CHADEMA Tumbo Joto Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma, Lowasa aungana na Membe kupinga mabadiliko

Ninachoo kifurahia tu kwasasa kazi zinapigwa, Kuna watu wanashinda huku kutwa wakijaza upepo wa kwenye mitandao. Waambieni waende huko mitaani na vijijini wakaone baadhi ya mambo yalivyo. Hadi kufikia 2020 kunawatu watapata aibu , . Bro Magu anapiga kazi sio mchezo. Taratiibu naona serikali ikirudi mikononi mwa wanchi na maamuzi mengi kwa sasa yanafanywa na wananchi. Miradi yote inasimamiwa na wananchi. Kweli Magu ni mpango wa Mungu.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Jumapili Maci 12, 2017 baada ya kukamilika vikao vya utendaji vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Tunapoelekea kwenye Mkutano huo, zipo dalili kuwa baadhi ya watu hawajafurahia mabadiliko hayo kutokana na sababu binafsi. Maeneo yanayolalamikiwa ni Kuondolewa kwa Hamasa na Chipukizi, Kuondolewa kwa Makatibu Wasaidizi wa Wilaya, Kupungua kwa nafasi za Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

Baadhi ya viongozi wa CCM wanaonekana kujawa na hofu kubwa juu ya hatma yao baada ya mabadiliko hayo kupita. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuboresha mfumo wa chama ili kiwatumikie wananchi zaidi badala kuwatumikia viongozi.

Aiseee kama ndoto vile! Kwa mara ya kwanza Mkutano huu Mkuu umewaweka pamoja mahasimu wa siku nyingi. Edward Lowasa na Benard Membe.Taarifa nilizopata kutoka kwa Jack Gotham, mshenga anayepatanisha Lowasa na Membe zinasema kuwa wawili hao hawafurahii mabadiliko ndani ya CCM. Lowasa anaona kuwa ikiwa mabadiliko hayo yatapita, mfumo wake wa kupata taarifa za siri ndani ya CCM utavurugika. Aidha, Membe kwa upande wake, anaona kuwa mabadiliko hayo yatamzika kisiasa kwani bado anayo ndoto ya kugombea Urais Mwaka 2020.

Hii ni taarifa ya awali na nitaleta detail ikiwa ni pamoja na wale wote wanaoshiriki katika mkakati wa kupinga mabadiliko hayo ya Katiba. Taarifa zao zipo Kiganjani na soon nitakapotua Dodoma, nitatoa orodha ya wanaoshiriki kwenye mkakati huo na jinsi wanavyoshiriki. Bahati nzuri watu wenyewe ni wachache sana tena ni wale wale. Wamekwisha! Wasubiri kuvuliwa nguo ikiwa wataendelea na mkakati huo. Vihela vyenyewe walivyopewa ni kiduchu!

Hii Taarifa kama ingeandikwa na Mr Tupa Tupa ningeamini..... Very soon najua atakuja kutupa mambo ya ukweli yanayojiri
 
Hongera vyama vya upinzani.... CCM wanaandaa vikao/mikutano yao, wala sijasikia maneno maneno, mko sawa, mkoa poa tu, na hakuna fitna za kijinga. Subirini nyie muandae vikao au mikutano yenu, mtawasikia watakavyoanza kulisumbua jeshi letu la polisi.....

Yaani watatomboka balaa
 
..........mchakato na hitimisho la mabadiliko ya Katiba ya CCM na hivyo kupelekea mabadiliko makubwa katika muundo na mfumo wa uongozi na uwakilishi wa chama hicho ni changamoto kwa wanamageuzi na hususan UKAWA. Niwashauri UKAWA warudi kwenye drawing board.
 
Ninachoo kifurahia tu kwasasa kazi zinapigwa, Kuna watu wanashinda huku kutwa wakijaza upepo wa kwenye mitandao. Waambieni waende huko mitaani na vijijini wakaone baadhi ya mambo yalivyo. Hadi kufikia 2020 kunawatu watapata aibu , . Bro Magu anapiga kazi sio mchezo. Taratiibu naona serikali ikirudi mikononi mwa wanchi na maamuzi mengi kwa sasa yanafanywa na wananchi. Miradi yote inasimamiwa na wananchi. Kweli Magu ni mpango wa Mungu.
Likes nyingi sana kwako Mkuu
 
Siku hizi likizo za martenity mnaenda Sauz...tehtehteh....wekeni vyeti bana..acheni utani kabsa.
 
Kwa mara ya mwisho CHADEMA kufanya marekebisho ya katiba ilikuwa mwaka 2004. Hivi mpaka sasa mnaamini kuwa Katiba hiyo ni valid?

Kinachotakiwa sio mabadiliko tu bali mabadiliko yenye tija. Nyie mnafanya mabadiliko ili kukidhi hila zenu badala ya maendeleo ya chama na taifa kwa ujumla.
 
Nipo hapa Dodoma,nawahakikishia mabadiliko makini yaliyoanza tangu mwaka 2012....Lazima chama kiirudishe serikali kwenye mstari.Tutahakikisha yule mkulima,mfugaji,msanii,mwanamichezo,mfanya kazi, mfanyabiashara anamilikI hatima ya Tanzania.CCM ni ya wazslendo wote
haaahahahaha CCM hiihiii nayoijua ama kuna ccm ingine :D:D:D:D. khaaaaa! uve made my day eti CCM ya wazalendo
 
Uzuri wa Ccm kila kitu kinaendeshwa kikatiba
kumpata Kiongozi yeyote
Na inapo fanya mikutano yake hata Kunguni macho ni Dodoma!!
Njoo kwa jirani wazee wa viroba
hahaha
Watu 3wakisha kaa chumbani
waka amua basi full stop.
Mabadiliko Nimuhimu ndani ya Ccm
kwani mbowe alichaguliwa kwenye chumba!!! je ccm ni lini mshawahi kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa demokrasia zaidi huwa mnajifungia chumbani na kuamua mwenyekiti afu kura huwa anapata zote khaaaa :D:D

demokrasia gani mnaongelea eti top 5 ile ya migiro na january hayakutafutwa chumbani??? kweli ukiwa ccm lazma ujitoe ufaham
 
Eti mtu mmoja cheo kimoja.

Kama kweli rais Magufuli anataka wazo lake hilo likubalike, basi aanze yeye kujivua uenyekiti na rais wa Zanzibar ajivue umakamu mwenyekiti Zanzibar. Kama hilo kwao haliwezekani basi hata kwa akina "Pangu pakavu" halitawezekana.

Nitawashangaa kweli CCM kama wataswagwa ili kupitisha mapendekezo hayo ambayo yanawalenga kina fulani.

Kama kweli kuna nia njema basi mapendekezo hayo yang'ate kuanzia juu mpaka chini. Kama cheo kimoja kwa mtu mmoja ikiwezekana basi iwezekane kote na kama itawezekana tu kwa baadhi ya watu basi na isiwezekane kabisa.

Yetu macho kwenye mapendekezo hayo ila ni wakati sasa kwa wana CCM kubadilika na siyo kupelekwa pelekwa tu!

Ni mimi G Sam nikiwa nimejichimbia UDSM kusaka ushahidi wa nyaraka za malipo ya mradi wa hostels za UDSM
 
Back
Top Bottom