CHADEMA: Tumepokea taarifa za kujiuzulu mbunge wa Siha kupitia mitandao ya kijamii

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) . TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) leo tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.

Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.

Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.
Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya 'hapa kazi tu' na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

CHADEMA tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.

Tutaendelea kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao mwisho wa safari hii.

Imetolewa leo Alhamis 14 Novemba, 2017

JOHN MREMA-Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
Ni sawa mmepokea. Haina tatizo. Ni mojawapo ya media of communication
 
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine

kwahiyo huko ccm wamejaa vibuyu wanangoja aje mtu toka cdm kisha akawanie ubunge wao wapo tu.
 
kwahiyo huko ccm wamejaa vibuyu wanangoja aje mtu toka cdm kisha akawanie ubunge wao wapo tu.
haahhhah...sasa kama huyo mbunge wa siha hilo jimbo ni lake atapewa tena agombee kwa tiketi ya CCM kwa sababu anakubalika na wananchi ndio maana akashinda
 
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
Kwel kabsa, hata kama ni mm dalili ya mvua nshaiona
 
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
Sidhani kama sisiemu watawachagua kama wawakilishi wao maana hawakawii kutoka ccm na kuwagharimu. Watakufa kiasiasa ka mende
 
haahhhah...sasa kama huyo mbunge wa siha hilo jimbo ni lake atapewa tena agombee kwa tiketi ya CCM kwa sababu anakubalika na wananchi ndio maana akashinda

Sina uhakika na utaratibu wa ccm kupata mgombea wake, ila nijuavyo kuna ushindani kabla ya kupata mgombea I guess. Hili kosa la kuzawadia nafasi za kugombea naiona cdm na leo ndio inayowagarimu.
 
Mbona chadema walilikimbia bunge la katiba na kuja kudai wakiwa nje!? Wa CCM wanapojiulu ubunge na nyazifa zao zingine kisha kuhamia chadema hao hawaonekani kuwa wasaliti wa wapiga kura wao na waharibifu wa fedha za umma ila huwa ni mashujaa waliojitambua. Kweli Nyani haoni kundule
 
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
sasa unataka kusema huyo jamaa anaweza akapewa dhamana ya kuwania ubunge kupitia CCM kwenye hilo jimbo alafu ashinde -labda ashinde kwa goli la mkono
 
Poleni wana ufipa na pia M/kiti anapaswa kujitathimi kama kweli bado anastahili kuwaongoza. Tafuteni hoja za msingi kulikoni huko chadema huko jikoni kunafukuta.
 
Tunacheza sana na rasilimali za nchi, ni kuwasaliti waliokuamini na kukupa ridhaa yao uwatetee.
Aliyeanza mchezo huo ni Nyarandu na mkashangilia. Mbona sasa mnalalamika wakati score hadi sasa ni ukawa 1 ccm 2 tu. Si mnaweza mkasawazisha au kushinda kabisa kwani muda wa mechi bado sana kwani ni hadi Oct 2020. Why give up so early hadi kuamua kususa kabisa mchezo! Mnawanyima raha watazamaji wa mchezo. Au tuhesabu a technical knock out?
 
Back
Top Bottom