Nafikiri hapa ndipo tunapotofautiana, mimi nasema Lowassa kwa sasa ni adui nambari one wa CCM. Ni kweli aliutaka Uraisi kupitia CCM lakini nani kweli anajua kwa uhakika malengo yake? Je yawezekana kwamba moyoni ni kweli alitaka kuleta mabadiliko from within? Kikwete anapewa benefit of doubt, Magufuli anapewa benefit of doubt, kwa nini Lowassa hapewi benefit of doubt kwa tuhuma zozote zile?Mag3; Kujibu swali lako: Lowassa si adui wa CCM. Matamanio ya kile anachokitaka (Urais), ndio chanzo cha mgogoro wa Lowassa na wenzake. Kwa vitu vingine vilivyobaki, CCM na Lowassa ni damu damu.
Hapana, I disagree, Lowassa hakuwahi kuwa Mkuu wa nchi na hakuwahi kuwa kiongozi mkuu wa chama chake, sasa aliwezaje kufanya anayodaiwa kuyafanya bila idhini ya wakubwa wake? Hizo nguvu alizitoa wapi? Pamoja na hayo tayari kasema anazikubali sera na ilani ya Chadema lakini kama ilivyo kwa malowassa-phobia hawako tayari kumpa hata hiyo benefit of doubt, kwa nini?Nafasi aliyoleta Lowassa kwenye upinzani ni kubwa. Lakini inategemea jinsi gani wananchi wataitumia nafasi hiyo. Wakimwachia Lowassa, hakutakuwa na mabadiliko yoyote. Atafanya kama yale aliyofanya akiwa CCM.
Zakumi si kila kinachosemwa humu ni ukweli uliothibitika, zingine ni hisia tu kulingana na utashi wa mchangiaji. Mimi ni katika waliokuwa mstari wa mbele kumkataa Lowassa lakini wakati huo alikuwa bado yuko kundini huko CCM. Sasa ukweli usioweza kupingika ni kwamba katoka, na ushahidi kwamba hawako tena pamoja ni, kwa mfano, uwanja anaopewa Dr Slaa na status quo kumkandia Lowassa. Miaka yote Dr. Slaa hakuwahi kupewa nafasi kama hiyo TBC hata alipokuwa anagombea Uraisi mwaka 2010, kwa nini sasa?Wachangiaji maarufu katika ukumbi huu walituambia kuwa Lowassa ali-sponsor ACT, kuisambaratisha CDM. Lowassa ali-sponsor watu mbalimbali wachaguliwe kuwa wajumbe wa NEC. Na hawa watu ndio waliokuwa wamchague Lowassa kupitia CCM. Leo baadhi ya hawa wachangia wanamkumbatia Lowassa as a game changer.
My two cents;
Wachangiaji wote humu kwenye jukwaa, hakuna hata moja anayeongelea kiini cha matatizo yaliyotufikisha hapa tulipo nacho ni haki. Imefikia mahali wengi mnaona tendo la kukosa haki ama kunyimwa haki ni la kawaida tu kama sehemu ya maisha. Mnachosahau ni kwamba bila haki hakuna amani, haki hujenga ustaarabu na hivyo kuwezesha maisha kuendeshwa kiutaratibu kwa kufuata sheria.
Ukosefu wa haki hustawisha uonevu kwa mnyonge na kumjengea kiburi mwenye nguvu, kiburi ambacho bila kudhibitiwa hufungua milango ya uhalifu wa aina zote. Binadamu kwa hulka yake hakubali uonevu na ingawa anaweza akavumilia uonevu kwa muda, iko siku uvumilivu wake utafikia mwisho. Hakuna kiumbe hatari kama binadamu anapofikia hali hiyo ya kukata tamaa ya maisha.
Watu mnaongea kama vile uwanja wa ushindani kisiasa upo sawa, mnaongea kama vile uchaguzi ujao, kama zilizopita, utaendeshwa kwa uhuru na haki na mnaongea kama vile vyama vyote vitakayoshiriki vina haki sawa na chama tawala. Manongea kama vile hamuishi Tanzania, mnaishi nchi nyingine tofauti...nchi iliyostaarabika na inayoheshimu misingi ya utawala unaofuata sheria.
Siku Dr. Slaa alipoongea, aliondoa mashaka yote yaliyokuwa moyoni mwangu kuhusu kuteuliwa kwa Lowassa kugombea Uraisi na UKAWA kupitia chama cha Chadema. Mwanzoni, pamoja na kutaka CCM iondoke, nilipokea uteuzi huo shingo upande kidogo nikisubiri msimamo wa Dr. Slaa...naam, nilimsikiliza kwa makini sana na baada ya kumsikiliza sikuwa na wasi wasi tena, UKAWA walikuwa sahihi.
Kauli zinazoendelea kutolewa na viongozi na wafuasi wa CCM si kauli za kiungwana, ni kauli za walevi wa madaraka,kauli za waliojawa kiburi na kauli zisizo na chembe cha ustaarabu...naam ndiko walikotufikisha CCM na kama Lowassa atatusaidia kuondokana na kadhia na manyanyaso haya ya miaka 50 naunga mkono. Dr. Slaa nitaendelea kumheshimu lakini kwangu hapa kapotoka.
Sitaki kuingia ndani sana kwenye swala la Dr. Slaa kwani ni moja katika watu niliokuwa na imani kubwa nao lakini kwa kitendo chake ameonesha ama hakuwa tayari kwa mabadiliko au alijiaminisha bila yeye mabadiliko hayawezekani. Ninachoomba ni wananchi wapewe haki na wawe huru kumchagua watakaye. Serikali isitoe upendeleo kwa CCM bali itoe fursa sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki.
Ndugu zangu, gari (Tanzania) limekwama, limegota kwenye tope...Magufuli anataka kulinasua kwa kulisukuma bila kutoka ndani ya gari, Lowassa kavua buti katoka kwenye gari alisukume. Nawaacha na usemi huu, adverse circumstances need desperate measures...kama hakuna upepo wa kusukuma boti, dawa si kusubiri upepo bali ni kupiga makasia. UKAWA wanapiga makasia.
Mag3,
Unayosema kuhusu haki ni kweli kabisa. Amani ina ingredients zake, na ya muhimu zaidi ni haki. Mchango wako umeenda kidogo nje ya msururu wa michango ya hivi karibuni kwenye huu mjadala. Na napenda niseme uliyoyasema ni mambo ambayo wataka mabadiliko walitakiwa wayashikie bango mwanzoni kabisa. Ila uchaguzi unapokuja unakuja na yake mapya kabisa.
Wakati wa mchakato wa katiba (ambako baadae ilikuja kuzaliwa UKAWA), kuna watu walitahadharisha kuhusu haki. Kwamba kwa jinsi mchakato unavyoenda tangu mwanzo ilikuwa hakuna nafasi ya haki kupatikana na ilikuwa ni bora kwa wale wadai haki wa ukweli wasiruhusu kuwa distracted na quick gains ya kukimbilia katiba mpya. CCM iliiba wazo la katiba mpya na ikalifanya kuwa ni la kwao na wakalifanya wanavyopenda wao kwa masilahi yao wenyewe. The fact that UKAWA ya leo, ilikubali kushiriki mchakato ule tangu mwanzo wakijua kabisa mapungufu yake na kukosekana kwake kwa misingi ya haki ndio kulikotufikisha hapa leo. Sasa kwa sababu tu walishiriki mwanzo, hakuwafanyi leo hii kukosa haki ya kuukosoa mchakato wa katiba kwa sababu tu na wao walikuwepo. Kama unakubaliana na hili, naomba linganisha na hili la Dr. Slaa kwa jinsi utakavyoona vinaingiliana na muktadha wa Slaa kumkaribisha Lowasa (Japo sio muhimu sana).
Katika hiyo aya ya juu nnachojaribu kukisema ni kuwa, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya kuwa na wazo zuri na kutumia njia SAHIHI kulifikia hilo wazo zuri. Usipotumia njia SAHIHI basi utapoteza gharama zako za mali, wakati na afya yako kwa sababu hutakaa ufike katika wazo zuri ulilokusudia. Mwisho wa siku, ili kufika katika malengo ya lile wazo lako zuri itakubidi ni lazima urudie mchakato mzima wa utekelezaji wako kwa kutumia njia SAHIHI. Mimi ni mfuasi mkubwa wa msemo, "Measure twice and cut once". One should always measure carefully (double check, tripple check) and make the decision to cut only once. Nikileta nadharia hii katika suala zima la madaliko hapa nchi ndio na kutana na mabadiliko yanahubiriwa kwenye uchaguzi huu.
Tatizo kubwa ninaloliona katika madadiliko haya yanayo huburia ni kuwa yako vague. Hayako specific tunabadilisha nini ili kuleta nini. Na hapa sizungumziii utitiriri wa ahadi kama anazotoa Magufuli kwa sababu surprisingly nae anahubiri mabadiliko, na pia sizungumzii kelele za mfumo mfumo bila kusema ni nini huo mfumo na mfumo unaokuja baaada ya huu mfumo mbovu ni upi. Hapa nazungumzia an actual road plan ya kuyafikia hayo madiliko ambayo haiishi tu kwa kusema CCM itoke madarakani. Baada ya hapo, tutajua mbele ya safari. Labda kuna watu kwa uelewa wao (mdogo au mkubwa) wanaweza kuafford kusema "tutajua mbele ya safari" ila mimi siko katika mtazamo huu. Na kinachonifanya niamini hivi ni kuwa, mabadiliko ya kweli hayaangalia leo tu, mabadiliko ya kweli yalenga kuweka msingi leo ili vizazi na vizazi vije kufaidi matunda yatokanayo na mabadiliko hayo.
CDM hapo mwanzo walikuwa na a glimpse ya hayo mabadiliko ninayozungumzia hapa. Nasema glimpse kwa sababu hoja yao kuu ilikuwa imejikita kwenye jambo moja tu, UFISADI. Toa UFISADI, weka serikali ambayo haina watu MAFISADI then huo ndio utakuwa msingi wa Tanzania bora. Sasa anapokuja Lowasa hili suala linabadilika kabisa. Ni kweli hajawahi kuwa convicted, lakini kufumbia macho yote anayokuja nayo ni kuamua tu kuvuka barabara huku umefumba macho. Makala baaada ya makala zimeandikwa juu Lowasa. The fact kuwa hajawahi kuwa convicted ni moja ya sababu kwa nini CCM inatakiwa kuondoka madarakani. Sasa huyu akiwa leo ndio kiongozi wa mabadiliko halafu tukategemea matunda ya mabadiliko yale yale tuliyo yatamani ni kujidanganya wenyewe. Na kinachonifanya niyaangalie zaidi mabadiliko haya ya Lowasa kwa jicho la tatu, ni over expectations kwa kundi la vijana ambao kwa maoni yangu wanafata tu who is the most popular candidate at that time ndio maana tunawaona na boda boda zao ( boda boda ni mfano tu) kwenye kampeni za wagombea wote wote. Tunategemea taifa la aina gani hii expectation isipofikiwa. Niliwahi kuandika humu JF sio kwenye jukwaa hili, "The future of the entire nation, can not be reduced into one big social experiment of seeing if we can get CCM out". Haya ni matusi kwa hili taifa zima. Nimesema hapo juu kuhusu kutumia njia SAHIHI, hii ya LOWASA sidhani kama ni njia SAHIHI. Tukipata matokeo kama tuliyoyapata kwenye mchakato wa katiba, sie tunaojinadi kutaka mabadiliko tusirudi kushangaa na kugeuka kwenye kutoa lawama kama tulivyofanya kwenye mchakato wa katiba.
Wengi tumeshangilia CCM kugawanyika. Je ilimeguka kwa misingi ya tofauti za kiitikadi na maono au kwa misingi ya kutaka ukuu? Tumebaki na CCM yenye mafisidi inayomnadi Magufuli, na CDM inayoongozwa na sura za CCM mafisadi wengine ikimnadi Lowasa. Wote wanatumia mapesa na mapesa wanayoyapata toka kwa matajiri ili wawalinde kwenye uongozi wao, na wanatafuta kura kwa masikini ambao wanawaahidi watawabana matajiri hao hao ili walete mabadiliko! Khaa. Mambo ya ajabu sana.
Mimi naomba unishawishi tu nimchague mgombea unayemtaka kwa sababu zingine na sio unitajie msusururu wa ahadi ambazo husemi utazitekeleza vp au kunipa matumaini ya mabadiliko ambayo najua kabisa yatanirudishe hapa hapa nilipo.
Ukiona unapata hamu ya kuniuliza kwa hiyo kama wote hawafai sasa conclusion ni nini kama baadhi ya watu walivyo muuliza Dr. Slaa kwenye press yake? Kwanza nikwambie rudi kwenye jibu la Dr. Slaa, pili KWANI WANAOGOMBEA URAISI NI WAWILI TU?
Nguruvi3,
..upande wa kwanza: diwani wa ukawa, wabunge wa ukawa, na waziri mkuu na serikali ya ukawa. Raisi Lowassa.
..upande wa pili ni diwani: ccm, wabunge wa ccm, Raisi, waziri mkuu na serikali ya ccm.
..I am just tired na hiki kiburi cha CCM. I cant take it no more. I am going with the first choice hapo juu.
JokaKuu,
Umenifurahisha. Ila kwenye chagua namba moja mbona Lowasa hujamnasibisha na UKAWA. Umemtaja kama mgombea binafsi bana.
Mimi siko kwenye hizo chaguzi zote mbili. Kwa nini sitachajua hilo chaguo la pili, well its CCM halihitaji maelezo zaidi. Kwanini sitachagua hilo chaguo la kwanza kama ulivyoliweka hapo, well, historia ya nchi imenifundisha nisikipe chama kimoja serikali na bunge.
Atakae pata kura yangu ya uraisi, hatapata kura yangu kwenye ubunge. Nakushauri sana ndugu kama kweli unataka serikali ijayo iwe accountable usifanye uamuzi wa kutoa kura zako zote kwenye chama kimoja. Haijalishi nani ataend up madarakani, kwa maslahi ya taifa hili tunahitaji upinzani imara.
Natamani ningekuwa na uwezo kufanya kampeni inayosema "Ewe mtanzania, usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Acha kucheza ngoma ya wanasiasa".
Kumchagua LOWASA na genge lake alafu uite ni mabadiliko kwa hali za wananchi,nikujipumbaza kwa hali ya juu sana
Sitaki kuingia ndani sana kwenye swala la Dr. Slaa kwani ni moja katika watu niliokuwa na imani kubwa nao lakini kwa kitendo chake ameonesha ama hakuwa tayari kwa mabadiliko au alijiaminisha bila yeye mabadiliko hayawezekani. Ninachoomba ni wananchi wapewe haki na wawe huru kumchagua watakaye. Serikali isitoe upendeleo kwa CCM bali itoe fursa sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki..
Dr. Slaa aliharibu toka ile press conference ya Serena, yeye na CCM wanajua hilo.
Wamekaa na kusoma upepo wakaona wazi kuwa kuna sehemu wamekosea kuchanga karata zao.
Ile ya jana Star TV imezidi kumchafulia Dr. Slaa.
Amejikanyaga sana.
Hii kasi ya kujiadhirisha mbele ya kadamnasi inamfuta kabisa kutoka kuwa mtu mahiri na mwenye busara.
Inaelekea baada ya Serena, kafuata interview ya Tido na sasa Star TV kujitetea mno na kuendelea kutoa hoja ambayo ni kutwanga ngumi kwenye maji.
Lakini pia hii ni mbinu ya kuondoa wanahabari kufuatilia kampeni za Ukawa. Propaganda za CCM ni distortation na mis-information.
Dr. Slaa anajitangaza kana kwamba kaonewa haki ya kuwa mgombea wa Chadema/Ukawa (his tone and choice of words says it in plain english despite his continuous refusal kuwa hautaki Uraisi) hivyo anatafuta sympathy ya wananchi ambao wanahamasishwa kuanza maandamano ya kumuaga na yeye eti anaanza kampeni ya kuaga wananchi kutembelea mikoa.
Go figure mtu anayedai kuwa na roho safi kabisa!
..WHAT?!
..R U SERIOUS kuwa Dr ataanza ziara za kuaga mikoani?
..unajua itafika wakati watu wataona mabadiliko hayawezi kuleta na vyama au sanduku la kura.
..kwa kweli ccm wasipokuwa makini tutaishia kuwa kama Libya, Misri, au hata Zaire.
Mkuu wangu nikwambie tu kwamba Mbowe is too smart than all of them japo Zitto alimshtukia toka zamani. Mbowe mshikaji lakini inapofika katika maslahi ya nchi niseme ukweli tu kuwa Mbowe mwenyewe alihujumiwa na ile status Quo maadam ana Ambitions zake anataka kuwa someone powerful. A Legend kabla Mola hajamchukua nje ya fikra za Kichama na hawezi kuachia nafasi zinapotokea ama kuzuiwa.Hii kasi ya kujiadhirisha mbele ya kadamnasi inamfuta kabisa kutoka kuwa mtu mahiri na mwenye busara.
Inaelekea baada ya Serena, kafuata interview ya Tido na sasa Star TV kujitetea mno na kuendelea kutoa hoja ambayo ni kutwanga ngumi kwenye maji.
Lakini pia hii ni mbinu ya kuondoa wanahabari kufuatilia kampeni za Ukawa. Propaganda za CCM ni distortation na mis-information.
Dr. Slaa anajitangaza kana kwamba kaonewa haki ya kuwa mgombea wa Chadema/Ukawa (his tone and choice of words says it in plain english despite his continuous refusal kuwa hautaki Uraisi) hivyo anatafuta sympathy ya wananchi ambao wanahamasishwa kuanza maandamano ya kumuaga na yeye eti anaanza kampeni ya kuaga wananchi kutembelea mikoa.
Go figure mtu anayedai kuwa na roho safi kabisa!
Mkuu RevHii kasi ya kujiadhirisha mbele ya kadamnasi inamfuta kabisa kutoka kuwa mtu mahiri na mwenye busara.
Inaelekea baada ya Serena, kafuata interview ya Tido na sasa Star TV kujitetea mno na kuendelea kutoa hoja ambayo ni kutwanga ngumi kwenye maji.
Lakini pia hii ni mbinu ya kuondoa wanahabari kufuatilia kampeni za Ukawa. Propaganda za CCM ni distortation na mis-information.
Dr. Slaa anajitangaza kana kwamba kaonewa haki ya kuwa mgombea wa Chadema/Ukawa (his tone and choice of words says it in plain english despite his continuous refusal kuwa hautaki Uraisi) hivyo anatafuta sympathy ya wananchi ambao wanahamasishwa kuanza maandamano ya kumuaga na yeye eti anaanza kampeni ya kuaga wananchi kutembelea mikoa.
Go figure mtu anayedai kuwa na roho safi kabisa!
Hili la kuweka mayai yote kapu moja linaweza kutokea.JokaKuu,
Umenifurahisha. Ila kwenye chagua namba moja mbona Lowasa hujamnasibisha na UKAWA. Umemtaja kama mgombea binafsi bana.
Mimi siko kwenye hizo chaguzi zote mbili. Kwa nini sitachajua hilo chaguo la pili, well its CCM halihitaji maelezo zaidi. Kwanini sitachagua hilo chaguo la kwanza kama ulivyoliweka hapo, well, historia ya nchi imenifundisha nisikipe chama kimoja serikali na bunge.
Atakae pata kura yangu ya uraisi, hatapata kura yangu kwenye ubunge. Nakushauri sana ndugu kama kweli unataka serikali ijayo iwe accountable usifanye uamuzi wa kutoa kura zako zote kwenye chama kimoja. Haijalishi nani ataend up madarakani, kwa maslahi ya taifa hili tunahitaji upinzani imara.
Natamani ningekuwa na uwezo kufanya kampeni inayosema "Ewe mtanzania, usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Acha kucheza ngoma ya wanasiasa".
..fortunately Lowassa ameliacha genge lake CCM.
..hata Dr.Slaa amesema wale wabunge 50 na wenyeviti wa mikoa wa chama 20 waliokuwa wahame na Lowassa kwenda chadema, wamebadilisha mawazo na kubakia CCM.
cc Alinda, King Suleiman