CHADEMA wanaingilia Ngome ya CUF - Mtatiro

CHADEMA wanaingilia Ngome ya CUF - Mtatiro

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katika hali ya kushangaza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro amesema CHADEMA kufanya maandamano na Mkutano Temeke Mwisho ni kuingilia ngome yao.

Akizungumzia mwaliko wa CHADEMA kuitaka CUF kushiriki mapokezi ya wabunge wa upinzani kesho na hatimaye kushiriki mkutano wa pamoja Mtatiro amesema kamwe CUF haiwezi kushirikiana na CHADEMA.

Mtatiro amesema mwaliko wa CHADEMA ni wa kisanii na wamegundua Temeke ni ngome kuu ya CUF kwa hiyo CHADEMA haiwezi kupata watu mkutanoni bila kuishirikisha CUF.Mtatiro ameuliza tangu lini Chadema imegundua CUF siyo CCM B? Mtatiro amelalamika CHADEMA inatafuta umaarufu Temeke kupitia mgongo wa CUF.

Kwa upande wake Chama cha NCCR Mageuzi kupitia Katibu Mkuu Sam Ruhuza kimesema kitashiriki kikamilifu mapokezi hayo kwani CHADEMA siyo adui yao bali adui yao ni CCM tu.

Wabunge wa CHADEMA na NCCR waliungana pamoja bungeni kupinga uonevu,ukandamizaji na udhalilishaji wa Spika wa bunge Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai dhidi ya Upinzani bungeni.Hata hivyo mara zote CUF wamekuwa wakiungana na wabunge wa CCM kuwapinga wapinzani wenzao.

Kesho Jumapili CHADEMA imepanga mapokezi makubwa na maandamano kisha mkutano mkubwa wa hadhara Temeke Mwisho kwa lengo la kulaani ukandamizaji wa Spika na Naibu wake.

Source:Tanzania daima/Nipashe.
 
Sasa ngoja kesho, Mtatiro na ccb yake watashuhudia kama kweli Temeke Mwisho ni ngome yao au la! Kimbunga kinakuja, na kitang'oa Magamba na CCM B.
 
Sasa ngoja kesho, Mtatiro na ccb yake watashuhudia kama kweli Temeke Mwisho ni ngome yao au la! Kimbunga kinakuja, na kitang'oa Magamba na CCM B.

Mtatiro anapaswa kujua kwamba kwenye uchaguzi mkuu uliopita mgombea ubunge wa Chadema Temeke alizoa kura zaidi ya 20,000
 
TMK sio Pemba muzee, hata huko Pemba tunakuja kuwashika, Lindi-Mtwara tumeshawashughulikia, Tanga tumeshawazika, Tabora ni historia, bado Pemba huko ndo tunaenda kuwafuta kabisa kwenye uso mwa dunia. M4C kanyaga
 
Mtaa wa Tiro bwana, wakati anasema hayo alikua ameisha kula ule mchicha wa Tarime nini? Mbona sioni kabisa mantiki ya kwanza kukataa mwaliko huo halafu pia kutoa statement za kijinga hivyo, wakazi wengi wa Dar ni wa kuhama hama, leo Temeke, kesho Kinondoni mara Ilala, kama issue ni ngome, mbona hasemi chochote kilichotokea Mtwara? CDM pia walilitenga huko na kupata mapokezi makubwa na mazuri tu, hiyo nayo si ni ngome yao, au?
 
Huyu Mtatiro naye anajiita kiongozi wa chama cha upinzani.

Kila wakati yanaulizwa maswali ya kuwa kwa nini vyama vya upinzani havishirikiani. Sasa chadema kama chama kikiuu cha upinzani kimeonesha njia kwa kuvialika vyama vingine vidogovidogo kikiwemo CUF, then Mtatiro anakataa.

Anazidi kuwaaminisha watanzania wachache ambao walikuwa bado hawajaamini kuwa CUF ni ccm B.

Pole sana Mtatiro. Kama unadhani kuwa temeke ni ngome ya ccm B, then subiri hiyo kesho uone.

Onyo kwako: Si kila kwenye wataalam wa ilim akhera basi ni ngome ya cuf. Kama bado mna mawazo hayo, basi endeleeni kusubiri.
 
Hivi Mtatiro nae wameanza kulewa pombe wanayokunywa ccm? Hivi ni katika andika gani nitakuta kuwa temeke ni ngome ya cuf? Naona kijana huyu anakoelekea ni kubaya. Uoga mtupu. Sasa na kuanzia kesho ndio atagundua temeke ni sehemu ya Tanzania ambako wanaishi watanzania wenye itikadi tofauti. Najua temeke ina majimbo mawili ni wapi kati ya hayo ni la cuf na hata kama lipo wananchi wote pale ni wanachama wao tu?

Kuna wakati niliwahi kujenga imani na huyu kijana Mtatiro lakini kadiri siku zikienda kansa ya ubinafsi na ubaguzi inazidi kumuenea mwili mzima
 
Eti Temeke ni Ngome yao!!!!??? wana wabunge wangapi hawa Manguberi wa CCM hapa Temeke?
 
Bwana maendeleo na shemeji yake hawajazuia maandamano?
 
Nawalaumu CHADEMA kwa kuwaalika hawa CCMb kujiunga nao!!!!
 
kumbe kuna territories eh? sasa mbona cdm hawakuwazuia cuf kwenda arusha? angesubiri cdm waende tmk kisha waaibike kwa kukosa watu, kelele za nini. hao wapinzani wa design ya mtatiro ndio ambao hawaishi kutushangaza sisi ambao sio poloticians. maana tunashindwa kujua hasa lengo lao ktk upinzani ni nini! ni kumpinga mpinzani mwenzio au kupinga chama tawala!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom