CHADEMA vs Serikali ya CCM

Mafwi Munda

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,750
1,599
Je, huu ndio mwanzo wa mwisho wa ccm?! Tunaona wananchi wanaichoka CCM sasa inatetewa na kila chombo cha dola na vyenye kutoa maamuzi.

Msajili wa vyama, tume ya uchaguzi, polisi na mahakama vyote vime side na ccm. Sasa makosa ya Serikali wanataka yatumike kuihukumu CHADEMA.

Wanaanza kusema CHADEMA ifutwe ili kuiondolea CCM upinzani. Wameona CCM imeshindwa kujitetea yenyewe sasa wanatumua vyeo vyao walivyopewa na mwenyekiti wa ccm kuimaliza CHADEMA.

Wote walioteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa wanajitoa akili kutaka kuiangamiza chadema, msajili wa vyama vya siasa, mwenyekiti tume ya uchaguzi, IGP, DED na majaji wa Mahakama wote wanaitafutia CHADEMA makosa.

Hii haitakuwa haki kwa CHADEMA kuhukumiwa na mpinzani/hasimu wake kisiasa. Wakitaka kuihukumu chadema walete chombo huru kisicho na maslahi yoyote kisiasa Tanzania.
 
Na ikiwa ccm na serikali wamevunja katiba nao wafutwe?!
CHADEMA wanatafutwa kufutwa na kila chombo cha dola na hata ccm wanaunda serikali ndio mpango wao kuondoa ushindani dhidi yao. Kama wanataka haki waruhusu chombo cha nje kilicho huru kisicho na maslahi yoyote ndani ndicho kisimamie chaguzi zote na uendeshaji wa shughuli za siasa nchini.
Tofauti na hapo chadema hawawezi kupata fair trial kwa namna yoyote.
Hao ccm mwenyekiti wao ndiye rais na ana control vyombo vyote vinavyotumika kuikandamiza chadema, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa, polisi, mahakama.
Sasa chadema atahukumiwaje na mpinzani wake halafu utegemee apate fair trial?!
Huo ni uonevu kuihukumu chadema wakati serikali nzima haiwatendei haki.
We have laws in this country but no justice
 
Back
Top Bottom