Kauli zilizowahi kutolewa na mmiliki mwenza wa Chadema Lowassa kwamba yeye ameshikilia amani ya nchi kwani watu kwa kauli yake wanaweza kuingia mitaani siyo kauli ndogo
Namhusisha pia na Maalim Seif kwamba vijana wanamsumbua wakitaka awape ruhusa walianzishe hiyo kauli aliitoa alipokuwa anahojiwa na kituo kimoja cha luninga.
Lowassa amekuwa akiirudia kauli hii kila apatapo nafasi kuelezea uchaguzi wa 2015 alivyotolewa kamasi.
Kinachoendelea Arusha kuhusu suala la watoto wetu waliofariki ni jambo la aibu kubwa ambapo Watanzania wenzetu viongozi wa siasa za upinzani wameshiriki kwa kiwango kikubwa kwenye aibu hii. Badala ya kuwafariji wafiwa na kuwaacha watoto wapumzike kwa amani watu hawa wamekuwa wakielezea umma propaganda za rambirambi za wafiwa huku wakijipa kazi ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu za rambirambi hio.
Sasa maombolezo yamegeuka mtaji wa kisiasa. Nakumbuka kauli ya Lema alipokuwa anaelezea kutopata nafasi kusema lolote uwanjani, alisema ....Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.... (Mwisho wa kunukuu). kwa wenye akili ya kutafakari unajua anachokitafuta Lema ni kuona nchi inaingia kwenye machafuko.
Mchungaji Msigwa (Mbunge) aliwahi kuonyeshwa katika video mitandaoni akitaka kutekeleza kwa vitendo sera ya chama chake kutaka kumpiga mkuu wa Wilaya Richard Kasesera....
Turudi kwa Sugu (Mbunge) amekuwa mara kwa mara akitaka kupigana ndani ya Bunge pale anapoona jambo analolazimisha kukataliwa.
Halima Mdee naye hivi karibuni amejadiliwa na Kamati ya Nidhamu na Hadhi ya Wabunge kwa kauli zenye uchu wa vurugu na kulivunjia heshima Bunge alizozitoa wakati Bunge linaendelea.
Inawezekana haya yanayofanyika leo watu wasijue nini hatima yake lakini ni wazi hawa ndugu zetu hawapo tayari kudumisha amani na mshikamano wa nchi yetu. Wapo tayari kuona watu wakifarakana na inawauma sana wanapoona serikali inatimiza wajibu wake ndiyo maana wanajitahidi kuchafua hali ya hewa kila inapobidi ili kuondoa utulivu wa kisiasa.
Mitandaoni hali ni tete kabisa, vitisho, kebehi hata wananchi ambao wengine walionyesha kushangilia pale polisi wetu walipopoteza maisha wakiwa kazini hata wengine waliokamatwa kwakuwatukana viongozi walijitokeza mawakili kutoka upinzani kuwatetea mahakamani.
Sijasema ya Tundu Lisu maana kila mmoja anajua nini mefanya, anafanya na matarajio yake kwa amani ya nchi yetu.
Ni wakati sasa wa Watanzania kupitia viongozi wao kuungana kuleta maendeleo chanya ikiwemo kushiriki shughuli za kiuchumi na kuhakikisha wanatekeleza sera za umoja wa kitaifa.
Kinyume na hapo, nawaambia CHADEMA kuwa roho za watanzania wasiziweke rehani kwa uchu wao wa madaraka. Wafanye siasa safi