Umejieleza sana but nilitaka kuona hitimisho lako ni la aina gani.
Udikiteta umetamalaki idara zote za nchi.
Waliopotezwa, waliouawa, waliopigwa risasi, waliofunguliwa kesi za uchochezi, waliojeruhiwa wakabaki vilema wote walikutwa na hayo wakiipigania haki yao na ya kwako pia wakipinga udikiteta ktk nchi yao na kutaka haki itendeke.
Ikiwa mtu kafikwa na hayo wewe ulitaka yamfike yapi ili ujidhihirishe kuwa ni mpambanaji.
On my side naipongeza upinzani kwa jitihada zao kwani yanayofanyika sasa hata Idd Amini Dada nahisi hajawahi yafanya.
Unyama wa serikali hii ni grade wanu duniani. Aliyofanyiwa Dr Shika na watesaji urusi wamefanyiwa wenzetu tayari ktk nchi hii.
Sina imani na ccm, sina imani na viongozi wake maana wanayoyafanya hata shetani anawashangaa.
Angalia kifo cha mawazo, mwangosi, maisha ya kibiti, aliko saanane, ya mbowe kuharibiwa bustani, kukomeshwa kwa fao la kujitoa, maslahi ya watumishi, maisha ya wakulima, gharama za elimu hakika napata kinchefuchefu kusikia neno ccm na kuona vazi la kijani(kumradhi watani zangu yanga).