CHADEMA: Tumeshinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Tumeshinda

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Molemo, Oct 30, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  WAKATI Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akitambia ushindi mkubwa walioupata katika kata 22 kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jumapili, CHADEMA wamemtaka aache kuwa kama vuvuzela, wakidai wao ndio washindi.
  Chama hicho kimesema kutokana na idadi kubwa ya kura walizopata katika kata zote hata zile ambazo hawakushinda ni dhahiri kuwa ngome yao inazidi kuimarika maeneo mengi nchini kiasi cha kuweza kuwanyang'anya CCM kata.

  Kauli ya CHADEMA ilitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche, wakati akijibu tambo za Nape na kudai kuwa kada huyo ni sawa na vuvuzela, kwani kama angekuwa anafanya tathmini angeweza kubaini ni kwanini wananchi wanazidi kuikataa CCM.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Mtaa wa Lumumba, Nape alisema kuwa idadi kubwa hiyo ya madiwani waliyopata ni ishara kwamba CCM bado kinakubalika kwa wananchi na kitaendelea kushinda katika chaguzi zijazo.

  Kauli ya Nape inakuja ikiwa ni siku moja tangu kumalizika kwa uchaguzi huo mdogo kwenye kata 29, ambapo CCM iliweza kurejesha kata zake 22 na kupoteza tatu zilizochukuliwa na CHADEMA iliyoshinda kata tano na CUF ikipata kata moja. Nape alisema ushindi huo umetokana na chama hicho kuhubiri amani mara kwa mara katika mikutano yake, tofauti na vyama vingine ambavyo sera zao ni za kumwaga damu, kitendo ambacho wananchi hawakikubali.

  "Ushindi huu unadhihirisha kuwa hata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 chama chetu kitawashinda wapinzani," alijigamba. Nape aliponda opereshini ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayoendeshwa na CHADEMA nchi mzima, akidai inaandamana na vurugu na kwamba haitakisaidia chama hicho. Alisema operesheni hizo zimekuwa zikisababisha vurugu na vifo katika maeneo mbambali kilipopita chama hicho.

  "Juhudi zote walizofanya Katibu Mkuu, Dk. Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, hazikuzaa matunda, hiyo inatokana na siasa chafu za vurugu, hivyo wananchi wameamua kukinyima ushindi," alisema. Nape pia alisema kuwa CCM inalaani vurugu zilizotokea katika baadhi ya maeneo kulikofanyika uchaguzi huo kwamba huo si utamaduni wa Watanzania.

  Alisema kuwa uchaguzi ulifanyika katika kata 29 na kati ya hizo 27 zilikuwa za CCM na mbili za CHADEMA, hivyo wao waliweza kuzirejesha kata zao na kutwaa nyingine tatu. "Nape aache kupiga kelele kama vuvuzela bali wakae chini na kujifanyia tathmini, wajiulize ni kwanini watu wanazidi kuwakataa. Sisi kwanza tumeweka historia tangu mfumo wa vyama vingi uanze kwa kusimamisha wagombea kwenye kata zote, tumeweza kutetea kata zetu mbili na kuchukua za CCM tatu," alisema.

  Katika kujibu hoja hizo, Heche alisema kuwa wanachokifanya CCM sasa ni sawa na kufiwa na watoto halafu ukajipongeza kwa wale waliobaki, huku akibainisha kuwa uchaguzi huo umewawezesha CHADEMA kufika katika vijiji 116 na kusimika matawi. Kuhusu madai ya Nape kwamba Operesheni ya M4C haikufua dafu katika uchaguzi huo kwa vile inachochea vurugu, alisema kuwa taarifa za magazeti mengi ya jana zilieleza bayana kuwa vitendo vya vurugu kwenye uchaguzi vilisababishwa na CCM kwa kuwashambulia wafuasi wa CHADEMA.

  "CCM ni chama cha rushwa na wamechaguana kwa rushwa hata Mwenyekiti wao Jakaya Kikwete amekemea hilo kwenye mikutano ya UVCCM na UWT, sasa kwa mantiki hiyo Nape apime mwenyewe nani kapoteza na kama anafikiri tunafanya mzaha, basi angoje mwaka 2015," alisema.


  Source:Tanzania Daima
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Molemo,ndiyo tumeshinda,lakini ushindi ni mdogo sana kulingana na kasi ya mabadiliko,tatizo liko wapi??
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Molemo,
  Kweli mmeshinda hongereni sana tumeona nguvu ya umma Chadema inakubalika kila sehemu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Subiri, kidogo utakubali tu. Mimi nashangaa sana CDM inamudu vipi kuchuku majimba, na kata za CCM, kipindi hiki wakati wapiga kura ni wale wale. Niliona Igunga jinsi vija walivyolia kwa kutokujiandikisha. Nasubiri hasa 2014-15 nijiridhishe.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Safi heche,kijana huwa hapotezi mda kumwacha adui atambe safi sana,nape mpiga kelel tu kama vuvuzela
   
 6. c

  chama JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Molemo
  Lini tunafanya sherehe za ushindi?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mimi nilishawambia Huyu HECHE ndiye atakayeua hiki chama kwa vile hana sifa za kuwa mwanasiasa. Hivi hapa amesema nini sasa? NAPE kaongelea uchaguzi wa madiwani yeye anaibuka na uchaguzi wa viongozi wa CCM ngazi mbalimbali. Huku si kuishiwa kweli? Hivi hakuna mwana-CDM mwingine anayeweza kukisemea hiki chama?
   
 8. C

  Concrete JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kabla ya kubeza mafanikio ''hafifu'' ya CHADEMA anza kuangalia kwanza mwenendo mzima wa uendeshaji uchaguzi ulikuwaje.
  Kisha tutakupa majibu sahihi hapa hapa
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Bora wewe umesema ukweli. Hivi ni lini ngozi nyeusi itakubali kuwa hapo imeboronga?
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mbaazi ikikosa maua. Haya leta visingizio , mwenendo ulikuwaje? kazi kweli kweli.
   
 11. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nilishasema hili na nalirudia tena;bila kuweka base vijijin cdm tutakesha na hawa magamba, watu wanahitaj mwamko kaskazin tumefanikiwa ila bado kuna maeneo ya nchi bado sana, kuna maeneo mtu unakwenda watu wanakushangaa kama umetoka sayari ya mars, kazi bado sana, kijua ndo hiki tusipouanika sasa tutautwanga mbichi!
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,244
  Trophy Points: 280
  NAPE haoni kwamba CCM is dying slowly
   
 13. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Tatizo Daftari la wapiga kura,

  kabla ya uchaguzi ccm alikuwa akitetea kata 27 Chadema 2, baada ya uchaguzi ccm kata 22 na Chadema kata 5, anagalia na uelewe nani anashuka na nani anapanda ingawa ni kwa mwendo wa taratibu lakini unaweza kuona mwelekeo.

  pia hata kule amabapo ccm ameshinda angalia idadi ya kura wamepishana kwa uwiano upi, trust me mabadiliko yanakuja though ni kwa taratibu kutokana na uelewa finyu wa walio wengi.
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Heche tuambie wapenzi wa CDM , Peza zote zilizotumika kwenye M4C na kwenye kampeni ndo matokeo ambayo tulikuwa tukiyatarajia kweli? au ndo unataka kutufunika tusione kama mnatumia fedha za walipakodi kwa manufaa ya wachache na siyo kwa manufaa ya chama?
   
 15. Anthony Lawrence

  Anthony Lawrence JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,544
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Mabadiliko si lazima yaje kwa ghafla. Wakati mwingine huchukua muda wa kutosha ili kupata mabadiliko ya ukweli na uhakika. Kinachotakiwa ni kusonga mbele na mapambano. kurudi nyuma iwe mwiko. Kukata tamaa awe ni miongoni mwa maadui wakuu wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchii hii. Mungu ibariki Tanzania
   
 16. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  endelea kutuletea habari za kakakuona, hizi huziwezi wewe
   
 17. M

  Molemo JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu
  Everything is undercontrol.Chama kitatoa tathmini rasmi muda mfupi ujao.Utaweza kuona chama kilipata jumla ya kura ngapi katika hizo kata kipindi kilichopita na sasa chama kimepata kura ngapi.Kwa kifupi ni mabadiliko makubwa.Isitoshe tumenyanganya kata 3 za CCM.
   
 18. C

  Concrete JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Jifunze kusoma, kuelewa na kutafakari kwanza kabla ujachangia chochote humu JF.

  Heche anaonyesha ni namna gani CCM ilivyojijengea mifumo ya kutumia rushwa kwenye kila chaguzi zinazofanyika nchini na udhihirisho ni mizizi ya rushwa ilivyo ndani ya CCM nakuonekana dhahiri kwenye chaguzi za ndani na JK kukiri hilo wazi wazi hivi karibuni.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nakushukuru sana kutambua hilo.Kumnyanganya adui kata 3 huku ukiwa umemaintain ulizokuwa nazo si kazi ndogo.Ni heshima kubwa tumepewa na wananchi.Isitoshe maelfu ya vijana kwetu bado hawajaandikishwa kwenye daftari la kura.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,756
  Likes Received: 8,025
  Trophy Points: 280
  Nape ana akili sana
   
Loading...