CHADEMA: Tundu Lissu kurejea nchini na atafanya mikutano nchi nzima, wanachama waombwa kuchangia chama!

kama serikali yenye bahari,maziwa,misitu,madini,gesi, maeneo ya utalii na ardhi yenye rutuba inayostawisha kila mmea na watu inao nabado inaombaomba ni miaka zaidi ya60 ccm ikipewa ridhaa yakuiongoza nchi watu wake bado nimasikini wakutupwa kuna ubaya gani chadema ikitumia rasilimali watu na ndio kitu pekee walichonacho?
 
Mjumbe wa kamati kuu na Katibu wa BAWACHA mkoani Mwanza amesema wanamtarajia Tundu Lissu kurejea nchini hivi karibuni na kwamba pamoja na kuendesha kikao cha Baraza kuu pia atafanya mikutano nchi nzima.

Katibu huyo amewaomba wanachama wa CHADEMA kuchangia chama ili kukiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha.

Amezungumza hayo katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa mubashara na Star tv kikiongozwa na mtangazaji nguli Mansour.

Maendeleo hayana vyama!
Zege halilali
 
Si wanachama tu, CDM imewaomba watanzania wote wanaotaka HAKI, UHURU na USAWA basi wajitokeze kuunganisha mnyonyoro ..kuelekea kwenye Tanzania wanayoihitaji.

Mwitikio si wa kawaida by the way, naona mtaa wa saba hawana furaha kabisa kwenye hili.
Wapenda amani uhuru na maendeleo wooote wanakaribishwa
 
Back
Top Bottom