Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,662
Dogo Zitto amenipunguzia sana kasi ya kupenda siasa na wanasiasa,mm pamoja na UCCM wangu nilikuwa natamani siku awe mwana ccm lakini asiyekuwa mamluki kama alivyo sasa. Namchukulia Zitto kama machagudoa walioko soko la vitunguu Mwanza.mimi mwenyewe ni mpiga kura wa zzk. . Kusema ukweli dogo watu hawakua na imani naye tena. Hata uchaguzi wa 2010 alipita kwa mbinde
huna hoja... Piga kimya
Sasa subirini leo Kigoma sukari itakaposhuka
picha ya tanzania daima siyo ya kweli bali ni yakugushi sijui wanamdanganya nani.
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?
Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kamwe chama hicho hakitakubali kuwa legelege katika kusimamia misingi yake, ikiwemo katiba inayowaunganisha wanachama wote.
Alisema kuwa licha ya kuzushiwa propaganda nyingi ikiwemo udini na ukabila, lakini chama hicho kimefanikiwa kuzishinda hali aliyoelezea imewakomaza katika safari yao ya kuchukua madaraka.
Kauli hizo alizitoa jana mjini Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa wananchi katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya CDT, ikiwa mwanzo wa ziara yake ya kukiimarisha chama.
Dk. Slaa alisema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010, chama hicho kiliwaahidi Watanzania kuwa kama kingeshika dola, kingekuwa imara kusimamia serikali itakayowatumikia wananchi.
Alibainisha kuwa ili kuitimiza ahadi hiyo, chama hicho kamwe hakiwezi kuwa legelege kwa wanachama na viongozi wasiotaka kufuata katiba na taratibu za chama.
Watanzania tulieni, tulieni, tulieni. Chama hiki kipo kwa ajili ya kuwatumikia ninyi na kusimamia maslahi yenu. Acheni ushabiki kwenye masuala mazito, alisema.
Dk. Slaa alisema amekuwa akipigiwa simu na watu wengi wakimuulizia hali ya mambo inavyokwenda ndani ya chama hicho, hasa baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwavua uongozi baadhi ya makada wake akiwemo mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Mimi nawaambia watulie tu Nawaambia waviamini vikao vya chama chao, ndani ya CHADEMA hakuna mtu mkubwa kuliko katiba. Wote hapa tunaunganishwa na katiba.
Chama hiki kimepita kila aina ya propaganda ikiwemo hii ya juzi ya ugaidi, zote tumezishinda na tutaendelea kuzishinda. Hata hii ya sasa inayosukumwa na mipango ya hujuma inayopangwa na CCM, wakishirikiana na vyombo vya dola na watendaji wa serikali, tunazidi kuimarika na kutukomaza kwenda kushika dola.
Wakati wa kampeni mwaka 2010 tuliwaambia Watanzania kuwa tunakwenda kusimamia maslahi ya Watanzania. Tulisema elimu bure, mwaka jana wameamua kutuiga, tulisema vifaa vya ujenzi vishuke, pia wameamua kutuiga, lakini wameshindwa kutekeleza, alisema kiongozi huyo huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi hao.
Dk. Slaa alisema kuwa CCM wameshindwa kutekeleza kile kilichokuwa kikisemwa na CHADEMA, ambayo sasa inaamini ikiingia madarakani itatimiza mambo iliyowaahidi wananchi.
Safari yapata matatizo
Ziara ya Dk. Slaa jana iliingia dosari baada ya magari aliyokuwa akiyatumia kupata hitilafu za kiufundi zilizosababishwa na kile kinachodaiwa ni mafuta machafu waliyoyaweka katika kituo kimoja cha mafuta kilichopo wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Mafuta hayo yaliyafanya magari yaliyokuwa kwenye msafara huo kushindwa kwenda mwendo uliotarajiwa, na hivyo kusababisha Dk. Slaa na timu yake kufika katika viwanja vya mkutano saa 12 jioni.
Dk. Slaa leo anatarajia kwenda mkoani Kigoma ambako atahutubia mikutano mbalimbali ya hadhara pamoja na kufanya shughuli za kuimarisha chama kila eneo atakalolitembelea.
Source:Tanzania Daima Alhamisi
Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria mkutano..........
Dr Slaa akiaga umati huo huku wananchi wakiwa na hamu ya kuendelea kumsikiliza..........
Poleni sana ule umati wa wanakahama ni pigo takatifu kwenu masalia na vimelea vyake vyote
Ile picha watu werevu waliishtukia kwa sababu Dr. Slaa kafika uwanjani saa 12 na robo lakini kwenye ile picha jua kali linawaka. Kahama saa 12 na robo hakuna jua kali!
Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai...
Mapambano yapi? Kati ya nani na nani?
Kuna picha za Nov 2011 ziliwekwa kwenye thread na Kurugenzi ya Habari CHADEMA zikidai ni mkutano ulifanyika Wilayani Kahama jana wakati ni ulaghai wa kiwango cha juu kabisa.
Imebidi MOD's waifunge hiyo thread.
Wananchi wameisha anza kuuelewa ulaghai wa CHADEMA na kwa sasa CHADEMA wako desparate mpaka wanachakachua picha.
Ukweli utaendelea kujipambanua kila siku
Mapambano yanaendelea....
Tatizo watu mnaanza kutukanana jamani why?
Naomba huyu anaejiita molemo atutajie kituo cha mafuta kilichowekwa mafuta machafu...maana ni kosa kabisa kisheria, sasa ataje hicho kituo sasa ili watu waamini kuwa mzee slaa alichelewa kufika kahama...nachojua slaa alifika kahama saa 9 alasiri lakini alishindwa kwenda uwanjani kwa idadi ndogo ya watu na aliambiwa kuna abango yamebebwa na ataweza kuzomewa lakini aliamua kukaa mpaka saa 11;30 aliponda uwanjani kusalimia tu wala hakuhutubia
Mapambano yapi? Kati ya nani na nani?
mi nilikuwepo mkuu watu walikuwa nyomi hadi juu ya miti asikwambie mtu
Pamoja na udaku wake ni moja ya gazeti linalopendwa hapa nchini na mauzo yake ni ya juu sana ukilinganisha na uhuru, habari leo, etcTanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Pamoja na udaku wake ni moja ya gazeti linalopendwa hapa nchini na mauzo yake ni ya juu sana ukilinganisha na uhuru, habari leo, etc
Mkuu Molemo kuna Gazeti linasema kwamba Dr. Slaa jana alizomewa na kufanyiwa vurugu huko Kahama na pia aliambulia idadi ndogo ya wananchi. Gazeti la Tanzania Daima linakuja na habari kwamba amehutubia mkutano mkubwa wa hadhara! Hivi sheria za nchi si ni kwamba mwisho wa kuhutubia mikutano ya hadhara ni saa kumi na mbili; sasa Dr. Slaa alifika saa kumi na mbili viwanjani, alihutubia saa ngapi?
Pia hapo kuna sauti ya tulieni, tulieni alikuwa akituliza nini? Siyo hizo vurugu ambazo tumeambiwa kuwa alifanyiwa?