Mimi ni kati ya watu nisiyopenda propaganda za kijinga.Nani anaweza akaamini kuwa CHADEMA walipata watu umati wote huu jana wakati mtu mmoja alikuwa ameshauawa na wengine kujeruhiwa mchana huohuo? tuache kudanganyana hapa,CHADEMA wametengeneza hii picha siyo halisi.kama kweli watu wamejaa hivi baada ya mauwaji basi chama hiki kipo mioyoni mwa watu na hakuna atakaye kizuia.Hata hivyo msimamo wangu mpaka nitakapopata ushahidi mwingine ni kuwa picha hii chadema wameichakachua tu MasalaKulangwa
Huamini picha? Au huamini kuwa pamoja na kazi mliyofanya watu bado walikwenda kupata ujumbe wa ukombozi?
Ushauri tu, nadhani sasa utajifunza kuwa kuondoa uhai hakurudishi nyuma dhana ya ukombozi. P.W. Botha aliua wengi, lakini wengi zaidi walijitokeza na akashindwa.
Nina uhakika mabadiliko yamekuja ni watu kusoma majira na nyakati vinginevyo mtakuja kutuambia hapahapa. Mwenye masikio na asikiye maneno haya ninayoandika hapa leo. Kama kuna mtu anataka kuwa mwanasiasa nampa ushauri wa bure aingie CDM mapema kabla ya milango haijafungwa.
Jamani yule mwanamziki wa zamani lemi ongala aliimba,
ukiwamtenda mabaya huishi kulalamika(kalola)
maana yake ndo naiona kwa magamba,wanagombana mpaka na picha duh!