Mandla Jr.
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 3,098
- 631
Wana JF, Salaam,
Chadema walizindua mfumo wa wanachama kuchangia chama chao kupitia Mitandao ya simu kama vile M-pesa, tigopesa nk nk. Ni mfumo mzuri na ni vyema kuutumia kama chama.
Lakini pamoja na gharama kubwa za uzinduzi wa huduma hii kukusanya pesa kutoka kwa wananchi wenye mapenzi mema na chadema mpaka leo haifahamiki chama kimekusanya kiasi gani kutoka kwa wavuja jasho wa Tanzania. Na kibaya zaidi kumekuwa na usiri mkubwa juu ya makusanyo ya pesa kupitia njia hii.
Habari ambazo ziko wazi ni kuwa kwasasa ni M/Kiti-Mbowe na Katibu Mkuu- Dr Slaa ndio wanajua ni kiasi gani kimekusanywa kupitia mfumo huu. Hali hii imeleta sintofahamu kubwa ndani ya chadema hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani kuna Wilaya na Mikoa iko hoi kutokana na ukata wa pesa.
Nimalizie kwa kusema "Uungwana ni Vitendo" ni vyema tukawa WASAFI!!!
Mandla
Wa Dodoma.