Nitakusahihisha jambo moja na ambalo labda halikueleweka. Katika andiko langu lile nilieleza jinsi gani ilivyo ngumu kuchakachua kura za Ubunge. Nilieleza na sheria haijabadilika kuwa kura za Ubunge zinahesabiwa na kutangazwa kituoni; hata kura za Urais ni hivyo hivyo na ndivyo ilivyotokea mwaka 2010. Kitu ambacho kilitokea ni kuwa agizo/amri haikutolewa kuzuia kutangazwa matokeo ya kura za Urais hadi yapelekwe NEC. Amri iliyotolewa ni kwa vyombo vya habari kutokutangaza matokeo ya Urais hadi yatakapotangazwa "rasmi" na NEC. Kwa maneno mengine, matokeo ya Urais yalitangazwa majimboni kama sheria inavyotaka - wasingeweza kutuma bila kuyatangaza ila vyombo vya habari havikuweza kutangaza hadharani kabla ya NEC. Hivyo, maripota wa TV au radio kina Ufoo Saro, George Marato na wenzao walipopewa nafasi ya kutangaza matokeo walikuwa na matokeo ya Urais mkononi lakini mabosi wao wa ITV waliwaambia wasiwaambie yale ya Urais bali yale ya Ubunge kwanza..
Kwanini? kwa sababu matokeo ya awali ya Urais yaliyokuja kutoka sehemu ambayo tayari yalikuwa yametangazwa na yale ya Ubunge yalionesha Dr. Slaa alikuwa anaongoza. Ilibidi wazuie hadi mikoa ya Lindi, Mtwara, Tabora na Tanga ilipoanza kuleta kura zake ndiyo Tume ilipokuwa inatangaza kura za Urais ikaanza na mikoa ile ya ngome ya CCM. Hawakuanza na kura ambazo tayari wengine walikuwa nazo za mikoa ambayo wapinzani (CDM) walikuwa tayari wamepata kama Arusha, Musoma Mjini, Mbeya mjini n.k.
Ukilielewa hili utaelewa kwanini walijitahidi sana kupitisha sheria ya Cybercrime na kudhibiti takwimu. Kama siyo rasmi siyo sahihi hata kama ni sahihi.
Kwahiyo mpaka hapo unaona pamoja na kuwepo sheria ya kutangaza matokeo vituoni, bado serikali hakuruhusu matoke hayo yatangaze na vyombo vya habari maana walijua kuwa kama vyombo vya habari vingetangaza basi wasingeweza kuchakachua.
Na kilichofanyika Tume ya uchaguzi walitangaza matokeo ambayo ni ya uongo kwani kulikuwa hakuna tena kitu cha kuwafanya wasifanye hivyo. Na ninakumbuka mgombea wa urais kupitia Chadema yaani Dr. Slaa alilalamikia tume kutangaza matokeo ambayo hayakuwa ya kweli. Hivyo basi kusema kuwa CCM hawawezi kuchakachua kwa vile matokeo yanatangwa vituoni hali vyombo vya habari hawaruhusiwi kuyatangaza ni kujidangaya maana watakachuchua maeneo ambayo ni ya vijijini, wananchi hawana umeme, Tv za kuweza kuona kama klichotangazwa katika vituo vyao vya kupigia kura ndicho kinachotangazwa na tume!
Kwenye Ubunge nako ni vile vile pamoja na kutangaza matokeo vituoni bado kulikuwa na udangayifu mkubwa na uvunjwaji wa sheria rejea mbunge aliyekimbia na masanduku ya kura na tume limtangaza kuwa ni mshindi.au ucheleweshaji wa matokeo kwa maeneo yalioshinda wapinzani mf.Mwanza, Arusha na maeneo mengine, umwagikaji wa damu sehemu ambazo wapinzani walifanya vizuri na nk. Hivyo basi hatuwezi kuja hapa kujipa matumini kuwa tume itafanya tofauti na miaka ya nyuma.
Kikubwa wananchi wahimizwe baada ya kupiga kura basi walinde kura zao maana naona njia hii inasaidia kwa kiasi fulani.
Hiki si kweli kama ingekuwa ni kweli, na kama wangekuwa wanajiamini kuwa mikoa hiyo kuna kura nyingi za CCM basi wangeacha TV/redio sikakusanya matokeo na kuyaleta kama yalivyo na kwa jinsi hiyo watu wangeona wenyewe jinsi kura za CCM zinavyoongezeka kutoka katika mikoa hiyo. Walichofanya baada ya kuona Dr. Slaa anaongoza, na kupata matokeo ya hiyo mikoa kulikuwa hakuna jinsi zaidi ya kuchakachua tu..
Leo hii nikikuuliza Mkoa wa Mbeya vijijini CCM walipata kura ngapi za urais si dhani kama kunajibu la ukweli kilichopo (kama kipo) ni namba za kubumba.
Alinda
Hapa kuna hoja moja. CCM wakinuia kuchakachua hawawezi kualumiwa kwasababu ndiyo nia na dhamira yao
Utamlaumu vipi mwzi kwa kuiba ikiwa wizi ndio dhamira na nia yake?
Tume ya uchaguzi inapotumia mwanya ulioachwa wazi na wapinzani, nayo hailaumiwi kwasababu tunajua ni 'dugu moja'
Wapinzani wanaposhindwa kusimama kutetea kura zao, hapo kuna kosa.
Ina maana wameshindwa na kutoa loop hole ya kutendewa ubaya.
Kwa mfano, Filikunjombe katangazwa kupita bila kupingwa
Kuna hoja hapa
1. Ilitokeaje ikiwa UKAWA walitumia miezi na miezi kufanya vetting ya wagombea na tukasikia wamegawana
2. Ni nani amekwenda kuthibitisha kuwa lipo tatizo na kwanini limetokea
3, Ni nani atahakiki matokeo, ataongoza usimamizi ikiwa wote wamekwenda majimboni
4. Ni nani kati ya Watanzania atakayekwenda jimbo hilo la Filikunjombe kuhakiki kura za Urais
In fact Mzee Mwanakijiji huenda akawa ndio amewafungua macho kuwa jimbo hilo bado lina maana kwao
Sasa inapotokea mambo ya namna hii, ni lazima kuwaambia ukweli kuwa hawajajipanga.
Na huo ni ukweli wanaotakiwa waishi nao ili siku za mbeleni waubaini kama hawataki kuuzuia
Nikufikiria kwa mara nyingine "Fursa" ya ujio wa Lowassa ilivyochezewa kama shilini cho cha shimo, nashindwa kuelewa munkari uliotokea Ukawa mpaka wakapoteza mwelekeo.
Nafikiri kukosekana kwa kuwa na timu maalum zenye kufanya ground work (kutokuaminiana) na walio wenyeviti kung'ang'ania na kutaka kushikilia kila kitu kwa sababu wanazozijua ndiko kutakako waangusha Ukawa.
HIvi Lowassa si tunajua alikuwa na timu iliyojisuka vizuri kabisa ndani na nje ya CCM na walijiandaa vizuri kabisa? je hao wadhamini laki nane si walipatikana kutokana na yeye kujijenga na kuielewa vita na kuuelewa ugumu wa kazi yake ndani ya CCM?
Je Ukawa kabla ya "Rizki" Lowassa kuwaangukia, walikuwa wamejipanga vipi ki-oganaizesheni kuingia uchaguzi huu? je walitarajia suala la hoja tuu kutokana na atakayeteuliwa kuwa mgombea wa CCM?
Walipoanza Tongozana viongozi, wale watendaji (technocrats, organizers, lawyers, finance managers, Campaign strategist) kwa nini nao hawakuanza kwa kasi kuunganisha nguvu kama walikuwa wameshasomana tangu awali kama maadui?
i am totally lost in the amount of disorganization ya kuingia uchaguzi mkuu na tunajiandaa kisaikolojia kuwa goli la mkono ndio litawapa CCM ushindi huku tunaona wazi kuna madhaifu ya wazi!
May be I am too naive or have too much expectations after all these years of bashing and demanding strategic planning kwa Ukawa (Wapinzani), hoping watakuwa wasikivu na waelewa.
Naweza kusema mipango yao ilikuwa mizuri tu.Nikufikiria kwa mara nyingine "Fursa" ya ujio wa Lowassa ilivyochezewa kama shilini cho cha shimo, nashindwa kuelewa munkari uliotokea Ukawa mpaka wakapoteza mwelekeo.
Nafikiri kukosekana kwa kuwa na timu maalum zenye kufanya ground work (kutokuaminiana) na walio wenyeviti kung'ang'ania na kutaka kushikilia kila kitu kwa sababu wanazozijua ndiko kutakako waangusha Ukawa.
HIvi Lowassa si tunajua alikuwa na timu iliyojisuka vizuri kabisa ndani na nje ya CCM na walijiandaa vizuri kabisa? je hao wadhamini laki nane si walipatikana kutokana na yeye kujijenga na kuielewa vita na kuuelewa ugumu wa kazi yake ndani ya CCM?
Je Ukawa kabla ya "Rizki" Lowassa kuwaangukia, walikuwa wamejipanga vipi ki-oganaizesheni kuingia uchaguzi huu? je walitarajia suala la hoja tuu kutokana na atakayeteuliwa kuwa mgombea wa CCM?
Walipoanza Tongozana viongozi, wale watendaji (technocrats, organizers, lawyers, finance managers, Campaign strategist) kwa nini nao hawakuanza kwa kasi kuunganisha nguvu kama walikuwa wameshasomana tangu awali kama maadui?
i am totally lost in the amount of disorganization ya kuingia uchaguzi mkuu na tunajiandaa kisaikolojia kuwa goli la mkono ndio litawapa CCM ushindi huku tunaona wazi kuna madhaifu ya wazi!
May be I am too naive or have too much expectations after all these years of bashing and demanding strategic planning kwa Ukawa (Wapinzani), hoping watakuwa wasikivu na waelewa.
Hapa sidhani kama umeelewa. Tume haitangazi matokeo ya Ubunge yanatangazwa majimboni. Sasa kama jimboni hamkujipanga ndo itakula kwenu! Mgombea mwingine akikimbia na sanduku la kura tatizo siyo tume; wakichelewa kutangaza matokeo wakati tayari yameshakamilika huilii tume. Nitakumbusha kitu kimoja kama umesahau; wakati Nassari anagombea Arumeru Mashariki zilifanyika jitihada kubwa kuvuruga matokeo; nilitumia vyanzo vyangu kutangaza ushindi wa Nassari hapa JF, hakukuwa na jinsi isipokuwa kumtangaza Nassari ushindi. Sasa, kama huna wawakilishi wa kuaminika kura zako zinaweza kuchezewa; huwezi kutegemea huruma ya CCM kushinda. CDM wanataka kushinda "by any means necessary"? CCM wanataka kubakia madarakani "by all means necessary".
Hakuna kulinda kura per se bali kuhakikisha matokeo yanatangazwa. Kura huwezi kuzilinda zaidi ya zilivyo kwenye maboksi; la maana ni kuhhakikisha kura zote halali zimehasabiwa na kuandikwa zilivyo na kutangazwa mbele ya wajumbe na kubandikwa nje. Hiki ndicho watu wanatakia kugombania.
Ni kujidanganya sana kudhania kuwa hakuna watu wanaipenda kweli CCM na wako tayari kuona inatawala tena. Kufikiria kuwa ushindi wa upinzani unaporwa tu na kuwa hawashindwi kweli nalo siyo sahihi. Tanzania ina watu wenye kuipenda CCM kweli na wapinzani hawajaweza kuwashawishi wote. Na yapo maeneo ambayo ni ngome ya CCM, kama vile yapo maeneo ambayo ni ngome ya upinzani. Kudhania vinginevyo ni kutokuwapa credit Watanzania. Wapo watu wanaamini kabisa kuwa CCM haipendwi ila inashinda kwa hila tu. Hili si kweli. Siyo Watanzania wote wanaipenda CHADEMA.
Alinda
Hapa kuna hoja moja. CCM wakinuia kuchakachua hawawezi kualumiwa kwasababu ndiyo nia na dhamira yao
Utamlaumu vipi mwzi kwa kuiba ikiwa wizi ndio dhamira na nia yake?
Tume ya uchaguzi inapotumia mwanya ulioachwa wazi na wapinzani, nayo hailaumiwi kwasababu tunajua ni 'dugu moja'
Wapinzani wanaposhindwa kusimama kutetea kura zao, hapo kuna kosa.
Ina maana wameshindwa na kutoa loop hole ya kutendewa ubaya.
Kwa mfano, Filikunjombe katangazwa kupita bila kupingwa
Kuna hoja hapa
1. Ilitokeaje ikiwa UKAWA walitumia miezi na miezi kufanya vetting ya wagombea na tukasikia wamegawana
2. Ni nani amekwenda kuthibitisha kuwa lipo tatizo na kwanini limetokea
3, Ni nani atahakiki matokeo, ataongoza usimamizi ikiwa wote wamekwenda majimboni
4. Ni nani kati ya Watanzania atakayekwenda jimbo hilo la Filikunjombe kuhakiki kura za Urais
In fact Mzee Mwanakijiji huenda akawa ndio amewafungua macho kuwa jimbo hilo bado lina maana kwao
Sasa inapotokea mambo ya namna hii, ni lazima kuwaambia ukweli kuwa hawajajipanga.
Na huo ni ukweli wanaotakiwa waishi nao ili siku za mbeleni waubaini kama hawataki kuuzuia
Katika mazingira yaliyopo ya bunge kutawaliwa na CCM na kuendeshwa kibabe na Spika kupitisha hoja zao hata kama zina maslahi huku zile za upinzani zikipigwa chini, nini Upinzani walipaswa kufanya kushinikiza Serikali ikubali tume huru ya uchaguzi? Kufanya mikutano na maandamano pekee? Nini cha ziada walipaswa kufanya? Tumeshuhudia kilichotokea kwenye bunge la katiba walivyotumia wingi wao kupitisha mambo kibabe...
Ni kitu gani haswa wapinzani wangeweza kufanya kuishinikiza serikali isalimu amri kwenye jambo hili ambalo kwa vyovyote hawako tayari kulibadili sababu lina maslahi kwao? Rais ndie mwenyekiti wa chama tawala mwenye nguvu juu ya mihimili yote ya dola wanapledge loyalty kwake!
Nakubaliana na Nyani Ngabu kwamba wakati mwingine tunawatwisha mzigo mzito kuliko uwezo wao wapinzani kwenye hili. Shinikizo la kweli litakaloifanya serikali kuzibua masikio litatoka kwetu wananchi na sio vyama vya upinzani peke yao.
Na kwa bahati mbaya sana vyama vya upinzani ambao ni waanga wakubwa wa hii tume hawakufanya chochote cha kuibana serikali ii itekeleze takwa lao.
Uko sahihi lakini swali ninalojiuliza bado ni kwamba wapinzani walipaswa waibane serikali kivipi? Kwa njia zipi? Kupitia Bungeni? Kupitia maandamano na migomo nchi nzima?
Ni njia ipi ambayo ingekuwa effective kuishinikiza serikali hii "SIKIVU" ili iweze kufanya mabadiliko hayo ambayo pengine yangeweza kuwaumiza wao wenyewe?
Mkuu Nguruvi3 na wadau wa great thinkers, ombi maalaumu, tuchepuke kdg. Naomba mada mbili zinanisumbua sana moyo wangu
Naomba uje na mjadala kuhusu zuio la polisi kutembea kwenye daladala nakutembelea maeneo ya kijamii kama sokoni au mahospitali, maana kwa mtazamo wangu naona kama hakuna uvunjifu wowote wa kisheria na pia kila mgombea anayo haki ya kikatiba ya kuwa popote, naona itaibua sintofaham kubwa sana kwamba polisi kama wanaegemea upande fulani.
Pili, ni kuhusu haya mapingamizi ya NEC na wagombea kupita bila kupingwa, kuna mapingamizi jamani yanahuzunisha sana, mara muhuri mara sijui jina au sahihi mtu anaondolewa kugombea, is ths a democracy we need?? Mm nadhani ifike mahali NEC baadhi ya vitu wich can be amended wasiwe wanawadisqualfy wagombea, ninahuzuni sana.
Kweli tunawalaumu wapinzani kwa uzembe, bt mara nyingine human error can prevail na sio sahihi kudisqualfy kwa makosa kama hayo.
Kwakweli Tume huru ya uchaguzi need reform kwa hili
Pole kwa kuwahamisha, nakuomba uje na bandiko tulijadili kama haitakwaza