lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,481
- Thread starter
- #81
Saccos ya mtei na watoto wake
Hivi unaweza kuitetea kweli CCM mbele ya watu wenye upeo mkubwa wa mambo ya siasa za vyama vingi kwa maneno mepesi namna hiyo? Au unaweza kuiangamiza CHADEMA kwa hoja dhaifu namna hii.Sasa hoja hizo ndo zinazoifanya CCM ya Kikwete kuonekana kama kijiwe cha wahuni,wapiga dili tu,tofauti na CCM ya enzi za Mwalimu iliyokua inatetewa na vijana mahili wa wakati huo kama akina Edward Moringe Sokoine,Salim Ahmed Salim,Paul Sozigwa n.k.lakini ninyi watetezi wa sasa hivi wa CCM kila kijana anamtetea mtu wake,sio chama.Unaweza kukuta wewe kwa uandishi wako unampigania mtu anaeitwa Mwigulu na wala sio CCM.Maana hicho ulichoandika ndizo kauli za Mwigulu,halafu anautaka Urais.