CHADEMA Tanga wamuunga mkono Slaa

CHADEMA Tanga wamuunga mkono Slaa

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoni Tanga kimesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wanamuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu Dkt Wilbroad Slaa kwa kitendo chake cha kukaa pembeni kutokana na ujio wa Edward Lowassa na kupewa nafasi ya kuwania urais.

Sisi wanachama na viongozi wa chama chetu mkoani Tanga tunaunga mkono kwa dhana kwamba kumsimamisha Lowassa kutaathiri mwenendo wa chama chetu kwa vile ndugu Lowassa haonekani vema na jamii kutokana na matendo yake Katika serikali ya CCM.

Madai kwamba Lowassa amenunua nafasi ya Urais katika chama chetu kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 10 hayajakanushwa popote hivyo na sisi tunaona ni Madai ya kweli.

Chama chetu kwa miaka kadhaa kimekuwa kikijenga kwa jamii kwa kueleza mabaya ya CCM ikiwemo suala la Katibu Mkuu kutamka majina ya watu 12 akiwemo Lowasa Kuwa siyo wasafi ni mafisadi katika list of Shame iweje leo awe mgombea wetu.

Tusitishike na mikutano kujaa watu kwani wapo vijana ambao hawana shughuli za kufanya wanapenda mikusanyiko hivyo tusijifarague kuona tunaweza kushinda na mgombea huyu ambaye kule CCM katika vigezo 13 walivyoweka hakuwa anakidhi vipi sisi tumuone anafaa?

Kwa kuwa michakato imeshafanyika kibabe na shinikizo la fedha sisi tutawapigia kura wagombea wetu wa udiwani na ubunge lakini Rais hatutampa mgombea wetu kwa kuwa hatoshi na hana sifa ya Kuwa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwisho mwenyekiti kama una nia njema na chama kanusha suala la Lowassa kukupa fedha wewe binafsi vinginevyo huko twendako kwenye kampeni hoja hii itatumaliza na jamii iliyokuwa ikituamini kupoteza matumaini ya sisi kuwa Chama Tawala na hili tutawaumiza sana Watanzania ambao wamejenga matumaini kwa muda mrefu na sasa tumeharibu mwelekeo na matumaini yao.

Jonathan Bahweje
Afisa wa Chadema
Kanda ya Kaskazini

Wewe kweli ni Dume la Mende na bila shaka wewe mende.
 
wazee wa ulipo tupo hawataki kusikia maneno mengine zaidi yakuungwa mkono safari ya matumaini..anyway safari njema..namie naunga mkono tamko..
 
Chadema kamwe haiwezi kujibu upuuzi puuzi kama huu, tuna mambo ya msingi ya kufanya kama Chama kwa kipindi hiki...tunawashauri wale wote wenye upuuzi kama huu waendelee kuutoa tu lakini hatutaingia kwenye mkumbo wa kuwajibu maana tutawapa umaarufu wa bure msioustahili...
 
mtoa post umevurugwa, chadema tanga hawawez kutoa tamko dhidi ya chama maisha yote! na bado hao uliwataja hapo hawatambuliki chaema, hao unawatambua ww!
 
nickname
31st March 2011 16:54
#1 JF Senior Expert Member Array


Join Date : 20th December 2009
Location : Dar es Salaam
Posts : 460
Rep Power : 688
Likes Received20
Likes Given13


icon1.png
Mbowe aiuza CHADEMA kwa Lowassa


Kuna mpango wa Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe wa kulipwa mamilioni ya fedha ili Viongozi wa Chadema waache kumsema Mr. Monduli kuwa ni fisadi.

Mh.Zitto Kabwe anajitahidi kwa kila hali kuzuia mpango huo

Na Mwandishi wetu | Gazeti la Sauti Huru

Mmoja kati ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi(jina tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya siri na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Freeman Mbowe ili kuingia ubia na chama hicho.

Inaelezwa kuwa ,lengo la kigogo huyo ni kukiziba mdomo chama hicho kisimrushie makombora ya ufisadi kama walivyowahi kumrushia siku za nyuma.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa gazeti hili kwa muda mrefu sasa umebaini kuwa kigogo huyo wa CCM amekuwa na mawasiliano ya siri na ya karibu na Mbowe huku vikao vingi vikifanyika ndani ya hoteli moja ya kitalii iliyopo jijini Arusha (jina tunalo)

Imebainika kuwa ndoa hiyo ya siri ni ya wanasiasa hao wawili,lakini ikilenga uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kigogo huyo wa CCM amemuahidi Mbowe kwamba wataunda "serikali ya umoja wa kitaifa" endapo Mbowe atasaidia kuacha kumuandama kwa tuhuma za ufisadi na kuwadhibiti viongozi wengine wa chama chake, kutofanya hivyo kwenye maandamano na mikutano yao ya hadhara, pamoja na kwenye mahojiano na vyombo vya habari.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa tayari kigogo huyo amempa mwenyekiti huyo wa CHADEMA kiasi kikubwa cha fedha ili chama hicho kinapoendelea na kampeni yake ya bomoa-bomoa mafisadi yeye asiguswe kabisa, kama hatua ya kumfikisha ndoto yake ya kutaka chama tawala kumteua kuwa mgombea wa nafasi ya urais.

Chanzo chetu cha uhakika kikiongea na Sauti Huru kwa sharti la kufichwa jina lake kimedai " huu mpango unafanywa kwa siri kubwa na ninajua hata mhusika (anamtaja) akijua habari hii imetoka atafadhaika sana"


Habari zaidi zinadai kwamba kigogo huyo amefikia hatua hiyo baada ya kusoma alama za nyakati na kuona kwamba uwezekano wa mwenyekiti wa chama chake kumuunga mkono ni mdogo, hivyo hatoweza kupenya katika kinyang'anyiro cha uraisi 2015.

" Huyu bwana amesoma alama za nyakati ,ameona kabisa uwezekano wa kuungwa mkono na mwenyekiti wake(wa CCM) ni mdogo sana hivyo ni lazima atafute njia nyingine hata kama njia hiyo itakuwa na madhara kwa chama chake", kilieleza chanzo hicho na kufafanua;

"Si kwamba hajui mwenyekiti atalalia wapi, anajua lakini yuko tayari hata kukisaliti chama ili wote wakose,hivi ninavyoongea nanyi watu hawa wana mawasiliano ya kila mara juu ya suala hili ila Mbowe kaweka ngumu kuwa lazima waandikishiane ajue kabisa endapo (kigogo huyo atafanikiwa kuingia madarakani basi wataunda government of unity(serikali ya umoja wa kitaifa)".

...Aidha imefafanuliwa kwamba habari hizi zimeweza kumgusa hata Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zitto Kabwe, lakini kwa namna ya pekee Zitto ameweza kudhoofisha mkakati huo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni 'unafiki kwa Mbowe'

"Mtakumbuka siku za hivi karibuni Zitto alishutumiwa na chama chake kwa madai ya kuwa na uhusiano wa mashaka na Idara ya Usalama wa Taifa. Chadema wamekuwa wakidai kwamba Zitto anatoa siri za chama chao nje na hata kumuundia kamati ya wazee kumshauri?" alihoji.

Aliendelea:" Kilichotokea katika kamati hiyo siku walipokutana na Zitto ilikuwa tofauti kabisa, Zitto akawabadilishia mada pale alipowaambia wazee,'jamani ugomvi wangu na Mbowe ni pesa za chama, anatumia chama hiki hiki kupata fedha toka nje ya nchi na ndani ya nchi, lakini ninapojaribu kumkosoa kuwa tabia hiyo si nzuri kwa mwenyekiti wa chama ananijia juu,nyie mnajua kuwa amepokea fedha mamilioni kutoka kwa(anamtaja kigogo huyo) kwa ajili ya kutunyamazisha tusipige kelele za ufisadi dhidi yake?' "

"Hivi hamjui tayari anafanya mazungumzo na mtu wa CCM kwa ajili ya power sharing ya mwaka 2015?"

Kwa mujibu wa habari hiyo ni kwamba kigogo huyo atafanya kila liwezekanalo CCM imteue kuwa mgombea wa nafasi ya uraisi; lakini anajua hilo litawezekana endapo kelele za ufisadi dhidi yake zitamalizika.

"Huyu mtu ni mjanja sana na kwa sasa ana nguvu na mtandao mkubwa ndani ya CCM unaoweza kumfanya ateuliwe na chama kuwa mgombea, si hilo tu anajaribu hata kutafuta nguvu nje ya nchi ili endapo akikataliwa aweze kuwa na cha kuieleza jumuiya za kimataifa,"

"Na kwa hatua aliyofikia ni kwamba endapo hatoteuliwa hasa kutokana na ufisadi wake,yuko tayari hata chama chake kipoteze nafasi ya uraisi kitu ambacho kinaonyesha kuwa hana sifa za kiuongozi isipokuwa ni tamaa ya utawala."

Source: Gazeti la Sauti Huru

My Take:
Wale viongozi wa Chadema na wakereketwa waliopo humu JF watuthibitishie hii habari kama ni kweli.​


Last edited by nickname; 31st March 2011 at 18:13.​

SAUTI HURU siyo Gazeti, ni kipeperushi cha CCM miaka nenda miaka rudi, tupa kuleeeeeeeeee!!!!!!!!
 
Wapuuzi ninyi.

chadema hakimtambui mtu anayeitwa Jonathan Bahweje, msemaji wa Chama kanda ni mwenyekiti Aman Golugwa.


Peleka ushuzi wako kwako siyo chadema

Mmemkana katibu mkuu babu daktari wa kanoni padri Dr.W.Slaa itakuwa Jonathan?

Pesa mwanaharamu.
 
Last edited by a moderator:
yaani we dume la mende kweli umekurupukia chooni hahaahaahha na propaganda mfu toka lumumba wanakafuga misukule
 
Kama wewe ni mfanya biashara hilo deal haaliwezi kukupita chama hakina aset. Aset ni watu na watu mda wowote wanaweza kubadilika. Biashara kwanza mabaadiliko baadaye
 
Alisema Mwenyekiti wa CCM, wenye njaa tu ndio wamenunulika, walioshiba na wenye uchungu na Tanzania hao mmeanza kuwaona
 
huu mkoa si ndio upo nyuma kimaendeleo kuliko mikoa yote?
 
Dume la Membe hii ni nakala au ndiyo taarifa yenyewe. Lazima utakuwa umesahau kanuni za official letters.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom