CHADEMA: Tumepokea taarifa za kujiuzulu mbunge wa Siha kupitia mitandao ya kijamii

N
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) . TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) leo tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.

Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.

Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.
Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya 'hapa kazi tu' na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

CHADEMA tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.

Tutaendelea kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao mwisho wa safari hii.

Imetolewa leo Alhamis 14 Novemba, 2017

JOHN MREMA-Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Ndugu mkurugenzi,nafikiri kams chama mnstakuwa kutafakari kwa kina juu ya haya ya yanayotokea.
Kujibu hoja nzito,kwa sentesi yepesi hayatakisaidia chama.
Mimi nadhani kuna sehemu mambo hayapo sawa.Haiwezekani viongozi wanajiuzulu,halafu majibu mepesi kwamba wamefikia bei.Kuna tatizo,
Kwa mtazamo wangu,nadhani kuwalazimisha viongozi kuponda kila kitu kinachofanywa na serikali,wakati kitu hicho kinashangiliwa na umma wa watanzania ni sababu moja ya msingi.
Pili chadema haina sera,itikadi,filosofia,na mfumo imara wa uongozi.
Mkumbukeni Masha aliwaambia mambo ya
mambo ya msingi sana,mnapaswa kuyazingatia.
Maendeleo,huwa hayajifichi,watu wanayaona,sasa ukiwaaminisha kwamba hayapo,watakushangaa,na mwisho wa siku watakuona wewe kuwa mbsbaishaji na kukukimbia.
 
Back
Top Bottom