Takribani vyama vikuu vyote vya siasa Tanzania viko kwenye migogoro ya uongozi wa juu.
Kwa kuanzia; CCM kunafukuta ikiwa inajiandaa kutekeleza dhana yao ya kujivua gamba ambapo viongozi magwiji EL na Chenge wanatakiwa kuondolewa kwenye uongozi.
Huku chama kilichovuma miaka ya 90 CUF kikiwa katika hekaheka za kumbadilisha katibu wake mkuu Seif.
Wakati hayo yakijiri chama cha NCCR-Mageuzi kilichowahi kuongozwa na Mh. Mrema kikiwa kwenye mshikemshike wa kuvuana vyeo tumesikia aliyekuwa Katibu mwenezi wa chama Mh. Kafulila jana kavuliwa cheo hicho huku kukiwa na mipango ya kumuengua mwenyekiti wa chama hicho Mh. James Mbatia.
Je, Chadema wanajifunza nini na wamejiandaa vipi na mageuzi haya yanayotokea?