CHADEMA, ukiona wenzako wananyolewa wewe tia maji!

kauli au maoni ya mtoa mada yana ukweli ndani yake .....Migogoro mingi huanza na jambo moja dogo sana hivyo ni wajibu wa chama kuwa makini sana ktk maamuzi yake

Mfano suala la Posho kwa wabunge linaweza ku tatizo akizingatia kuwa na ndani ya CDM moja kuna mgawanyiko mkubwa kuhusu hizo ingawa wengine hawasemi huwezi jua nyuma ya Shibuda yupo nani na kauli anazotumia ujasili anaupata wapi

Hapa JF tunapeana habari,kuelimishana, kukumbushana, [Kubudishana hii inategemea na jukwaa uliloko ] ni maana kwamba si kila jambo kubisha tu pasipo hoja ya msingi

Ahsanteni
Shibuda awe na wafuasi, huyo ni mropokaji tu.
 
CHADEMA mwendo mdundo hap hakuna chakutia majg wala kupaka sabun zaid zaid 2tatia mafuta meng tena ya kupikia. Cc migogor ya kipuuz kama hiyo hakunaga
 
Nafikiri chadema nao huwa wanapita katika misukosuko hii, cha msingi ni kuangalia namna ya kutatua migogoro
Chama ni wanachama na chama kinaongozwa na vikao kama chama hakifanyi vikao maana yake hakifuati utaratibu iliojiwekea vivyo hivyo na wanachama wake watavunja taratibu. Lakini si mradi vikao tu, viwe vikao vya maamuzi kuendelea kuwa na vikao vya kupeana taarifa bila utekelezaji ni kuruhusu mgogoro ukue, nitatolea mfano wa magamba na CCM, kama NEC ya CCM iliyokaa April ingefikia maamuzi nafikiri leo chama kingekuwa kinazungumzia maeneo mengine, kinachoendelea ni kupeana taarifa tu bila utekelezaji. Kwani mnafikiri CDM hawapati migororo au wako salama? Hapana, migogoro ipo lakini inapotokea ni wepesi wa kuishughulikia, chama kinapounda tume wanachama wake wako makini kufuatilia, huwa wanawasumbua viongozi wao ili wapate updates, kwa vile viongozi wako accessible hadi mitandaoni ni rahisi kwao kupata majibu ya kuridhisha, tofauti na CCM na CUF wala NCCR ni vigumu sana kuwasiliana na say Msekwa au Mkama au Seif au Mbatia. angalau siku za hivi karibuni Nape, January, Mtatiro wameanza kuiga mtindo wa kina Zitto kutolea misimamo mitandaoni.

Mimi nafikiri kinachovisumbua vyama vyetu hadi kufikia viongozi wa juu kulumbana ni mawasiliano. Tujiulize ni muda gani umepita toka Hamad Rashidi amwandikie Lipumba barua huko Marekani, kwanini majibu yake yajibiwe na vyombo vya habari? Nafikiri kama kungekuwa na mawasiliano kati ya Lipumba, Seif na Hamad Rashid CUF isingefikia hapa. Tatizo kwa vyama vyote ni mawasiliano, hatuwezi kuepusha migogoro kwa 100% lakini tunaweza kuipunguza tukifanya vikao vya mara kwa mara lakini viwe vya maamuzi na utekelezaji.
 
Wewe bado unamisemo hiyo ya kizamani, walikuwa wanaweka maji enzi zile za kunyoa kwa wembe, siku hizi saluni kibao zinazotumia mashine za kisasa.PAMBAF.
 
Wewe bado unamisemo hiyo ya kizamani, walikuwa wanaweka maji enzi zile za kunyoa kwa wembe, siku hizi saluni kibao zinazotumia mashine za kisasa.PAMBAF.
Kwa hiyo na wewe unajihesabu umechangia, inaonesha hujui maana ya misemo si ya mitaani yooo man.
 
KATUNI(589).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom