CHADEMA tumetegua bomu letu,CCM msije kuthubutu

RUTO

Senior Member
Dec 19, 2013
147
29
Kati ya vitu vilivyokuwa vikiiumiza kichwa "think tank" ya CHADEMA ni huyu bwana mdogo Zitto. Mikakati yake miovu ya kuidhoofisha CHADEMA tuliijua siku nyingi tukambana kuaccess zile sehemu nyeti za chama. Lilipokuja kusanuka hili la "mkakati wa mabadiliko 2013" ikabidi tumbane hapo hapo. Na kwa sasa ndo tunamalizia stori yake hivyo tutaelekea 2015 tukiwa wepesi na imara dhidi ya CCM.

Sasa tuje kwa washindani wetu wa kisiasa CCM. Umewahi kuwaza timu hizi mbili ndani ya CCM? Timu ya LOWASSA akiwa na wachezaji mahiri kama Zungu,Mahanga, Bashe,Sophia Simba, Chenge, J. Makamba na Wenyeviti wa CCM wa mikoa na Wilaya pamoja na makatibu wao?

Vipi kuhusu hii ya SITTA na wachezaji mahiri kama Mwakyembe, Zitto, Kitila, Tibaijuka, Magufuli, Lembeli, Kilango, Filikunjombe, Nape, Kinana, Mukama, Mwandosya, na wengineo?

Silaha ya LOWASA kwa chama na kwa Watanzania ni FEDHA.
Silaha ya SITTA kwa chama na kwa Watanzania ni UTENDAJI ULIOTUKUKA.
Falsafa yao kwa pamoja ni: NISHINDE MIMI AU TUKOSE WOTE.

Timu zote hizi mbili zina maadui wawili wakubwa. Adui wa ndani na nje. Adui wa kwanza kwa kila timu yupo ndani ya chama chao, yaani katika CCM adui wa LOWASSA ni SITTA na wa SITTA ni LOWASSA. Adui wa nje kwa kila kundi ni CHADEMA.

CHADEMA ni ADUI kwa kila timu katika mazingira ya mapambano ya kusaka USHINDI. Lakini CHADEMA ni AHUENI katika kila timu wakati wa KUSHINDWA. Katika mazingira ya mapambano ya kusaka USHINDI kwa kila timu CHADEMA ni adui kwa mantiki kwamba kila timu inahitaji hasimu LOWASSA/SITTA awe dhaifu na hapohapo CHADEMA awe dhaifu ili ajihakikishie USHINDI. Lakini CHADEMA ni AHUENI katika kila timu wakati wa KUSHINDWA kwani mmoja kati ya LOWASSA/SITTA anapotangazwa kuwa AMESHINDWA basi anatamani MSHINDI awe CHADEMA ili falsafa ya NISHINDE MIMI AU TUKOSE WOTE itimie.

Lakini naomba ieleweke kuwa SITTA atakaposhindwa kupenya ndani ya CCM atatoka na ndio maana CCK ambayo ilikuwa CCJ iko STANDBY. Hii ni kwa sababu mpinzani wake yaani LOWASSA tayari amekwisha kushinda ndani ya CCM kutokana na nguvu ya FEDHA iliyomwezesha kuunda mtandao. Hivyo timu ya SITTA inajua haiwezi kupenya kamwe ndani ya CCM.LOWASSA akishindwa kupenya ndani ya CCM jambo ambalo ni nadra kutokea ni kwamba ATAWAVURUGA akina SITTA au timu yoyote itakayokuwa imepenya na kuibeba CHADEMA. Kwa sababu ndio timu ambayo madhara yake ni madogo.

UTABIRI WANGU KATIKA VYAMA KUHUSU WATAKAOSMAMISHWA KOGOMBEA

CCM-EDWARD LOWASSA

CCK-HARRISON MWAKYEMBE

CHADEMA- WILBROAD PETER SLAA

UTABIRI WANGU KUHUSU CHAMA KITAKACHOSHINDA URAISI WA NCHI

CCM-16%

CCK-32%

CHADEMA-52%
 
Umenikumbusha uzi wa Aweda kuhusu proposal aliyopewa mkulu....

Well I know and I know the change is a must...
 
Analysis yako ni nzuri ila ungejaribu kuwaingiza Membe ma Migiro katika hayo makundi au unadhani hawana impact katika ccm ya sasa? naungana na wewe kwamba haya makundi ya CCM yatagawanyika vibaya na kutoa upenyo rahisi kwa chadema.Ushauri kwa chadema: anzeni kupanga safu ya mashambulizi sasa, safishemi chama haraka kwa kuondoa wasaliti akina zito mara moja. msijali kuhusu wafuasi wake watapotea kimyakimya "bwana wao" atakapotimuliwa.
 
Sijaweka NCCR, CUF, TLP, DP, UPDP nA na vingine kwani najua havina madhara labda pale ambapo vitaungana. Membe na Migiro nimewapuuzia hata kama JK anawasapoti kwani hawana sifa za utendaji wala fedha kama Sitta na Lowassa. Sifa zao ambazo Lowassa na Sitta hawana hazina madhara kwa makubwa kwani hata JK haya makundi yanamzidi nguvu, Hamuoni anavyoendeshwa na bunge kama remote kuhusu baraza lake la mawaziri?
 
Haya mkuu.
 
Hii ni sawa Na mwanamke alietoa mimba then ikagoma Kutoka na ikageuka Kua jipu na kumuua yeye mwenyewe!

Ccm walichokosea ni kuwarudisha wale waliokua Wana makundi ndani ya Ccm! Wangewaach na kukomaa wenyewe! Sasa Kwa kuogopa mpasuko Wote wakarudishwa na kupewa Asante ya uwaziri! Sasa Kz kwao 2015 mimba Hiyo Imegoma toka Imegeuka bomu!
 
Sijaweka NCCR, CUF, TLP, DP, UPDP nA na vingine kwani najua havina madhara labda pale ambapo vitaungana. Membe na Migiro nimewapuuzia hata kama JK anawasapoti kwani hawana sifa za utendaji wala fedha kama Sitta na Lowassa. Sifa zao ambazo Lowassa na Sitta hawana hazina madhara kwa makubwa kwani hata JK haya makundi yanamzidi nguvu, Hamuoni anavyoendeshwa na bunge kama remote kuhusu baraza lake la mawaziri?

Kwa Membe hapo pana hoja kwani huyu alipata fedha nyingi sana alipopeleka jeshi Comoro
 
Back
Top Bottom