Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
Nimekuwa najiuliza kama CHADEMA ndio chama kikuu cha upinzani Tanzania ni dhahiri pia ndio chama kinachochukiwa zaidi na chama tawala kwa siasa za Afrika.
- Hebu jiulize siku Mh.Tundu Lissu alipopigwa risasi 32 Dodoma inaonyesha Mh. Tundu Lissu hakuwa na ulinzi wowote wa chama chake na kama kungekuwa na gari ya walinzi wake basi wasiojulikana wangeweza kujulikana siku ile kwani walinzi wa Tundu Lissu wangepambana na wasiojulikana hata kulifahamu au kulizuia gari lao ingewezekana
- Suala la Mbowe kukamatwa Mwanza
Hili tukio nalo ni ushahidi tosha kuwa siku ya tukio hakukuwa na ulinzi wowote wa CHADEMA kwa mwenyekiti wao kwani kitendo cha jeshi la polisi kuvamia gesti na kujua Mh. Mbowe kalala chumba namba ngapi na kwenda kuvunja mlango na kumchukua kirahisi bila kuambiwa sababu za kumchukua ni ushahidi tosha wa kuwa ulinzi wa viongozi wa chama kikuu cha upinzani upo chini sana.
Kwa matukio hayo mawili CHADEMA mnapaswa kuimarisha idara yenu ya intelijensia kama kweli mna nia ya dhati ya kuwalinda viongozi wenu.
Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app