa amefanya uvamizi wa kutumia silaha kuiba Shilingi 35,000 na simu?

Tunaomba mtuunge mkono tafadhali, nawaombeni tena, tuungenj mkono, tutaishangaza serikali na watu waliopo nyuma ya hili.

Abdoulquarim Malisa
 
FB_IMG_1574277425198.jpg
 
Kuna somo wanatufundisha CHADEMA, ukiwaangalia Chadema wa mwaka 2011 kwenye lile vuguvugu la mabadiliko ni walewale hadi leo. Wanaipenda mikakati yao na kuiishi. Hawajawahi kutenganisha uhalifu na Chadema bila kujali chama chao kinatafsiriwa vipi na WANANCHI amabo wanawaomba ridhaa ya kuwaongoza.

Chadema wamepitia mengi mno ya kukatisha tamaa na pengine hata wangeweza kuweka mpira kwapani, lakini hawajawahi kufanya hivyo. Angalia trend ya maisha yao na namna wanavyoweza kuuishi uhalisia wao.
 
Ukitaka kujua nguvu ya CHADEMA waulize Vodacom kwanini hawakutoa gawio kwa wanahisa mwaka huu.

Ile operation vunja laini ya voda iliwashusha Vodacom japokuwa hawakutaka kukiri ukweli.
 
Back
Top Bottom