CHADEMA Siwaelewi mnachokisimamia

Sodium 23

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
482
489
Wakuu nmeamua kufunguka kwa hawa ndugu zetu CHADEMA kufuatia kukithiri siasa za matukio na kubadili gia angani. Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambao aidha walibadili gia angani au yalipotea bila utekelezaji:
1. UFISADI; Mkiwa mwembeyanga mlituaminisha Lowassa ni fisadi, mlisimamia hilo kwa takribani miaka saba lakini ndani ya masaa mkataka kutuaminisha sio fisadi
2. ILANI YA UCHAGUZI; mlituaminisha kuwa Magufuli anatekeleza ilani ya CHADEMA lakini hata mwaka mnasema ni dikteta. Nawasubiri mtengue kauli kwamba JPM hakuiga sera zenu
3. MSIBA WA ARUSHA. Mnatuaminisha kwamba RC wa Arusha amekula rambirambi lakini akihamia CHADEMA mtasema hajala rambirambi ila amekula pilau.
MY TAKE: Kuweni makini na watu wasiokuwa na hoja wala misimamo thabiti....Amini amini nawaambia Makonda akihojiwa Star TV ndo unakua mwisho wa stori za Mrisho gambo na upepo utabadilika itakua ni Makonda na Star TV.
Tujifunze kuweka akiba ya maneno
 
Hivi wanachokisimamia kwa sasa ni kusubiria matukio ya majanga kusafafisha wahujumu uchumi na mafisadi ndo gia ilivobadilishwa angani toka jeshi la ukombozi wanyoge
 
Hamuwezi kushinda Uchaguzi TanZania hata iweje, hata kama ikitokea Miujiza labda Watanzania siku moja wakawaamini na kuwapigia kura nyingi lkn bado hamtaweza kuiondoa CCM kwa maana mfumo wa Tanzania hauko tayari kwa hilo, na huwo ndiyo ukweli anzieni hapo kwanza, mengine yote ni kupoteza muda tu, ...
 
Kauli zilizowahi kutolewa na mmiliki mwenza wa Chadema Lowassa kwamba yeye ameshikilia amani ya nchi kwani watu kwa kauli yake wanaweza kuingia mitaani siyo kauli ndogo

Namhusisha pia na Maalim Seif kwamba vijana wanamsumbua wakitaka awape ruhusa walianzishe hiyo kauli aliitoa alipokuwa anahojiwa na kituo kimoja cha luninga.

Lowassa amekuwa akiirudia kauli hii kila apatapo nafasi kuelezea uchaguzi wa 2015 alivyotolewa kamasi.

Kinachoendelea Arusha kuhusu suala la watoto wetu waliofariki ni jambo la aibu kubwa ambapo Watanzania wenzetu viongozi wa siasa za upinzani wameshiriki kwa kiwango kikubwa kwenye aibu hii. Badala ya kuwafariji wafiwa na kuwaacha watoto wapumzike kwa amani watu hawa wamekuwa wakielezea umma propaganda za rambirambi za wafiwa huku wakijipa kazi ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu za rambirambi hio.

Sasa maombolezo yamegeuka mtaji wa kisiasa. Nakumbuka kauli ya Lema alipokuwa anaelezea kutopata nafasi kusema lolote uwanjani, alisema ....Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.... (Mwisho wa kunukuu). kwa wenye akili ya kutafakari unajua anachokitafuta Lema ni kuona nchi inaingia kwenye machafuko.

Mchungaji Msigwa (Mbunge) aliwahi kuonyeshwa katika video mitandaoni akitaka kutekeleza kwa vitendo sera ya chama chake kutaka kumpiga mkuu wa Wilaya Richard Kasesera....

Turudi kwa Sugu (Mbunge) amekuwa mara kwa mara akitaka kupigana ndani ya Bunge pale anapoona jambo analolazimisha kukataliwa.

Halima Mdee naye hivi karibuni amejadiliwa na Kamati ya Nidhamu na Hadhi ya Wabunge kwa kauli zenye uchu wa vurugu na kulivunjia heshima Bunge alizozitoa wakati Bunge linaendelea.

Inawezekana haya yanayofanyika leo watu wasijue nini hatima yake lakini ni wazi hawa ndugu zetu hawapo tayari kudumisha amani na mshikamano wa nchi yetu. Wapo tayari kuona watu wakifarakana na inawauma sana wanapoona serikali inatimiza wajibu wake ndiyo maana wanajitahidi kuchafua hali ya hewa kila inapobidi ili kuondoa utulivu wa kisiasa.

Mitandaoni hali ni tete kabisa, vitisho, kebehi hata wananchi ambao wengine walionyesha kushangilia pale polisi wetu walipopoteza maisha wakiwa kazini hata wengine waliokamatwa kwakuwatukana viongozi walijitokeza mawakili kutoka upinzani kuwatetea mahakamani.

Sijasema ya Tundu Lisu maana kila mmoja anajua nini mefanya, anafanya na matarajio yake kwa amani ya nchi yetu.

Ni wakati sasa wa Watanzania kupitia viongozi wao kuungana kuleta maendeleo chanya ikiwemo kushiriki shughuli za kiuchumi na kuhakikisha wanatekeleza sera za umoja wa kitaifa.

Kinyume na hapo, nawaambia CHADEMA kuwa roho za watanzania wasiziweke rehani kwa uchu wao wa madaraka. Wafanye siasa safi
 
Vichwa vya watu vingekuwa kama computer ningekununulia RAM hata GB4 ili thinking capacity yako iongezeke kidogo
Unajitoa fahamu mkuu.
Jaribu kuchunguza kauli na matendo ya viongozi wenu. vinatia mashaka makubwa.

Seems mmekosa upeo na mwelekeo
 
Hamuwezi kushinda Uchaguzi TanZania hata iweje, hata kama ikitokea Miujiza labda Watanzania siku moja wakawaamini na kuwapigia kura nyingi lkn bado hamtaweza kuiondoa CCM kwa maana mfumo wa Tanzania hauko tayari kwa hilo, na huwo ndiyo ukweli anzieni hapo kwanza, mengine yote ni kupoteza muda tu, ...
Hahahaaaaa,naona mmepanic!Hili ni povu la jazba baada ya kuelemewa na kuona hatari ya kupigwa chini mbeleni!
 
Chadema wlifurahi sana kufa wale watoto kule arusha....kila siku ni kiki za hao watoto...Chadema ni janga la Taifa
Siwez kufurahia vifo vya wale watoto, ila haya ya kibiti Naomba waongeze kasi. Baada ya mjumbe mmoja kwa wiki wapige watatu kwa siku.
 
Suala la vifo vya watoto Arusha tuachane nalo na tumuombe mora awapumzshe vzur. Kumbuken kua wazaz na ndugu wa hawa watoto tuna wakwaza sn na kuwaumuza nawaomben sn wakuu.
 
-Fao la kujitoa mkakimbia nalo
-Ajira za watoto wa chuo kikuu mkawapa makada wa ccm
-Mkaona hela ni ndogo mkaanza kula rambi kagera (ukitoa msiba sasa hiv ni wa ccm), Arusha macho kweupe, fisi ni fisi. Mnang'ang'aniza rambi rambi zijenge hospital. Inafika wakati serikali ya ccm inategemea rambi rambi ifanye maendeleo? Puuuuuuuuuuuuu mlaaniwe kbsa
-Mkaona haitoshi HELSB kutoka 8%-15% ili mle na familia zenu na mahawara zenu
-Mkaona haitoshi watoka pabaya increment mkalala nazo mbele, nyie mnalaana. Sijui mnakoelekea kwa huu mwelekeo wa rambi rambi mtahamisha mpaka vyuma vya reli mpate rambi rambi. CCM SASA HIV HAINA TOFAUTI NA PANYA ROAD
kazi mnayo mtajitetea hali mbaya hewa imesababisha bei ya nafaka imepanda bei sawa. SUKARI?
Eti bar zinafunguliwa saa 8, watu wafanye kazi. Nyie mbona ajira za vijana, mewapa makada wa ccm.? Puuuuuuuuu laana tupu. Ndiyo maana sasa hiv mnategemea rambi rambi. Vijana wameawaachia laana, wafia pia.
Mnajisumbua bure.
Sasa hiv Magufuli na Lowassa au kikwete na Magufuli, wakienda sehemu kwa pamoja Lowassa au Kikwete ataonekana ndiyo rais
 
Hivi una akili timamu kweli wewe?? Mbona mnapotoshwa na mambo ya siasa??? Muwe na mipaka? Mtu anawezaje kufurahia watoto wa wenzake kufa?? Labda ni wewe tu na ccm wenzio mnaokula rambirambi zao.
Kwa niaba ya chama changu nawaombeni radhi wafiwa na ndugu na jamaa,kuna watu humu jukwaani lengo lao ni kuamsha maumivu ya msiba.ndugu zangu chadema sisi ni watani wa jadi.
 
Back
Top Bottom