CHADEMA tamkeni wazi kumtambua JK (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Kweli upuuzi hauna bei. Ile ni ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano(feki) wa Tanzania. Mpangaji wetu mle kawekwa na Tume ya uchaguzi anatambuliwa kwa kutangazwa. Ofisi haijafungwa mpaingaji ndiye mvamizi; CDM wanachofanya ni kumuonyesha kwa vitendo uwezo walionao wakiwaungwa mkono wananchi waliowengi .
 
Pasco unajishushia heshima yako.
This is too low .... Lakini mambo yako siku hizi yanaonyesha ulipo.
VGL, actions speak louder than words, Chadema hawana haja ya kusema wanamtambua, mambo mengine yanamalizwa kuitu uzima tuu. Nilishawaambia siku nyingi kuhusu hilo katika thread yangu ya "Chadema Wamtambua JK Kinyemela", that was then, now sio kinyemela tena bali ni mambo hadharani!.
 
Nitakufuata popote Pasco unipe jibu, hata kama utakwepa. Ulikula kiapo kwamba KAMWE JK hatakutana na CHADEMA na LAZIMA atausaini muswada kabla ya tarehe 01/12/2011. Jambo mojawapo limeonekana ni UONGO wako (la kutokutana na CHADEMA kamwe!). Unatoleaje ufafanuzi uongo wa kiapo chako hicho? Mimi huwa sipendi watu waongo wachangie humu JF
Jabulani, huna haja ya kunitafuta popote as if sionekaniki. Mimi nipo tuu hapa jf 24/7 hivyo nipo sana.

Ni kweli nilikula kiapo kile na niliapa JK hakutani na yoyote kabla hajasaini!. Alipowaona Chedama jana aliwaambia hajasaini?.

Wewe hujawahi kulea mtoto au hata mdogo wako?. Hivi hujaona mtoto akililia sana kitu fulani, akipewa pipi hunyamaza?!.

Unazungumzia hizo pipi za Ikulu jana kwa jina la chai na vitafunwa?. Hivi hukuwaona walivyo kuwa wanatabasamu kwenye ile picha?. Unaijua sababu?.

Umeisoma taarifa ya Ikulu kuhusu mkutano wa jana, taatifa imesema hajasaini?.

Tarehe 1 sheria mpya in force!.
 
Pasco unajishushia heshima yako.
This is too low .... Lakini mambo yako siku hizi yanaonyesha ulipo.
Memo, mtu anaweza tuu kujishushia heshima kama hiyo heshima yenyewe anayo!. Very unforunately mimi ni mtu wa chini siku zote, down the earth ground zero usawa wa vumbi.

Kauli zangu ndio ukweli wangu na ni ukweli mchungu. Tafuta ile thread yangu ya Chadema kumtambua JK uicheki ni ya lini mpaka jana walipokutana ni lini!.

Naomba kutoa rai kwa Chadema na wapenzi wao, CCM iko taaban imekaa mkao wa kifo. Chadema ndio yenye matumaini ila inakabiliwa na vi homa homa vya msimu. Sisi tunaigawa dose chungu kwa Chadema, ndio tutakao iponya Chadema na sio nyie mnaoiimbia nyimbo na sifa, shangwe na mapambio!.
 
Jabulani, huna haja ya kunitafuta popote as if sionekaniki. Mimi nipo tuu hapa jf 24/7 hivyo nipo sana.

Ni kweli nilikula kiapo kile na niliapa JK hakutani na yoyote kabla hajasaini!. Alipowaona Chedama jana aliwaambia hajasaini?.

Wewe hujawahi kulea mtoto au hata mdogo wako?. Hivi hujaona mtoto akililia sana kitu fulani, akipewa pipi hunyamaza?!.

Unazungumzia hizo pipi za Ikulu jana kwa jina la chai na vitafunwa?. Hivi hukuwaona walivyo kuwa wanatabasamu kwenye ile picha?. Unaijua sababu?.

Umeisoma taarifa ya Ikulu kuhusu mkutano wa jana, taatifa imesema hajasaini?.

Tarehe 1 sheria mpya in force!.
Usizungumzie kusaini muswada, kwa sasa nataka uzungumzie kiapo cha kutokutana na CHADEMA kamwe ulichokitoa! Mbona unakwepa?
 
Jamani wale wote mliochangia kwa kusema mnakumbuka msiwe waoga kwa kuwaogopa wachangiaji kama kina Pasco msukuma mwenzangu huyu.ni ukweli usio na shaka kwamba CDM hawakusema hawamtabui raisi bali mchakato uliotumika,si suala la kukumbuka huo ndio ukweli,watu kama kina Pasco wana dream zao ndio maana wanatumia nafasi zao kujaribu kupotosha ukweli huku wakijificha eti hawana upande,lakini tunajua ya kwamba pasco uko upande gani,hata kama utajifanya popo lakini watu wanajua,ombi kwako ni kwamba usiendelee kujileta bad impression kwa wapenda maendeleo na wanaochukia dhuluma kwa taifa hili kwa kuandika vitu ambavyo watu watakudharau mwisho wa siku.Na hata juzi umekuwa ukipublisha JK hataonana na CDM sijui leo unasemaje?anyway we endelea na mpango wako,yawezekana una-long term plan kuwa ndani ya system ya kifisadi muda ujao na ndio maana unajaribu kutumia jukwaa hili kupotosha watu.labda utueleweshe kwa kinagaubaga ili nasi tukuunge mkono huenda una hoja lakini iweke vizuri tukuelewe ni nini hasa unatafuta au unataka kuiambia jamii.Na kwa wale mnaotaka tuingie sijui msituni au sijui tufanyaje nawashangaa kuona CDM wametumia njia hiyo bado mnabeza,tukiamua kuandamana napo mnasema hamlali kwa sababu ya peoplezzz power sasa tufanye je au kweli mnataka tuhame nchi ili muendelee kufanya ufisadi bila hata kukemewa japo hata mkikemewa bado mnaendela tu,na mmejidai kudandia hoja ya kupinga ufisadi nayo imewashinda kwa kuwa ninyi UFISADI si kitu haramu kwenu washabiki na wapenzi na wanachama na viongozi wa CCM.Mungu awape huruma na kekima ya kutambua mambo haya.
 
Memo, mtu anaweza tuu kujishushia heshima kama hiyo heshima yenyewe anayo!. Very unforunately mimi ni mtu wa chini siku zote, down the earth ground zero usawa wa vumbi.

Kauli zangu ndio ukweli wangu na ni ukweli mchungu. Tafuta ile thread yangu ya Chadema kumtambua JK uicheki ni ya lini mpaka jana walipokutana ni lini!.

Naomba kutoa rai kwa Chadema na wapenzi wao, CCM iko taaban imekaa mkao wa kifo. Chadema ndio yenye matumaini ila inakabiliwa na vi homa homa vya msimu. Sisi tunaigawa dose chungu kwa Chadema, ndio tutakao iponya Chadema na sio nyie mnaoiimbia nyimbo na sifa, shangwe na mapambio!.

sawa baba tupo pamoja...tunataka opportunist wote wanaojiita wanasiasa ndani ya CDM waondoke..offcourse tunaanza na .....!
 
Pasco, wewe kama mwandishi wa habari unapaswa kuwa makini zaidi ya hapo. Hivi wewe ulitaka Chadema waingie msituni kuanzisha vita? Maana ktk mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola tunaoufuata, kutoka nje ni desturi ya kawaida kuonesha hisia ya kutoinga mkono jambo, hata samwel Sitta amewahi kutamka hivyo. Chadema wana uhakika wameibiwa kura, na wana uhakika hawezi kumtoa kwa mujibu wa katiba. wafanyaje sasa? Tuhame nchi twende kenya? Acha ushabiki wa kiccm inayokufa very soon.

chadema hawana ubavu wa kuanzisha vita...unless opportunist wa maisha waondoke..haitawezekana!
 
Dhana za Chadema zinapotoshwa makusudi! Hata ahadi ya kuanza mchakato wa katiba ndani ya siku 100 hadi Rais anaipotosha! Mkuu Pasco ni vyema kuwa mtu huru ktk kukosoa lakini usitake uonekane huru kwa kukosoa tuuu mpaka unapotosha! Nakuheshimu sana kwasababu naijua nafasi yako! Hukosoi kwa namna ya kujenga hata kidogo bali kujionesha huna upande tena kwa kupotosha.hebu uliza motive ya cdm wakati ule ilikuwa nini na imefanikiwaje pengine utaelewa! Usitumie jina lako na heshima unayopewa humu na kwenye media house nyingi hapa Bongo kupotosha hoja nyingi makusudi! Hoja zako hazijengi bali kubomoa na tena huwa unasubiri "yaharibike" useme! Si vizuri mkuu! Nakushauri tu naamini utanisikia ingawa mimi ni mtu mdogo sana! heshima mbele mkuu.
Mtazamo, kama na wewe unadhani ukosoaji wangu kwa Chadema una ill motives behind, you are very wrong!.

Nimenote wapenzi wa Chadema humu jukwaani mnakuja juu sana chama chenu 'kitakatifu', kinapokosolewa!. Mbona kinaposifiwa hamsemi!. Ni mara ngapi humu jf nimeisifu Chadema?.

Wale mnaomini mimi ni CCM hivyo humu nimetumwa kuisakama Chadema, endeleeni kuamini hivyo. Ni heri kuwa na mfuasi mmoja mkweli kuliko wafuasi elfu moja ambao ni washabiki tuu wanaoshabikia kwa mkumbo!.
 
Alaah!kumbe mswaada umeshasainiwa?Pasco mbona umechelewa kutuambia wenzio tusio kuwa na network?mbona umetukalia kimya au muda muafaka ndio huu,maana inavyoonekana wewe unataarifa na unauhakika ya kwamba JK alishausaini mswaada huo,au mwenzetu ni number 10 maana tunaweza kudhaini wewe ni mtu wa kalamu tu kumbe hiyo ni comouflage tu,kama ni number ten basi yawezekana kweli una habari na ndio maana unauhakika ya kwamba umeshasainiwa.basi kama ni hivyo ungetoa taarifa hata hawa CDM wasingeenda huko maana unaonyesha unajua kila kitu kinachoendelea ikulu.Tufafanulie ulishasainiwa tayari au utasaniwa?maana taarifa ya Rweyemamu haikuwa na kichwa wala mguu ni mambo ambayo tunajua lazima yaandikwe hivyo kwani hata kwa Jairo hivi juzi Luhanjo alitoka ki hivyo,sasa wewe unategemea taarifa ya ikulu itasema CDM wanasema katiba ni mbovu?ninachotegemea mimi ni kupishana kwa kauli katika mazungumzo hayo kila upande utatoka na kauli yake,sasa ukweli tutaupima kwa kuangalia pia uadilifu.
 
Mtazamo, kama na wewe unadhani ukosoaji wangu kwa Chadema una ill motives behind, you are very wrong!.

Nimenote wapenzi wa Chadema humu jukwaani mnakuja juu sana chama chenu 'kitakatifu', kinapokosolewa!. Mbona kinaposifiwa hamsemi!. Ni mara ngapi humu jf nimeisifu Chadema?.

Wale mnaomini mimi ni CCM hivyo humu nimetumwa kuisakama Chadema, endeleeni kuamini hivyo. Ni heri kuwa na mfuasi mkweli mmoja, kuliko wafuasi elfu moja!.

They trust politicians! kupenda upofu kaka....!!
 
Alaah!kumbe mswaada umeshasainiwa?Pasco mbona umechelewa kutuambia wenzio tusio kuwa na network?mbona umetukalia kimya au muda muafaka ndio huu,maana inavyoonekana wewe unataarifa na unauhakika ya kwamba JK alishausaini mswaada huo,au mwenzetu ni number 10 maana tunaweza kudhaini wewe ni mtu wa kalamu tu kumbe hiyo ni comouflage tu,kama ni number ten basi yawezekana kweli una habari na ndio maana unauhakika ya kwamba umeshasainiwa.basi kama ni hivyo ungetoa taarifa hata hawa CDM wasingeenda huko maana unaonyesha unajua kila kitu kinachoendelea ikulu.Tufafanulie ulishasainiwa tayari au utasaniwa?maana taarifa ya Rweyemamu haikuwa na kichwa wala mguu ni mambo ambayo tunajua lazima yaandikwe hivyo kwani hata kwa Jairo hivi juzi Luhanjo alitoka ki hivyo,sasa wewe unategemea taarifa ya ikulu itasema CDM wanasema katiba ni mbovu?ninachotegemea mimi ni kupishana kwa kauli katika mazungumzo hayo kila upande utatoka na kauli yake,sasa ukweli tutaupima kwa kuangalia pia uadilifu.
Jigoku, kwani Alhamisi ni mbali?. Si mtaambiwa na wahusika wenye kazi ya kuwaambia!. Haraka za nini?.
 
Pasco is no longer credible in JF. Invisible, tafuta reporter mwingine wa matukio mbalimbali kuliko mtu mwenye kuweka dhahiri hisia za chama chake humu, abaki tu member wa kawaida kama Malaria Sugu, Rejao na FaizaFoxy
 
Siasa inalipa jamani,acheni kuongea ongea tu,...
tafuteni jimbo mle MILEHAAAAAAAA,.....NATAMANI MBUNGE WANGU AFE
 
tumshuru na kumpongeza kikwete kwa kukubali kwake kukaa meza moja na wapinzani wake ambao kila kukicha wanamtukana na kumkejeli kama aweda alivyomkejeli na kumtukana kwa kumfananisha na baba mbakaji....kwa msomi kama aweda jinsi ninavomfaham sikutarajia atumie maneno ya dharau na yasiyoenda shule kama yale.....kikwete alipata asilimia 61 ya kura zote tanzania.chama chake kilipata wabunge zaidi ya 200 kati ya zaidi ya 350.takwimu za chadema na upinzani zinajulikana kwa idadi na asilimia.....sasa unapoandika kejeli apa kwenye forum ambayo inasomwa na watu wenye akili zao waliosambaa dunia nzima huoni kuwa unajidhalilisha?????????????nawapongeza makamanda wa cdm kuamua kukaa meza moja na kikwete kuzungumzia mustakabali wa taifa letu changa la Tanzania.
 
tumkushuru na kumpongeza kikwete kwa kukubali kwake kukaa meza moja na wapinzani wake ambao kila kukicha wanamtukana na kumkejeli kama aweda alivyomkejeli na kumtukana kwa kumfananisha na baba mbakaji....kwa msomi kama aweda jinsi ninavomfaham sikutarajia atumie maneno ya dharau na yasiyoenda shule kama yale.....kikwete alipata asilimia 61 ya kura zote tanzania.chama chake kilipata wabunge zaidi ya 200 kati ya zaidi ya 350.takwimu za chadema na upinzani zinajulikana kwa idadi na asilimia.....sasa unapoandika kejeli apa kwenye forum ambayo inasomwa na watu wenye akili zao waliosambaa dunia nzima huoni kuwa unajidhalilisha?????????????nawapongeza makamanda wa cdm kuamua kukaa meza moja na kikwete kuzungumzia mustakabali wa taifa letu changa la Tanzania.
 
''Mtatoka nje lakini mtarudi tu kwasababu mimi ninabaki kuwa Rais wenu na hamna mwingine wa kumkimbilia mtakapokuwa na matatizo''- Jakaya Kikwete on Chadema's decision of boycotting his 10th Parliament inauguration speech.

Mtatoka nje lakini mtarudi ndani wapi? Hivi ndani una maanisha ndani ya jengo la Bunge au Ikulu. Hivyo vyote, hakuna ambacho kikwete ni mmliki wake au ni mali yake. Vyote alivikuta na ataviaacha. Hakuna kilichojengwa kwa mshahara wake. Vyote hivi ni ofisi za watanzania siyo ya Kikewte wala ccm.
Tunachofanya chadema ni kutumia hekima ili tusivuruge nchi yetu. Chadema siyo waajiriwa wa Kikwete, tuko kwa ridhaa ya watanzania na hakuna mtanzania mwenye haki zaidi ya mwingine. Wanachadema ni watz kama walivyo jk na wanaccm wote.
 
Back
Top Bottom