CHADEMA wameamua kutembea na udini, hawapo salama

Michael Uledi

Senior Member
Mar 29, 2023
132
322
George Michael Uledi.
Kyela, Mbeya.
July 23,2023.

CHADEMA wanafanya kila linalowezekana kutaka kuipasua nchi kwa sasa, walianza na ajenda mbaya ya Uzanzibari na Utanganyika bahati mbaya watu wameikataa katakata hasa kwenye suala la Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa DP World.

Bahati mbaya kwenye hilo wameshindwa kabisa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Uzanzibar na Utanganyika. Baada ya kuona ajenda hiyo haina mashiko kwa watu ukizingatia baadhi ya Viongozi wa Juu wa CHADEMA kama Salum Mwalimu anatoka Zanzibar, hivyo ajenda hiyo ingeweza kupasua chama chao katika pande mbili za Bara na Visiwani.

The next agenda setting at ajenda ya Udini kwa kutaka kuwagawa Watanzania kwa msingi wa Udini. Angalia list ya wasemaji wao wa leo pale Temeke Viwanja vya Buriaga. Wachungaji na Maaskofu wamepangwa na wao wakapangika kwelikweli bila kujali wajibu wao kwa Taifa wajibu wa kusimamia Umoja wa Kitaifa na amani ya Nchi hii.

Yaani Maaskofu wameamua kutumika na CHADEMA kutaka kuwagawa Watanzania kwa dini zao? What if Zitto Kabwe na yeye akaamua kuitisha Mkutano wake wa ACT-Wazalendo kwa kumua kuwaita Masheikh na viongozi wengine wa kiislam kwa lengo la kuusemea Mkataba wa Bandari na DP World Dubai, itakuwaje? Hapo vipi?

Hizi movement za CHADEMA na watu wao kamwe hazipaswi kufumbiwa macho hata kidogo. Mpaka leo hii, hakuna Askofu wa Sheikh ambaye kasimama kwenye Jukwaa la Siasa la CCM kuanza kuutetea Mkataba huu na CCM inafahamu implications za maamuzi hayo kwa Taifa letu.

Hivi CHADEMA wana ajenda ipi kwa watu wao? Je, ni Katiba Mpya, Udini au ni Ubara na Uzanzibar? Vyombo vya Ulinzi na Usalama na hata mabaraza ya Vyama vya Siasa Nchini vinapaswa kuchukua hatua haraka sana hasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Soon jamii ya Watanzania pia itaanza kuwadharau watu wa dini kwa kuwa sehemu ya wanaharakati wa Siasa za Bandari. Siasa za Bandari hazijaanza leo Duniani, tuache ushamba.

Bunge la Congress la Marekani liliwahi kuikataa Kampuni hiyo hiyo ya DP World Dubai kuwekeza kwenye Bandari zake kwa sababu za kisiasa na sababu za kiulinzi. DP World Dubai sio mara ya kwanza kupingwa hapa Tanzania na huko kwingine ishu haikuwa ubovu wa Mkataba la hasha.

Mwaka 2020 Bunge la Somalia lilivunja Mkataba wa IGA na DP World Dubai kwa sababu ya Siasa za Bandari wala sio jipya kwa watu ambao wanafatilia masuala haya ya Uwekezaji wa Bandari. Wakati Wabunge wa Bunge la Congress wanapinga Uwekezaji wa DP World Dubai Nchini Marekani hakukuwa na matumizi ya Maaskofu wala Masheikh kwenye Mikutano ya Kisiasa.

Haya mambo ya udini ya CHADEMA yanatoka wapi sasa? Mkutano wa Buruaga Temeke leo unapaswa kufutwa, kwani hauna maslahi kwa Taifa langu la Tanzania.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
George Michael Uledi.
Kyela,Mbeya.
July 23,2023.

Chadema wanafanya kila linalowezekana kutaka kuipasua Nchi kwa sasa,walianza na ajenda mbaya ya Uzanzibar na Utanganyika bahati mbaya watu wameikataa katakata hasa kwenye suala la Uwekezaji wa Bandari ya Dar es salaam kwa DP World Dubai.

Bahati mbaya kwenye hilo wameshindwa kabisa kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Uzanzibar na Utanganyika.Baada ya kuona ajenda hiyo haina mashiko kwa watu ukizingatia baadhi ya Viongozi wa Juu wa Chadema kama Salum Mwalimu anatoka Zanzibar hivyo ajenda hiyo ingeweza kupasua Chama chao katika pande mbili za Bara na Visiwani.

The next agenda setting att ajenda ya Udini kwa kutaka kuwagawa Watanzania kwa msingi wa Udini.Angalia list ya wasemaji wao wa leo pale Temeke Viwanja vya Buriaga.Wachungaji na Maaskofu wamepangwa na wao wakapangika kwelikweli bila kujali wajibu wao kwa Taifa wajibu wa kusimamia Umoja wa Kitaifa na amani ya Nchi hii.

Yaani Maaskofu wameamua kutumika na Chadema kutaka kuwagawa Watanzania kwa dini zao?What if Zitto Kabwe na yeye akamua kuitisha Mkutano wake wa ACT-Wazalendo kwa kumua kuwaita Masheih na viongozi wengine wa kiislam kwa lengo la kuusemea Mkataba wa Bandari na DP World Dubai,itakuwaje?hapo vipi?

Hizi movement za Chadema na watu wao kamwe hazipaswi kufumbiwa macho hata kidogo.Mpaka leo hii,hakuna Askofu wa Sheikh ambaye kasimama kwenye Jukwaa la Siasa la CCM kuanza kuutetea Mkataba huu na CCM inafahamu implications za maamuzi hayo kwa Taifa letu.

Hivi Chadema wana ajenda ipi kwa watu wao?Je,ni Katiba Mpya,Udini au ni Ubara na Uzanzibar?Vyombo vya Ulinzi na Usalama na hata mabaraza ya Vyama vya Siasa Nchini vinapaswa kuchukua hatua haraka sana hasa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Soon jamii ya Watanzania pia itaanza kuwadharau watu wa dini kwa kuwa sehemu ya wanaharakati wa Siasa za Bandari.Siasa za Bandari hazijaanza leo Duniani,tuache ushamba.

Bunge la Congress la Marekani liliwahi kuikataa Kampuni hiyo hiyo ya DP World Dubai kuwwkeza kwenye Bandari zake kwa Sababu za Kisiasa na sababu za kiulinzi.DP World Dubai sio mara ya kwanza kupingwa hapa Tanzania na huko kwingine ishu haikuwa ubovu wa Mkakaba lahasha.

Mwaka 2020 Bunge la Somalia lilivunja Mkataba wa IGA na DP World Dubai kwa sababu ya Siasa za Bandari wala sio jipya kwa watu ambao wanafwatilia masuala haya ya Uwekezaji wa Bandari.Wakati Wabunge wa Bunge la Congress wanapinga Uwekezaji wa DP World Dubai Nchini Marekani hakukuwa na matumizi ya Maaskofu wala Masheikh kwenye Nikutano ya Kisiasa.

Haya mambo ya udini ya Chadema yanatoka wapi sasa?Mkutano wa Buruaga Temeke leo ubapaswa kufutwa kwani hauna maslahi kwa Taifa langu la Tanzania.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Sasa wale wa chadema af ni waislamu unawashauri je?
 
Yaani sio kutumia tu kete ya Udini kwenye huu uporaji wa bandari, hata mkienda kutolea tamko huko Makka kuhusu mkataba wa bandari, bado hamtutoi kwenye reli. Mkataba wa bandari ni mbovu, hilo halina mjadala. Muislamu anayetaka kwenda kuongea kwenye huo mkutano aende, ama vipi waitishe mkutano wao. Lakini hakuna atakayeacha kuweka wazi mkataba wa hovyo leo kisa mtasema kuna wakristo wengi. Kama hao viongozi wa kiislamu wameamua kutoshiriki hilo ni juu yao.
 
Tusijisahalishe zile hoja za msingi jamani....,

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Kwamba waislamu wanauunga mkono Mkataba wa hovyo?

Hiyo ni counterpropaganda ya hovyo.

Hoja zijibiwe kwa hoja siyo ushuzi huu
 
Hawa makuwadi wa DP-World kumbe wapo wengi tu, sasa wameibukia na Udini baada ya lile la ubaguzi yaani uZanzibari na uTanganyika kugonga kisiki.
 
Uledi, ungepunguza upumbavu ubaki japo na akili kdg kichwani kuliko kuwa mpuuzi kwa 100%
Issue hapa ni kuuzwa kwa bandari na sio mambo ya dini!
Kumbuka haya ya udini yanakuzwa na CCM ambayo ndio mharibifu mkubwa wa ustawi wa nchi hii!
Nakushauri uwe unakaa kimya kuficha ujinga kuliko kutambulisha upuuzi wako hadharani!
 
Back
Top Bottom