Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Analysis ya kipuuzi sijawahi kuona tangu nizaliwe. Eti unawaita wanaohudhuria mikutano ya Chadema kuwa ni vibaka, wazururaji na watu wasio na makazi maalum?! Ulifanya utafiti gani kulibaini hilo? Hata kama ushauri wako ni mzuri kiasi gani, umeshauharibu kwa kauli zako za kashfa. Ulipaswa utambue umuhimu wa hayo makundi yanayojaza mikutano ya Chadema kisha utoe huo ushauri wako.

Mikutano na maandamano ndani ya CHADEMA ni zaidi ya siasa mkuu kama haujui, kuna siri nzito imejificha huko, suala la kupata kura na watu wachache kujitafutia umaarufu ni vitu viwili tofauti. Mikutano ile inayoambatana na maandamano ni mahsusi kwa ajili watu wachache kujipatia umaarufu ha haizalishi watachaguliwa au la ilimradi umaarufu huo unawawezesha wao kula. Usitemegee waache.
Nimeipenda sana comment yako, maana kinachoongelewa kikidharaurika matokeo ndio ya kulalamikia kuibiwa kura kumbe wenzako wanaofukua mitaani kama mnyama FUKO wamefanikiwa kuwakokotoa wapiga kura. Siasa za leo zinaendeshwa kisayansi.
Nadhani ungefahamu maudhui ya habari zaidi. Kundi kubwa hilo si wapiga. Nani aliye kazini ataacha kazi na kwenda mkutanoni kuanzia na wewe mwenyewe mdau utaacha kazi uende mkutanoni wakati unawajibika?
Siasa za kuwatembelea watu majumbani ni ngumu kwa sababu lazima uwe na hoja ya kuwaambia watu na vilevile ujiandae kuwa na majibu ya maswali watakayouliza. Chadema hawawezi kujibu hoja face to face ndio maana wanapendelea kupanda jukwaani kusema maneno wanayotaka halafu wanatawanyika.
Analysis ya kipuuzi sijawahi kuona tangu nizaliwe. Eti unawaita wanaohudhuria mikutano ya Chadema kuwa ni vibaka, wazururaji na watu wasio na makazi maalum?! Ulifanya utafiti gani kulibaini hilo? Hata kama ushauri wako ni mzuri kiasi gani, umeshauharibu kwa kauli zako za kashfa. Ulipaswa utambue umuhimu wa hayo makundi yanayojaza mikutano ya Chadema kisha utoe huo ushauri wako.
Siasa za kuwatembelea watu majumbani ni ngumu kwa sababu lazima uwe na hoja ya kuwaambia watu na vilevile ujiandae kuwa na majibu ya maswali watakayouliza. Chadema hawawezi kujibu hoja face to face ndio maana wanapendelea kupanda jukwaani kusema maneno wanayotaka halafu wanatawanyika.
Kwa maana hiyo.........wameshashindwa tayari.......
Hivi Jamani......hivi kweli CDM wanategemea mahudhurio yale ya mikutano ya hadhara ndio itawepeleka Ikulu kweli!!??......hivi CDM wameshashiriki chaguzi ngapi...ili ijifunze/kutambua kuwa wanatakiwa kufanya zaidi ya mikutano ya hadhara.......!!!.....kwa upande mwingine wale wachache waliohudhuria mkutano wa Lissu ndio wanaweza kuwa for Real.....
.............Kwa mtazamo wangu Chadema haipati idadi ya kura inayoendana na umaarufu wake kwasababu huwa haisimamishi wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kwenye jamii. .......
Hivi unaongea nini wewe? Unasema watu wanaokuja mikutanoni siyo wapiga kura halafu unaishauri Chadema iwafuate wapiga kura majumbani. Ina maana hao watu wanaokuja mikutanoni wanatokea mapangoni?
Kwa mtazamo wangu Chadema haipati idadi ya kura inayoendana na umaarufu wake kwasababu huwa haisimamishi wagombea wenye mvuto na wanaokubalika kwenye jamii. Chaguzi nyingi za chini zimekuwa zikigombewa na watu bora liende tu. Kinyume chake CCM wamekuwa wakizipa uzito mkubwa na kuweka watu ambao wanakubalika na kukusanya idadi ya kura inayozihitaji.
ZeMarcopoloNadhani chadema wameamua kuwa kwa sasa focus yao siyo kusinda uchaguzi ila ni kupata umaarufu ili jina lao lizoeleke masikioni mwa watanzania na kuvipiku vyama vingine vya upinzani. Baada ya hatua hiyo kuota mizizi then wataanza kupanga mikakati ya kuingia ikulu.
Hata hivyo kwa jinsi siasa zilivyo, katika harakati za kutafuta umaarufu wanaweza "kuokota" urais kama dodo chini ya mnazi.
Kila siku hakuna wanachozungumza zaidi ya ufisadi kwanini watu wasiwachoke.Wabadilishe maneno kwenye mikutano yao basi
Hoja yako ya chama kutosimamisha wagombea bora naikubali. Lakini kwa upande mwingine hujaelewa ninachoongelea kwamba ukipiga baragumu kuita watu mkusanyiko wa ghafla watakaoitikia mara moja ni wale wasio na kazi maalum na pengine wasio na kazi. Walio makazini itawawia vigumu kwani itabidi wapate ruhusu kwa mwajiri na sababu ziwe nzito na hao waaajiriwa ndio walio wengi wapiga kura. Waliojiajiri hali kadhalika wataangalia mambo mengi umuhimu wa kwenda mkutanoni au kuendesha shughuli yake inayomfanya aishi.
Kwa vyo vyote kuna kitu ambacho kinatakiwa kibadilike kwa kubuni mbinu bora zaidi za kupata wapiga kura. Kama sera zao zinaeleweka na wananchi wameshawasikia sana tu. Je, kwa mikutano hiyo kwa umati huo uliozoeleka unasaidia kuongeza kura kwenye ballot box au ni wahudhuriaji tu?
Unajijachanganya sana mkuu unaposema watu wanaokuja mikutanoni ni watu wasio na kazi na wasio na makazi. Kama unahisi kuwa idadi kubwa ya wapiga kura ni watu wenye kazi na makazi basi utakuwa unajidanganya sana. Kwa taarifa yako ni asilimia mbili ya hao watumishi wako unaowathamini na kuwalenga ndiyo huwa wanaojitokezaga kupiga kura siku ya uchaguzi.
Sababu za Chadema kutoshinda chaguzi kama inavyotarajiwa inaenda zaidi ya kutopata idadi ya kura za kutosha. Pamoja na kutosimamisha wagombea wanaokubalika, kuna tatizo la nchi kiujumla la watu kutojitokeza siku ya uchaguzi. Hili sidhani kama lipo ndani ya uwezo wa Chadema kusuluhisha, kwasababu linahitaji elimu zaidi itolewe kwa watu kuelewa umuhimu wa kupiga kura kwenye maisha yao.
Chadema wanaweza kugonga hodi kila nyumba, lakini kama watu hawajaona uhusiano kati ya kupiga kura na mabadiliko yao hakuna kitakachotokea.