Ha ha haa Mkuu
Nguruvi3, nimepitia uzi huu, duh! Nyakati hizo wana JF walikuwa wana JF kweli kweli na
nguvu za hoja zilitamalaki tofauti na sasa ambapo
hoja za nguvu ndizo zimekuwa fasheni katika mijadala. Asante kwa kutukumbusha wengine wetu tulikotoka...kwa kweli inafikirisha. Hivi Mzee
Mkandara alikuwa na ugomvi gani nawe nyakati hizo?
Mkubwa hata hizo hoja za nguvu zimekuwa hazina miguu wala kichwa.
Kwa mfano, uzi unaanzishwa '' Kwanini tusiwe na chama kimoja'' . Ukiingia kuusoma hakuna hoja yoyote, mada ina mstari mmoja '' ili tuwe kama China''. Ni ngumu sana kuchangia.
Kabla ya hapo kichwa hicho hicho cha habari kingetetewa au kupingwa kwa hoja na mantiki
Viongozi wengi sana ''wamekulia jamvini'' na wakubwa wakiingia ofisini kitu cha kwanza JF kuna trend nini. Jambo hili lilileta ustawi wa jamii, hoja zilifanyiwa kazi vyovyote iwavyo
Mwana wa Nnauye na mradi wa LB7 walifanikiwa kupoteza quality ya mada JF
Hili lina uhakika na mabaki ya LB7 ndiyo tunayosoma kila siku hapa na mada za hovyo sana
Wanakaa na kutafuta 'talk point' kisha kuileta bila kuwa na utetezi wa mantiki
Mfano, hivi kuna elimu ipi bure ikiwa watu wanalipa kodi?
Hilo lilikuwa kwa hasara ya Taifa na Mwana wa Nnauye anapaswa kuomba radhi
Mzee Kinana ni mtu makini sana. Alisoma madhaifu ya CCM hapa akafanyia kazi.
Ni kupitia hilo aliinusuru sana CCM akisaidiana na Mwana wa Nnauye
Ndiyo maana hata siku moja Kinana hakuwahi kupiga dongo JF, unajua alikuwa 'mwenzetu'
Mkuu unakumbuka mawazo kama ya ''treni ya Mwakyembe'', wazo la ring road Dodoma, mjadala wa Katiba, Diaspora, Kibaha-Dar lane 6, shule , afya n.k. ni zao la michango JF!
Hapo hujagusa vita ya ufisadi na rushwa kama UDA ambao eti leo ni vita mpya kabisa!! haha
Mkuu zama zile, leo watu wangedadavua uhusiano wa EL kurejea Lumumba, siku ya msafara wa Ruge! Waliompokea n.k.
Kudhani kuwa JF ikifa ni heri ni ujinga uliopitiliza. Watu makini wangeiacha huru ili wajue jamii inasema nini. Utafiti wa juzi umeonyesha hilo. Wangejifunza kupitia mawazo n.k
Katika makosa CCM inayofanya ni jitihada za kuiua JF. Hata wnaJF wa CCM wanaliona hilo ni wazo bovu sana na chanzo cha Chama kuchukiwa sana, kinaendeshwa na dola
Kwa bahati mbaya hakuna anayeweza kusema tena! CCM ya kupingana bila kupigana haipo
Imebaki CCM ya watu 3! Mwenye, katibu na Mwenezi. Hao ndio CC ndiyo NEC n.k
Kuhusu 'ugomvi' na
Mkandara , hatukuwa na ugomvi kama wanadamu. Tuna ugomvi kuhusu Zanzibar na masuala ya kijamii ambayo Mkandara aliyawekea lens ya udini, hilo tu!
Yeye anaweza kuita red kama pink, yellow kama Orange ndiyo maana hucheza na grey area
Mimi ni color blind, ninaona white or black