CHADEMA: Uvumilivu sasa basi


Medical Dictionary

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Messages
1,052
Points
1,195
Medical Dictionary

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2012
1,052 1,195
• WASEMA WIZI WA KURA SASA MWISHO na Mwandishi wetu WAKATI kauli ya Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka
viongozi na wanachama wa chama hicho kuacha
kulitegemea Jeshi la Polisi katika kukabiliana na
wapinzani wao ikiibua upya machungu ya mauaji
ya raia, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema uvumilivu wake umefika
kikomo. Badala yake CHADEMA kimesema kitachukua hatua
zote za kulinda haki zake za msingi, ikiwemo uhuru
wa kuendesha mambo ya siasa kwa mujibu wa
katiba na sheria na zaidi kupambana na hujuma
zote, zikiwemo za wizi wa kura wakati wa
uchaguzi. Msimamo huo ulitolewa juzi usiku na Mbunge wa
Ilemela, Ezekiel Wenje ambaye alisema CHADEMA,
kimevumilia vya kutosha kile alichokiita
unyanyasaji, uonevu na wizi wa kura ambao alidai
umekuwa ukifanywa waziwazi na viongozi wa CCM
katika chaguzi kadhaa hapa nchini. Akizungumza katika kipindi cha ‘Malumbano ya
Hoja' kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV,
Wenje alisema viongozi wa CHADEMA wamejitahidi
kwa muda mrefu kuwa waungwana na
kulazimishwa kukubali udhalimu huo kwa nia ya
kuokoa nchi isiingie katika machafuko. Huku akiungwa mkono na washiriki wengine wa
mdahalo huo, Wenje alisema serikali imekuwa
ikitumia vibaya madaraka yake na rasilimali za nchi
kukandamiza vyama vya upinzani, ama wale wote
wanaoonekana kuwa mstari wa mbele kuikosoa. "Kuanzia sasa hatutakubali tena uonevu huu.
Wapinzani wameibia kura zao waziwazi, na
tunapojaribu kusema ukweli, tunashambuliwa na
kupigwa. "Hakuna amani katika nchi inayoendeshwa kwa
uonevu, maana demokrasia ya kweli ni kutenda
haki na usawa kwa wote," alisema Wenje. Alidai kuwa CCM wamekuwa wakichelewesha kwa
makusudi na kuamuru kutangazwa kwa matokeo
yaliyochakachuliwa katika sehemu ambazo inajua
imeshindwa vibaya, jambo ambalo limesababisha
vurugu, maandamano na hata watu kupoteza
maisha. "Wakati katika uchaguzi wa Marekani matokeo
yote yalitangazwa kikamilifu, utashangaa kuona
pale Ilemela, msimamizi wa uchaguzi alishikwa
kigugumizi kutangaza matokeo kwa siku tatu,"
alisema. JK kikaangoni Mbali na msimamo huo uliotolewa na Wenje,
CHADEMA pia kimemshukia Rais Kikwete na
kumtaka awawajibishe mara moja maofisa wa
serikali waliohusika kutekeleza amri za viongozi wa
CCM za kuwapiga na kusababisha vifo vya
wananchi. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana,
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA,
Wilfred Lwakatare amesema kauli ya Kikwete mjini
Dodoma wakati akifunga mkutano mkuu wa CCM,
imebainisha na kuweka wazi kuwa vyombo vya
dola viliwakamata, kuwatesa na kuwaua wananchi hususan viongozi na wanachama wa upinzani kwa
amri ya chama tawala. Lwakatare alisema hoja ya Rais Kikwete ni jibu
tosha kwa Watanzania kwamba CCM imekuwa
ikilitumia Jeshi la Polisi kutimiza matakwa yao
kisiasa. "Kwa kuangalia muktadha wa mtiririko wa matukio
ya kudhibiti upinzani kwa kuvuruga kazi za kisiasa
za vyama vya upinzani yanayofanywa na vyombo
vya dola, kwa kuua Watanzania wasiokuwa na
hatia, kauli hiyo ya Kikwete imetufikisha kwenye
kilele cha ushahidi kuwa Jeshi la Polisi linatumika kisiasa kukabiliana na hoja na shughuli halali za
kisiasa zinazofanywa na CHADEMA. "Kikwete amethibitisha pasi na shaka kuwa CCM
waliwatumia polisi katika kumuua kijana Ally
Singano Zona wakati wanachama na wapenzi wa
CHADEMA walipofanya mapokezi ya viongozi wao
wa kitaifa Agosti 27, 2012, mjini Morogoro," ilisema
sehemu ya taarifa ya Lwakatare. CHADEMA pia kimedai kuwa kauli hiyo ya Kikwete
imefumbua fumbo la kwa nini polisi mkoani Iringa,
chini ya usimamizi wa RPC Michael Kamuhanda
waliamua kutumia nguvu kubwa kuingilia shughuli
halali ya CHADEMA kufanya mikutano ya ndani,
ikiwemo ufunguzi wa matawi katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa, na hatimaye wakamuua
mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, Septemba
2, 2012. "Kwa kuangalia mtiririko wa matukio ya huko
nyuma kama ambavyo tumewahi kuyatolea kauli
na taarifa huko nyuma na kuangalia ripoti za
uchunguzi wa tukio la Nyololo, hasa uchunguzi
uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania na Tume
ya Utawala Bora na Haki za Binadamu (TUBHB), sasa ni wazi kila mmoja anaweza kuona kulikuwa
na kila aina ya dalili ya maelekezo ya kisiasa
kutumia polisi kuidhibiti CHADEMA. "Kikwete pia amewasaidia Watanzania kuanza
kutafuta majawabu kwa nini watuhumiwa wa kesi
ya mauaji ya aliyekuwa Kiongozi wa CHADEMA, Kata
ya Usa River, Msafiri Mbwambo, ambao katika
tuhuma zao walishirikiana na viongozi wa CCM
kuua, waliweza kutoroka mikononi mwa polisi na hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa,"
alisema Lwakatare. Pamoja na kukumbusha vurugu za Ndago huko
Iringa, CHADEMA kimezidi kudai kuwa kauli ya
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete imefumbua
fumbo juu ya mazingira ya utata yanayozunguka
kifo cha kada wa CHADEMA, Mbwana Masoud,
kilichotokea Igunga baada ya uchaguzi mdogo, aliyekutwa ameuawa kinyama baada ya kutekwa
na kuteswa na vijana wa CCM waliopewa mafunzo
ya kufanya kazi hizo katika makambi ya Ulemo,
Iramba, Singida. "Upo uthibitisho mkubwa, kuwa CCM kimeingiza
silaha za moto bila kibali na kuwapatia vijana wake
katika mafunzo kwenye makambi maeneo
mbalimbali nchini. "Tangu utolewe ushahidi huo, kwa kutaja aina ya
bunduki, namba yake, uwezo wa kubeba risasi na
ilikotengenezwa, mbali ya polisi kushindwa
kufanya uchunguzi ili kuwaambia Watanzania kwa
nini CCM wanaingiza silaha nchini, Mwenyekiti wa
CCM, Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, ameshindwa kutoa ufafanuzi wowote, hali ambayo
inahatarisha ulinzi na usalama wa nchi," alisema. Lwakatare alizidi kuishambulia kauli ya Rais
Kikwete akidai imefunua ukurasa mpya wa kilele
cha ushahidi wa namna ambavyo kuna ushirika
kati ya CCM, serikali yake na vyombo vya dola, hasa
Jeshi la Polisi, kushughulikia vyama vya upinzani,
hususan CHADEMA kwa kuteka, kutesa na kuua raia wasiokuwa na hatia, lengo kubwa ikiwa ni
kutimiza matakwa ya propaganda za CCM kuwa
CHADEMA ni chama cha vurugu. Kutokana na hali hiyo, CHADEMA kimemtaka Rais
Kikwete kutekeleza barua ya Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyemwandikia kutaka
matukio yote ambayo vyombo vya dola,
vimetumika kuteka, kutesa na kuua kwa malengo
ya kisiasa ya kupambana na wakosoaji wa CCM na serikali yake, vifanyiwe uchunguzi huru, kwa
kuunda Tume ya Kimahakama/Kijaji ili ukweli
ujulikane na haki ionekane ikitendeka badala ya
kutoa lugha ya kisiasa kwa nia ya kujikosha mbele
ya umma. Aidha, wakati uchunguzi huo ukifanyika,
watuhumiwa wote, wakiwemo viongozi wa CCM,
serikali na watendaji wa Jeshi la Polisi waliokubali
kutumiwa na CCM, hata kuvunja haki za binadamu,
katiba na sheria, wanawajibika kwa wao kujiuzulu
au kufukuzwa kazi na Rais Kikwete.
Source:tanzania daima
 
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
5,380
Points
1,195
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2012
5,380 1,195
Kwa kweli sasa basi. Wasituchezee, wanachukulia poa sana.
 

Forum statistics

Threads 1,295,825
Members 498,404
Posts 31,224,345
Top