Habari wakuu
Kama mnavyojua hoja iliyotupa umaarufu sana sisi CHADEMA ni kupinga ufisadi, na tuliishika kwelikweli mpaka kuandaa list ya aibu ya mafisadi (akiwemo kipenzi chetu lowasa).
Awamu iliyopita CHADEMA haikupenda kabisa kitu kinaitwa
" tume za uchunguzi", tulizipinga waziwazi bungeni kwa hoja kwamba zinalenga kusafisha mafisadi, na zinatumia pesa za umma bure huku report zake zikitupiliwa mbali. Tukafikia kumpa jina la "dhaifu" mh Kikwete kwa kuwa muoga
"KUCHUKUA MAAMUZI" ya kuwatimua mafisadi.
Kwa kweli tulichokipinga ni, moja,
mafisadi kuundiwa tume za uchunguzi, pili,
udhaifu wa rais kutochukua maamuzi kwa haraka dhidi ya mafisadi
CHAKUSHANGAZA SASA
- Leo CHADEMA wanalia bungeni eti watu wanafukuzwa bila uchunguzi, eti rais na watendaji wake wanachukua maamuzi ya haraka sana,
- Leo chadema wanataka eti kufukuzwa kwa mafisadi kufuate mchakato, na tume za uchunguzi
- Leo CHADEMA wanatetea wabadhilifu wanaofukuzwa na serikali eti wanaonewa
Lakini wakati viongozi wa kisiasa wakitetea na kunung'unika kuhusu mafisadi kufukuzwa, watendaji wa chama wanafanya hayohayo. Mfano Meya wa Kinondoni kawatimua wafanyakazi kwa style ile ile
Kwa ufupi, TOKA LOWASSA NA SUMAYE wahamie CHADEMA kilichobaki vilevile ni BENDERA TU, MENGINE YOTE WAMEYABADILISHA, na hakuna wa kuzuia, sera imebadilika, salamu imebadilika (Lowassa mabadiliko), ofisi zimehamishwa kinyemera, hata MSIMAMO WA CHAMA HAUJULIKANI.
Hapa ufipa hatujielewi, KATIBU MKUU mwenyewe kashindwa kuanza kazi ya kuhamasisha sababu hajapewa SERA NA MSIMAMO wa sasa wa chama.
KIFUPI TUMECHANGANYIKIWA!!!!!!!!!