Alinda na
King Suleiman
Siasa za nchi zetu bado zina matatizo. Hata hivyo, kuna mambo yanayofanyika katika uchaguzi popote duniani kwa sababu maalum. Kwa wenzetu kuna watu wana strategists ambao
Balantanda, na sisi wengine tumepiga kelele sana.
Kinachotokea kwa CCM ni mambo mawili, kwanza wanaleta distractions za kampeni kwasababu hawana cha kuonyesha miaka 50, na pili hali yao ni ngumu kiasi cha kuwalizumu kutupa karata ya aina yoyote iliyo mbele yao
CCM wanajua hawana cha kuonyesha, na ilani zao hazina jipya, ni photocopy
Kwa upande wa wapinzani, wanakosa watu wa mikakati na hilo ni tatizo.
Kama mlitusoma hapo nyuma, tumeelezea kwa kirefu sana kuhusu maafa ya Jwangwani.
Tunawaeleza wapinzani kuwa tatizo si kilichotokea bali watu waliossababisha maafa yale.
Ndio maana tukahoji kama wapo na wanaendelea na kazi basi maafa mengine tarajiwa yapo njiani
Kwa wapinzani, walitakiwa kuwa na strategist watakaowalazimisha CCM kurudi katika hoja
Kwa mfano, suala la umeme. CCM wanasema bei ni kubwa kwasababu ya Richmond.
Well wangeulizwa wanasemaje kuhusu Escrow ya jana? Nani ameshatakiwa? Nani analipa gharama za pesa za viroba?
Pili, wakisema fulani ni fisadi ni rahisi kuwauliza nani alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Usalama?
Ilikuwaje waliweza kuishi na fisadi huyo hadi juzi?
Wlichukua hatua gani na kama hawakuchukua ni kwanini?
Hiyo ni mifano michache sana. Kazi ya wagombea si kujibu tuhuma rahisi kama hizo.
Hizo ni distractions ambazo zinaajibiwa na 'attacking dog(s)'
Sasa ukiangalia timu ya UKAWA, hakuna mkakati kama huo. Kumtanguliza Sumaye na Lowassa at the same time ni kuua brand ya upinzani. Wameliona hilo? Jibu ni hapana kwasababu hawana wana mkakati
Mgombea anatakiwa ajikite katika sera, mwisho wa siku wanaotukana hawataukuwa na hoja, watarudi kwenye mada na ndipo pa kuwashika.
Mungu aliwapa neema upinzani kutokana na maneno ya Mkapa 'wapumbavu na Malofa' utaona wananchi wanaichukulia kauli hiyo kwa hisia na hasira kubwa sana.
Wapinzani wanachotakiwa ni kuiongelea kauli hiyo kama sehemu ya hisia na kuwaleta karibu wananchi.
Kisha sera zinamwagwa wananchi wakiwa tayari na wazo la upumbavu na ulofa waliorushiwa
Kinyume chake tumesikia Babu Seya na UMASHO.
Nani anawashauri hawao viongozi asiyeweza hata kuona mambo rahisi kama haya?
Hayo yanawezekana kama kuna mipango ya namna ya kuongea, nini cha kuongea , nani aongee na kwa muda gani
Yanapotokea kama yale ya Jwangwani kupandisha watu, vurugu tupu ile dhana nzima ya kushambulia inaondoka inabaki kujilinda. Hapo kuna tatizo
Tusemezane