CHADEMA (Odinga) vs CCM (Uhuru) siasa za nje!

Hongereni mulioshinda tunawatakia utawala mwema.
 
Magamba bwana..msijali Uhuru atawachotea ela ya kampeni ila tambueni kuwa kura sio fedha
 


Naona hapo unapiga rangi upepo. Viongozi Gani walioenda kupiga kampeni kenya? Acheni siasa na hoja za kwenye kahawa. Leteni hoja za msingi na si hoja za kishabiki kama ushabiki wa mpira.
Tuhoji CCM wamefanya nini na Tuzungumze Chadema watafanya nini na si kuzungumzia watu ambao tayari wana barabara za juu na chini sisi bado tunapembua kiuwakinifu na tunakaribia kwenye mchakato na serikali iko mdahaloni.
Hapo unasemea watu wenye sekondari zinazoitwa sekondari zaidi ya 4000 sisi na CCM yetu tuna majengo yanayoitwa sekondari chini ya 1000. Tusiwe kama mbayuwayu tutafakari na kuchanganua wewe na mimi tunakwenda wapi na kizazi kijacho tunakiachia nini?

 
Hivi haya kweli yametokea maana nimesikia ati CDM walituma Ujumbe Kenya kumuunga mkono Odinga!... sijui wanaweza utuambia ni kwa sababu gani? je kuna mahusiano ya kimrengo au basi tu..

katika makosa makubwa na yaloushangaza ulimwengu kisiasa ambayo yamewahi kutokea ni pamoja na uchaguzi huu wa Kenya 2013, ambapo watuhumiwa wakubwa wa UKABILA (UHURU na ODINGA) wamekuwa ndio wagombea wakubwa na nawahakikishia kabisa ya kwamba uchaguzi wote wa Kenya umefanyika kwa kufuata UKABILA..watakana na kujivuta vumbi za uso lakini ukweli unabakia kwamba kabila ndicho kigezo kikubwa cha uchaguzi huo...Yale makabila mengine yamemchagua UHURU ama ODINGA kwa kuchuja bora Zimwi likujualo kuliko..
Mtakuja nambia...
 
Mambo ya Kenya waachiwe wakenya baada ya matokeo. Tuna mengi yanatusibu hapa Bongo petu! Tusipoteze muda na ya Kenya sasa. Hata kama tulikuwa tunaunga mkono mtu fulani, Wakenya wameamua na tunaheshimu uamuzi wao!
 

Umenifurahisha hhrhheh haya ngoja tusubiri
 
Upuuzi mtupu badala ya vyama hivi kujishughulisha na matatizo ya wananchi wake inakwenda tumia fedha kwa vitu visivyowahusu..Hii ni sawa na kutumia fedha ktk harusi ya jirani wakati watoto wako hawana ada ya shule...
 


Mpaka sasa sijaona ushahidi wowote unaoonyesha CDM walipeleka timu kumuunga mkono Odinga. Kwa nini tusitajiwe majina? Kila mtu anafahamu kuwa Mh. John Pombe Magufuri alikwenda kumuona mkono Odinga. Katibu wa chama ilisemekana alikuwa Nairobi kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
 

nnawasiwasi ile twite ya ccm wewe ndiyo uliandika
 
jamani si lazima wote tuanzishe thread,wengine ni vema tukabaki wachangiaji tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…