Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
CHADEMA tumekuwa kama wajenzi wa Mnara wa Babeli. Tunakuja na mikakati mizuri ila linapokuja suala la utekelezaji lazima tulikoroge. Sijajua tatizo kubwa ni viongozi wetu ambao hata elimu ya msingi hawana ama hulka ya wabunge tulionao.
Siamini kama kuna hoja tutaiasisi Bungeni itaungwa mkono na CCM. Tunaendekeza siasa za utengano badala ya kuungana. Ni sisi ndio tulioanzisha wabunge kutosalimiana na kutopeana haki za falagha kwa wale wenye mahusiano ya jinsia mbili. Juzi tumemsifu Ndugai na leo tunamtukana na kumsakama. Dr Tulia kapumzika sasa na sasa tumeanza kumkoroga Ndugai. Wapi tutapenya?
Tulifikia kwenye stage nzuri ya kutumia fursa ya jinsi Rais Magufuli alivyohandle suala la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutekeleza ule mpango wetu wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye. Tumefeli na hatutakuja kufanikiwa. Kuna wakati tulifanikiwa kuwashawishi wabunge wa CCM na walikuwa upande wetu. Sote tulimshambulia Makonda na tulimsifia Spika Ndugai kwa kuonesha msimamo.
Sasa Halima Mdee na Freeman Mbowe wamelikoroga. Mahaba yao kwa Wenje na Masha yamesababisha kuwatoka maneno yanahosababisha CCM wote sasa kuungana dhidi yetu. CCM wakiungana ni hatari kubwa sana kwetu. Wametuzidi Bungeni, wametuzidi mtaani na wametuzidi Mahakamani. Maneno ya Halima Mdee ndiyo yaliyowakosesha ushindi akina Masha.
Niwapmbe sana Makamanda. Tunajiharibia wenyewe. Tusimlaumu mtu mwingine. Tunawakatisha tamaa hata wale wanaotusaidia kupitia mitandao ya kijamii kama Mange Kimambi. Tunawakatisha tamaa pia wasanii wanaotusaidia kama Nay wa Mitego. Tunamkatisha tamaa kila mtanzania anayetuunga mkono. Tusishqngae 2020 tukapata wabunge wasiozidi 10. Tusishangae pia ikiwa Mgombea Urais wetu akapata kura chini ya asilimia 5. Adui wetu ni sisi wenyewe