Chadema uchaguzi wowote fanyeni hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema uchaguzi wowote fanyeni hivi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jun 19, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wengi wetu tuta kubaliana kwamba Chadema wamejitahidi mno kama Chama kuonyesha nini Mtanania anahitaji . Pia Chadema wamekuwa wabunifu muda wote na CCM wanafuata . Zaidi ya yote Chadema wana hubiri Tanzania kwanza , mtanzania awe na maisha yenye unafuu na posho baadaye . Kwa kuwa sasa wanalia na Utanzania maisha ya Watanzania nina washauri wazidi kuwaumiza CCM kwa hili . Ondoeni bendera zenu kwenye kampeni zozote .Ok zaweza kuwepo lakini mna alama mbili sasa . Mna Kombati na bendera . Lakini pia kuna ambao si wana Chadema kwa uanachama lakini waliwapigia kura hawa ni watanzania wapeni nao nafasi .

  Nashauri kama ilivyo kuwa uchaguzi uliopita , nilitembea sana Dar, Arusha na maeneo mengine kwa kweli sikuona posters za Chadema kwa uwingi kama za CCM lakini pamoja hilo kuonekana hata EU na wapenda haki wengine wali hoji ,ila wapiga kura watanzania na wana Chadema wameonyesha kwamba wao hawangalii posters ila message na mtu mwenye nia safi.Kwa mfano Dar Kawe na Ubungo watu wakaamua .

  Now badala ya kuhangaika na bendera za Chama kwenye chaguzi zijazo hakikisheni mnatumia bendera za Taifa letu .Ndilo tunalo pigania na si maslahi ya Chama . Wapeni watanzania nafasi ya kuiona na hata kuishika bendera ya Taifa lao maana najua wao wengi mno wanaiona kwambali na wengi hata kuishika na baadhi hata kuiona bado .Tanzania kwanza Chadema onyesheni mfano .Tuwaache wagombea wavae uniform za Chama na kama kuna mwingine atapenda sawa lakini onyesheni Utaifa kwa kusambaza bendera za Taifa kila kona .

  Naomba kusikia wewe unasemaje .
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!no comment!!
   
 3. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  pumba! waonyeshe uzalendo kwa kutekeleza waliyoyaahidi si kugawa bendera.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwani hadi sasa walicho kiahidi hujaona kwamba wanatekeleza na wana endelea kutekeleza ? Au wewe unadhani wanalala na kuchangia kwa kupinga then wanasema wanaunga hoja 100 kwa 100 ? Uko Dunia gani ?
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni wazo zuri. Naunga mkono hoja.
   
 6. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wazo zuri sn..pia vyombo vya habari itv,ch10, startv pamoja na redio zao..viache tofati zao viweke utaifa wao mbele tuikomboe nchi.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Watu wanaweza kusahau siku ya kupiga kura
   
 8. oba

  oba JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hiyo
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Watu hawawezi kukusahau siku ya kupiga kura . Rudia tena soma nilicho andika utaona nina maanisha nini . Maana mwisho wa siku watu watachagua Chama ambacho ni Chadema kwenye karatasi za kura hakuna uniform wala kofia za Chama .Sasa nifafanulie una maanisha nini hapa .
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Usije kushangaa "Serikali" ikapiga marufuku matumizi ya Bendera ya Taifa kwenye "shughuli za chama"
   
 11. C

  Chal Senior Member

  #11
  Jun 19, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  watekeleze kwani wao wana dola?wangepewa dola waunde serikali ndiyo ungewadai kutekeleza ahadi.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Yes you might right maana watajidai ni nyara za Taifa sijui Watanzania si wenye Taifa ,but again Chadema lione hili jitofautisheni na hao wagawa fulana nyie simamieni Taifa letu.Kila mmoja ba bebdera ya Taifa mkononi Utaifa utakuwa umeiva ile mbaya na kura zitapigwa .
   
 13. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Pendekezo lako ni zuri na kwa maoni yangu tungelipeleka mbali zaidi ya hapa: kwamba katika mchakato wa kuandika katiba mpya tufute kabisa huu utamaduni wa bendera na sare za vyama. Tuhimize wagombea na washabiki wao kutumia bendera ya taifa. Hili litasaidia wananchi wengi wanachama wa vyama mbali mbali na wasio wanachama kushiriki kikamilifu katika mikutano ya kampeni kwa kusikiliza hoja za wagombea badala ya mbwembwe za bendera na sare na hatimaye kufanya maamuzi kwa kuzingatia hoja!! Kwa utaratibu wa sasa hivi, kama sio mwanachama wa CCM kwa mfano unajisikia vibaya kuhudhuria mkutano wa kampeni huku ukiwa umezungukwa na kijani kila kona. Mara nyingi unakuta wananchi wasio wanachama wakiwa pembeni mbali na sehemu ya mkutano. Pili itaimarisha usalama wakati wa kampeni - hakuna mtu anayejitambulisha kwa alama za chama.
   
 14. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,974
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Basi wagawe bendera ya Taifa na ya CDM!
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mkuu nina mashaka na huu ushauri wako!
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ni wazo murua.Kwa tunaong'amua mambo, tulishajua mapema kuwa cdm imejikita kwenye anga za utaifa zaidi kuliko maslahi ya chama, na shuhuda za kuthibitisha hili ni nyingi. ILA kuna mahali vijijini niliwahi kupita, nikagundua kuwa watu hawatofautishi kati ya bendera ya taifa na ya ccm, au to be precise, hawatofautishi chama na serikali! kwao ulizungumzia serikali na taifa unamaanisha ccm...sasa hii ni changamoto in case zoezi hili liki'take-off.
   
 17. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni bora uelewe kwamba pesa wanaotumia CDM kwenye uchaguzi haifiki hata 5% ya pesa wanaotumia CCM! Vilevile zingatia kwamba kutengeneza bendera moja si chini ya shilingi elfu mbili. Sasa kusambaza bendera kila kona kwenye nchi yenye vijiji zaidi ya laki nne angalau kila kijiji kipate kabendera kamoja ni mabilioni ya pesa. Kama wapiga kura wanachagua kwa kuangalia message na sio paraphernalia ingekuwa bora hiyo hela waka invest kwenye message.
   
 18. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,186
  Likes Received: 1,187
  Trophy Points: 280
  waliwahi kumuwekea pingamizi mbowe 2005. Kwa jambo ilo, mahakama ikalitolea maelezo kuwa c kosa.
   
 19. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Umekuwa na mashaka mkuu ni sawa lakini una la kunisaidia kuelewa tofauti na wazo hili ? Usiniache tu nina hang no sema nijifunze
   
 20. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kusema na kutekeleza ni vitu viwili tofauti kabisaa. kwa hiyo hata kama wangepewa dola hungeweza kuwagarantee kwa hilo. hata ccm wanasema sana tu. na sera zao ni nzuri tu lakini utekelezaji ndo kimbembe. Pole.
   
Loading...