CHADEMA tamkeni wazi kumtambua JK (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA tamkeni wazi kumtambua JK (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Nov 28, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jana tarehe 27/11/2011 JK alikutana na ujumbe wa CHADEMA Ikulu kwa mazungumzo ya mchakato wa kupata katiba mpya. Mazungumzo hayo yanaendelea leo tarehe 28/11/2011. Nakumbuka kwamba CHADEMA waliwahi kutamka kwamba hawatambui kama JK ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Hoja yangu ni kwamba kama wamekutana naye kama Rais wa nchi, basi watoe tamko la kumkubali.
   
 2. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Kwani yeye ameshatamka nani Gamba au ametoa tamko la kuwavua Gamba CHEL?????
   
 3. Magwangala

  Magwangala JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 2,005
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  unafikiri kwa kutumia nini vile?Ni lini CDM walisema hawamtambui Kikwete kama rais?
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @VGL, CHADEMA hawakuhi kusema hawamtambui Rais, na hata msingi wa kutoka bungeni wakati rais Kikwete anahubutubia bunge sio kwamba hawamtambui ila hawakubaliani na MCHAKATO uliotumika kumpa kura za ushindi. Hili ndilo dai la CHADEMA na ndio sababu kuu ya kutaka katiba mpya kwa sababu kwa katiba iliyopo sasa tume ya uchaguzi inakuwa chini ya rais hivyo haipo huru, na mbaya zaidi hata pale tume inapofanya makosa kwenye kusimamia uchaguzi wakishaamtanga mshindi wa urais haku
  na mtu au chombo chochote kinachoruhusiwa kuhoji!

  Kwenye uchaguzi uliopita (2010) CHADEMA walijaribu sana kuiasa NEC wasitishe kutangaza matekeo ya kura za urais hadi pale watakapohakiki kura toka sehemu mbalimbali. Ushahidi wa madai yao (CHADEMA) walionesha lakini NEC kwa sababu haiko huru, ni tume ya ofisi moja ilifanya kama bosi wao alivyowataka - wakatangaza matokeo yenye utata.

  Hii ni kinyume kabisa na kanuni za utawala bora na vizuri tukajitahidi kuweka ushabiki wa kiitakadi na tukajitahidi kuelewa madhara yake kwa ustawi wa taifa.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wameenda kucheki kama bado ni yeye yupo.
  kwani alivamia ikulu.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  VGL, actions speak louder than words, Chadema hawana haja ya kusema wanamtambua, mambo mengine yanamalizwa kuitu uzima tuu. Nilishawaambia siku nyingi kuhusu hilo katika thread yangu ya "Chadema Wamtambua JK Kinyemela", that was then, now sio kinyemela tena bali ni mambo hadharani!.
   
 7. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Nakuuliza swali gumu, sikutukani,

  Hivi mama yako akikuambia kuwa baba yako alinibaka, nikapata mimba, ndo ukazaliwa wewe mwanangu VGL. utamkana baba yako hata kama ubakaji ni kosa la jinai? Huwezi kukana kwa sababu huo ndio ukweli ambao huwezi kuubadili. Baba yako ni baba yako bila kujali alitongoza au alibaka.  Je, baada ya Chadema kuwa na uhakika kuwa kura zao zimechakachuliwa (mimi nina ushahidi wa jimbo la ubungo, na baada ya kutangazwa na tume ya Taifa ( ambao mpaka leo wameshindwa kuweka vizuri ktk website yao vizuri ya Tume) Chadema wangefanya nini? Kwa mujibu wa katiba hii mbovu, kikwete ni Rais mara tu baada ya kutangazwa na tume ya uchaguzi. Hakuna mahakama ya kupinga kutangazwa kwake na si ushindi wake. Elewa. Kwangu mimi mshindi ni Dr Slaa. Huu ndio ukweli mchungu.
  Chadema hajawahi kusema hawamtambui rais, na hawawezi kufanya hivyo kikatiba, ila waliwahi kulalamika baba yao ( Rais) kubaka demokrasia akisaidiwa na tume na usalama wa ccm aka Taifa?)
   
 8. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  ninachokumbuka CDM waliwahi kusema kuwa hawatambui mfumo uliotumika katika uchaguzi na kumpa ushindi. Ila hawajasema kuwa hawamtambui yeye kama Rais
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Dhana za Chadema zinapotoshwa makusudi! Hata ahadi ya kuanza mchakato wa katiba ndani ya siku 100 hadi Rais anaipotosha! Mkuu Pasco ni vyema kuwa mtu huru ktk kukosoa lakini usitake uonekane huru kwa kukosoa tuuu mpaka unapotosha! Nakuheshimu sana kwasababu naijua nafasi yako! Hukosoi kwa namna ya kujenga hata kidogo bali kujionesha huna upande tena kwa kupotosha.hebu uliza motive ya cdm wakati ule ilikuwa nini na imefanikiwaje pengine utaelewa! Usitumie jina lako na heshima unayopewa humu na kwenye media house nyingi hapa Bongo kupotosha hoja nyingi makusudi! Hoja zako hazijengi bali kubomoa na tena huwa unasubiri "yaharibike" useme! Si vizuri mkuu! Nakushauri tu naamini utanisikia ingawa mimi ni mtu mdogo sana! heshima mbele mkuu.
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kazi ya chadema ni kutanga raisi wa tanzania?
  wapi na lini walisema hawamtambui raisi wa tanzania.....
   
 11. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mtoa hoja, naomba uelewe mara baada ya uchaguzi Chadema walionyesha ukomavu wa hali ya juu sana kwa kuwaambia wapigakura na mashabiki wao wasubirini watatoa tamko, maana wangetamka lolote wakati ule, tungerudia ya kenya, nadhani hata JK anawashukuru sana kwa hilo...... na ndio ukomavuuuu wa kisiasa
   
 12. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Pasco, wewe kama mwandishi wa habari unapaswa kuwa makini zaidi ya hapo. Hivi wewe ulitaka Chadema waingie msituni kuanzisha vita? Maana ktk mfumo wa mabunge ya jumuiya ya madola tunaoufuata, kutoka nje ni desturi ya kawaida kuonesha hisia ya kutoinga mkono jambo, hata samwel Sitta amewahi kutamka hivyo. Chadema wana uhakika wameibiwa kura, na wana uhakika hawezi kumtoa kwa mujibu wa katiba. wafanyaje sasa? Tuhame nchi twende kenya? Acha ushabiki wa kiccm inayokufa very soon.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mfano mzuri sana naamini atakuwa amekuelewa.....
  njia tuliyokuwa nayo chadema labda kuingia vitani je ndiyo ilikuwa furaha ya VGL.....
   
 14. Game Theory I

  Game Theory I Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pagumu hapo.Jamaa majuha kweli.Sijui waliyekutana naye ni nani.
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hoja ni Katiba...Mambo ya kutambuana au la yaliisha zamani!...Unasemaje kuhusu muswada unaoelekea kusainiwa na rais?
   
 16. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Nitakufuata popote Pasco unipe jibu, hata kama utakwepa. Ulikula kiapo kwamba KAMWE JK hatakutana na CHADEMA na LAZIMA atausaini muswada kabla ya tarehe 01/12/2011. Jambo mojawapo limeonekana ni UONGO wako (la kutokutana na CHADEMA kamwe!). Unatoleaje ufafanuzi uongo wa kiapo chako hicho? Mimi huwa sipendi watu waongo wachangie humu JF
   
 17. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tumejaliwa kuwa na wasomi lakini tuna upungufu ya wajuzi i.e wenye ufahamu kielimu wengine huwaita think tanks, ama magwiji wa fikra. kinachowasumbua wengi wetu ni kutathmini mambo kijuu juu kiasi kwamba hawaelewi hoja zinazojadiliwa vema. Na matokeo yake kupoto ukweli. CDM hawakuwahi kusema hawamtambui rais, wanaijua vyema sana katiba ya nchi, kutomtambua rais ni uhaini. Hawakubaliani na mchakato uliomwingiza rais madarakani. Rais anajiundia tume anaiita tume ya uchaguzi, wanatumia ofisi za serikali, wasimamizi wakuu wa majimbo ni wakurugenzi wa halmashauri, wanapojumlisha matokeo wana hiyari ya kukaribisha mawakala wa vyama ama la, wakitangaza matokeo (waliyojumlisha wenyewe) hakuna chombo chochote cha kuwahoji. Kwa mfumo huo hata watu 5000 tu kati ya 20,000,000 wanaweza kumwingiza rais madarakani.
  Pili CDM hawaupingi muswada wa marekebisho ya katiba kama JK na wabunge wake wanavyotaka umma uamini, wanapinga kupitisha muswada huo kinyume na kanuni za bunge kwa kutumia ubabe wa spika na wingi wa wadandia hoja.
  Mengine yamefafanuliwa na wachangiaji wengine.
   
 18. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ''Mtatoka nje lakini mtarudi tu kwasababu mimi ninabaki kuwa Rais wenu na hamna mwingine wa kumkimbilia mtakapokuwa na matatizo''- Jakaya Kikwete on Chadema's decision of boycotting his 10th Parliament inauguration speech.
   
 19. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachokumbuka ni kwamba Chadema walisema hawatambui mchakato mzima uliomweka JK madarakani, lakini kwa vile ndiye aliyetangazwa na tume kwamba ndiye mshindi hawakuwa na njia nyingine ya kumpinga kisheria na kikatiba, ndiyo maana walitoka nje ya bunge wakati rais analihutubia bunge ili kuonyesha hisia zao, baada ya hapo walirejea kuendelea kuijadili hotuba ile. Katu hawajawahi kusema hawamtambui rais kwani katiba imeshaeleza wazi akishatangazwa na tume ndiye raisi!!!! Wanaofikiria kwa kutumia masaburi kama wewe ndio wanaoeneza upotoshaji huu
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  du huu mfano mgumu kweli
   
Loading...