Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utafanyika Jumapili Maci 12, 2017 baada ya kukamilika vikao vya utendaji vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Tunapoelekea kwenye Mkutano huo, zipo dalili kuwa baadhi ya watu hawajafurahia mabadiliko hayo kutokana na sababu binafsi. Maeneo yanayolalamikiwa ni Kuondolewa kwa Hamasa na Chipukizi, Kuondolewa kwa Makatibu Wasaidizi wa Wilaya, Kupungua kwa nafasi za Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.
Baadhi ya viongozi wa CCM wanaonekana kujawa na hofu kubwa juu ya hatma yao baada ya mabadiliko hayo kupita. Hata hivyo, ni dhahiri kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuboresha mfumo wa chama ili kiwatumikie wananchi zaidi badala kuwatumikia viongozi.
Aiseee kama ndoto vile! Kwa mara ya kwanza Mkutano huu Mkuu umewaweka pamoja mahasimu wa siku nyingi. Edward Lowasa na Benard Membe. Taarifa nilizopata kutoka kwa mshenga anayepatanisha Lowasa na Membe zinasema kuwa wawili hao hawafurahii mabadiliko ndani ya CCM. Lowasa anaona kuwa ikiwa mabadiliko hayo yatapita, mfumo wake wa kupata taarifa za siri ndani ya CCM utavurugika. Aidha, Membe kwa upande wake, anaona kuwa mabadiliko hayo yatamzika kisiasa kwani bado anayo ndoto ya kugombea Urais Mwaka 2020.
Hii ni taarifa ya awali na nitaleta detail ikiwa ni pamoja na wale wote wanaoshiriki katika mkakati wa kupinga mabadiliko hayo ya Katiba. Taarifa zao zipo Kiganjani na soon nitakapotua Dodoma, nitatoa orodha ya wanaoshiriki kwenye mkakati huo na jinsi wanavyoshiriki. Bahati nzuri watu wenyewe ni wachache sana tena ni wale wale. Wamekwisha! Wasubiri kuvuliwa nguo ikiwa wataendelea na mkakati huo. Vihela vyenyewe walivyopewa ni kiduchu!