CHADEMA: Tumeshinda

Jamani hili swala liko bayana, sehemu kubwa ya wapiga kura ni wazee na vijana wachache ambao walijiandikisha. Kumbukeni kwamba asilimia kubwa ya vijana walikuwa hawaoni umuhimu wa kujiandikisha na leo hii ndo wanaona umuhimu. Ndo maana ukiangalia idadi ya waliojiandikisha ni kubwa kuliko wapiga kura halisi maana yake ni kwamba hili daftari linahitaji kuwa updated na CCM wanaliogopa hilo maana hata kule kijijini vijana wengi waliomaliza shule za kata hawaiungi mkono CCM lakini hawaja andikishwa na dio wahudhuriaji wazuri mikutano ya kampeni za Chadema.
Nasema hivyo kwa maana kwamba wengi wetu tumechukua taswira ya wingi wa watu katika mikutano ya Chadema kuliko CCM lakini inapokuja kwenye uhalisia wa kura CCM wanawazidi Chadema.
Ndo maana Nape hakuyaongea anayoyasema kabla kwani alitarajia kupoteza kata nyingi kuliko ilivyotokea kumfanya aamini kuwa wameshinda. Kimsingi huwezi kusema umeshinda wakati umepoteza kile ulichokuwanacho.
Lingine ni kuwa Nape ameathirika kisaikolojia na vuguvuga la mabadiliko inayoendeshwa na Chadema na ndo maana hakuwa anavitaja vyama vingine kitu ambacho nadhani ni hatari zaidi kwa chama tawala kilichokaa madarakani mda mrefu kama CCM.
Hata kwenye kata ambazo upinzani umechukua, utakuta imetumika nguvu ya ziada na hata umwagaji damu ambao umesababishwa na chama tawala kutokukubali kushindwa au uonevu wa vyama vya upinzani hasa pale CCM inapozidiwa kete.....hayo yamejionyesha sana kwenye kampeni.
Nape anapaswa kupambana na umaskini wa watanzania kupitia ilani ya chama chake lakini kama ataendelea kuwaza M4C kama ndo adui namba moja kuna hatari kubwa kwa chama chake.
 
Ndoto za mchana hata mwehu anaota

Chama
Gongo la mboto DSM

Ndoto zetu zinaendelea kutimia. Mlikuwa mna kata 27 mmeambulia 22 - you are stepping down little by little.

Where are the 5?
 
heche mbona unamstua adui, hapa nape alikuwa anafanya kosa ulitakiwa kukaa kimya au kumpongeza, hapa umempa mwanya wa kurudi na kusoma vizuri matokeo anaweza kuona hatari inavyomkaribia kwa karibu na kurekebisha hali ili kukwepa kutekwa na M4C.
 
Ndoto zetu zinaendelea kutimia. Mlikuwa mna kata 27 mmeambulia 22 - you are stepping down little by little.

Where are the 5?

Nilitegemea M4C ingewasaidia kumbe geresha tu !

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kilichosaidia kutoka kata zenu 27, mkaporomoka hadi kata 22 tukiwa tumewapokonya kata zingine ni nini?

Hatukutumia nguvu nyingi kuzipata 22 nyie mmetumia nguvu nyingi sana au umesahau vishindo vya M4C? Kumbe kelele nyingi tu sera hakuna

Chama
Gongo la mboto DSM
 
molemo,ndiyo tumeshinda,lakini ushindi ni mdogo sana kulingana na kasi ya mabadiliko,tatizo liko wapi??

tatizo ndugu yangu wa tz wamerogwa! Yaani vijisenti vya ccm vinawachanganya!!! Wao wakihongwa kidogo tu kwa pesa ya kula lisaa limoja wanasahau shida za miaka mitano!!!

Hatukutumia nguvu nyingi kuzipata 22 nyie mmetumia nguvu nyingi sana au umesahau vishindo vya M4C? Kumbe kelele nyingi tu sera hakuna

Chama
Gongo la mboto DSM

CCM HAIKUTUMIA NGUVU NYINGI KATIKA CHAGUZI HIZI?? Chama speak reality unless otherwise unafanya ushabiki! Ulitaka watumie nguvu gani zaidi.

Yaani pesa zote....nguvu ya dola....n.k, n.k, siyo nguvu nyingi
 
CCM imemwaga sera na watu wanaona matendo

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Subiri, kidogo utakubali tu. Mimi nashangaa sana CDM inamudu vipi kuchuku majimba, na kata za CCM, kipindi hiki wakati wapiga kura ni wale wale. Niliona Igunga jinsi vija walivyolia kwa kutokujiandikisha. Nasubiri hasa 2014-15 nijiridhishe.

Mla mla leo mla kesho kala nini?
 
CCM imemwaga sera na watu wanaona matendo

Chama
Gongo la mboto DSM

Una aibu kusema matendo! Matendo gani wameona? Rushwa katika chaguzi zenu...hadi chooni...Kutumia dola kuwatisha wananchi ili wasiwe huru kufanya uchaguzi? Ufisadi au?

Sema tu KUNA baadhi ya maeneo watu hawajapata elimu ya uraia. Hawajaijua vizuri CCM. Kadiri M4C inavyojipanga tena....ndipo utakuja kujua kwamba watu walikuwa hawajua uchafu wa chama chenu!
 
Mmetumia zaidi ya mil. 300 kwenye M4C sasa ni elimu gani ambayo hamjaitoa? kila kona Tanzania mlikuwapo nitakubaliana na wewe kama ukisemo somo limeshinda waachieni wenyewe CCM

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom