CHADEMA: Tumepokea taarifa za kujiuzulu mbunge wa Siha kupitia mitandao ya kijamii

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) . TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) leo tarehe 14 Disemba,2017 tumepokea taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Mbunge wa Siha Dr.Godwin Mollel amejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM .
Dr.Godwin Mollel ameeleza sababu ya uamuzi wake huo ni kutaka kulinda rasilimali za Taifa.

Sababu hii aliyoitoa ni ya kushangaza kwani Bunge ndicho chombo chenye wajibu wa kusimamia na kulinda rasilimali za Taifa kwa niaba ya wananchi.

Ni jambo la kushangaza kwa kuwa kitendo chake cha kulikimbia Bunge kama chombo cha kusemea na kutetea rasilimali za Taifa na kuja uraiani inatoa taswira gani maana kalikimbia Bunge lenye wajibu huo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi yetu.
Tunawashauri wale wote ambao wanajitoa waeleze sababu halisi na sio kuhadaa umma kwa sababu uchwara kama hizi, maana wapo wanaosema wanaacha kazi kwenda kuunga mkono dhana ya 'hapa kazi tu' na wengine wanasema wanaenda kuunga mkono juhudi za kuboresha maisha kwa kuacha kazi.

CHADEMA tuko imara sana na tutaendelea na ajenda zetu bila kuyumbishwa na wimbi hili la watu wachache ambao wameamua kuwasaliti wapiga kura wao kwa kutoa sababu zisizo za msingi ambazo hazina maslahi kwa Taifa bali kwa maslahi yao binafsi . Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.

Tutaendelea kujenga Taifa letu na Chama chetu bila kujali njaa za baadhi yetu wala maslahi ya watu wachache. Ila kwa hakika ni kuwa wale wenye dhamira thabiti ndio wataweza kufika mwisho wa safari ya kuleta mabadiliko salama. Ni dhahiri wale waliotanguliza ubinafsi hatutaweza kufika nao mwisho wa safari hii.

Imetolewa leo Alhamis 14 Novemba, 2017

JOHN MREMA-Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
Huyu Mbunge ni hovyo kabisa

na MCC ni wafa maji, kununua watu wachache hakuboreshi uchumi

Wananchi wanataaabika na Hali mbaya ya uchumi, vyuma vimekaza

MCC wanajifariji kwa kusema ni wapiga dili wanalalamika, IMF haoooo

Uchumi na ukosefu wa ajira unaumiza watanzania, hao viongozi wachache wanafiki hawatafanya MCc wapate kura

Kama Sizonje anaungwa mkono, weka Tume Huru ya uchaguzi

Kama mnaungwa mkono, kwa nini mawakala wa upinzani wanakamatwa?

Kununua wapinzania ni mbinu za Kishamba
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,792
2,000
Ewe Lissu sema neno moja tu kwa haya yatokeayo na roho yetu ipone.

Maana sasa inakuwa TOO MUCH....

KUNA NINI HUKO NDANI.!?
 
Jaimee

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
2,632
2,000
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
Kuna kaukweli kidogo,but kwa kupitia uchaguzi halisi hawa kamwe hawawezi kuchaguliwa,maana watanzania wa Leo wanauwezo mkubwa wa kutumia logic.Hata hivyo wanaweza kushinda ktk uchaguzi usio na uyakinifu ndani yake.
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
13,563
2,000
Huyu Mbunge ni hovyo kabisa

na MCC ni wafa maji, kununua watu wachache hakuboreshi uchumi

Wananchi wanataaabika na Hali mbaya ya uchumi, vyuma vimekaza

MCC wanajifariji kwa kusema ni wapiga dili wanalalamika, IMF haoooo

Uchumi na ukosefu wa ajira unaumiza watanzania, hao viongozi wachache wanafiki hawatafanya MCc wapate kura

Kama Sizonje anaungwa mkono, weka Tume Huru ya uchaguzi

Kama mnaungwa mkono, kwa nini mawakala wa upinzani wanakamatwa?

Kununua wapinzania ni mbinu za Kishamba
Ni aibu mwanaume kulalamika kununuliwa!

Hivi humo chadema kumbe wote mnanunuliwa hovyo tu kiasi hiki?
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,804
2,000
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
Sasa wabunge Aina hyo si wachumia tumbo tu

Ova
 
Nov 29, 2017
16
45
Tatizo wabunge wa CHADEMA hawaoni future yao uchaguzi ujao 2020,,,,wanajiuzulu na kujiunga na CCM ili wapate nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM...........wakisubiri mpaka uchaguzi mkuu CCM watachagua wagombea wengine
Hivi kujenga nchi yako sharti uwe mbunge ????? Lo wachumia tumbo kumbe hawana aibu mbele za nyuso za wapiga jura !!!!
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,804
2,000
Ni aibu mwanaume kulalamika kununuliwa!

Hivi humo chadema kumbe wote mnanunuliwa hovyo tu kiasi hiki?
Mnaonesha jinsi gani mlivyo....badala ya kutatua matatizo ya wananchi kwa kutumia fedha nyie mnatumia fedha kuwanunua hao makhba

Ova
 
Ntolonyonyo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,190
2,000
Chadema inabidi waitishe mkutano wa dhalura wadiscuss hili suala...hao wabunge wawepo ili watoe kero zao kama kweli zipo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom