SI KWELI PreGE2025 CHADEMA wameanza kutoa fomu za uchaguzi

SI KWELI PreGE2025 CHADEMA wameanza kutoa fomu za uchaguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
CHADEMA07JUL2025.jpg
 
Tunachokijua
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kimekuwa kikiendesha ajenda inayojulikana kama 'No reforms, No election' yenye lengo la kuhamasisha na kuchochea kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na wenye haki ili kuepusha malalamiko yaliyotokana na mapungufu yaliyojitokeza katika chaguzi zilizopita. Kupitia ajenda hiyo mara kwa mara, chama hicho kimekuwa kikisisitiza kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi.

Mnamo tarehe 06 Julai 2025 baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook walisambaza kipeperushi chenye muonekano wa gazeti kinachotumia jina la 'Mlipuko wa Volkano' kikiwa na taarifa liyoandikwa kwa wino mzito ikisema 'CHADEMA sasa kuanza kutoa fomu za uchaguzi'


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli, kwani hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na uongozi wa CHADEMA juu ya kuanza kutoa fomu kwa watia nia wa nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Aidha tarehe 30, Juni 2025, makamu mwenyekiti wa CHADEMA John Heche alizungumza alitoa hotuba, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia mambo yanayoeneldela nchini ikiwemo kupotea kwa watu, kutekwa na mwenenndo wa hali ya uchumi.

Heche alibainisha kuwa serikali inatamani viongozi wa chama hicho waende kusujudu kwao lakini wao wamekataa. Pia amesisitiza kuwa wamekataa kushiriki katika uchaguzi usio sawa na wa haki

“Tumekataa kuwa sehemu ya uchaguzi wenye unajisi. Tunaisihi serikali na tunaendelea kuisihi serikali ifanye mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi“Tumekataa kuwa sehemu ya uchaguzi wenye unajisi. Tunaisihi serikali na tunaendelea kuisihi serikali ifanye mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi”

Rejea hapa kuanzia dakika ya 19


View: https://youtu.be/DFoDqrsfFS4?si=de6wjYmQ2m86UanS&t=1155
hahahahaha
maFISIEMU mwaka huu hadi mseme
mbona hapo hanjasema bado
 
Back
Top Bottom