Watu wengi hata hapa jamiiforums,walikuwa wakitaka Ludovick atoe UKWELI wa anachokijua kuhusu tuhuma zinazomkabili.amejaribu kuongea kule mabadiliko,tena hakuzungumza chochote juu ya kesi iliyo mahakamani.kila alipoulizwa swali,linalohusu mambo ya kanda ya lwakatare,alikataa na kusema hilo liko mahakamani.sasa tatizo limetokea.mawakili wa lwakatare,kwa kuhofia kuwa sasa ludovick anaweza kusema hadharani ukweli wa sakata hilo,Wamekimbilia kuomba mahakama imfunge ludovick mdomo.
Mimi ni wakili,na nilikuwepo mahakamani,wakati wakili mwenzangu anawasilisha malalamiko yake dhidi ya ludovick.ukweli kabisa,gazeti la mtanzania walilolipeleka mahakamani kama ushahidi,halikuwa limeandika chochote kinachoingilia kesi ya mahakamani,na wala mahojiano ya ludovick aliyoyafanya na mabadiliko,hayakuwa yanaingilia mahakama.nimeyasoma yote mawili.sasa wakili mwenzangu nyaronyo,akamdanganya hakimu,na kulalama kuwa jamhuri inahusika kupanga njama hizo ili ludovick aseme hicho wanachokiogopa chadema.
Baada ya kusema hayo,hakimu,bila kusoma gazeti kuona kama kweli kilichoandikwa kiliingilia kesi,wala kutaka kujua kama kweli mahojiano ya ludovick na mabadiliko yaliingilia mahakama,ndipo akatoa onyo alilolitoa kwa ludovick,na magazeti yenyewe.Binafsi nilimsikitikia ludovick kwa kuwa alifokewa tu kama mtoto, mdogo,wakati hakimu hakusoma gazeti liliandika nini.nikatamani kama ludovick angekuwa na mwanasheria,asingeonewa vile.
Kutokana na hayo,hata waandishi waliokuwepo,walisikiliza maoni ya nyaronyo huyohuyo,aliyepika uongo mahakamani na ndicho walichoandika leo.Nilimsikia Nyaronyo akiongea na mke wa lwakatare kuwa walitaka wasababishe dhamana ya ludovick ifutwe ili arudishwe gerezani,asije akaamua kutoboa kila kitu nje ya mahakama.isingekuwa huruma ya hakimu katemana,ludovick jana angerudishwa lupango.ikumbukwe kuwa chadema wameshaiaminisha jamii kuwa mkanda ule siyo halisi na umetengenezwa,na sasa wanawasiwasi kuwa ludovick anaweza kuwaharibia.
Isipokuwa chadema wamekuwa mabingwa wa kulaumu kuwa mahakama zimekuwa zinatumika kuziba watu midomo.sasa ni ajabu katika hili wao ndiyo wamekimbia mahamani kumziba ludovick mdomo.hatimaye,napendekeza ludovick apate wakili,kwani kwa nia hii ya chadema,wanaweza hata kutengeneza au ka hack e mail yake na kuandika kama yeye ili arudishwe lupango.kwa kweli nimemhurumia sana ludovick,ama hakika chadema ni wanafiki.