CHADEMA ni WikiLeaks ya TZ zaidi kuliko chama cha siasa?

Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
GREAT THINKERS
Hebu wana jukwaa sasa tujadili sera za hivi vyama vya upinzani kwa umakini ili tuweze kujua kama vina uwezo wa kutuletea mabadiliko tunayoyataka.

Hapa tutajadiliana sera za chama kikuu cha upinzani CHADEMA muda ukiruhusu tunaweza kulinganisha na vyama vingine vya upinzani hasa CUF ambacho ni cha pili in rankings.

CHADEMA imejikita zaidi katika kufichua ufisadi ndani ya serikali kwakuwa inaamini kuwa hili ndilo tatizo la msingi. Hili lilithibitishwa na ilani ya uchaguzi ya chama ya 2010 – 2015. Nakubaliana na hilo kwamba ufisadi unaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa hivyo kustahili kupigwa vita kama sera ya CDM inavyotaka.

Hata hivyo ukisoma ilani ya uchaguzi ya CDM, inaonekana iko too ‘generic' na kisiasa zaidi na imeshindwa kuonesha wapi mtanzania alipo na itampeleka wapi.

Ilani ya uchaguzi ya CDM haioneshi quantitatively ni kwa jinsi gani itashughulikia maswala ya kiuchumi mfano:
1) Mfumuko wa bei Tanzania
2) Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mtizamo wa CDM inataka kiweje?
3) Kuporomoka kwa thamani ya shilingi
4) Mgawanyo wa budget kwa sekta mbalimbali e.g Kilimo na elimu uweje
5) Makadirio ya mapato na matumizi ya kuendesha nchi kama ingeweza/ itapewa ridhaa ya kuongoza nchi.

Assumption niliyokuwa nayo hadi sasa ni kuwa CDM ni kama WikiLeaks ambayo kazi yake kubwa ni kufichua ufisadi. Lakini bado si chama cha Siasa ambacho kinaweza kupewa nchi kwa misingi y a kisera zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa, kijamii na kiuchumi Tanzania.

Hivi ni kweli kwamba viongozi wa CDM walikurupuka tu kutaka uongozi bila kujiandaa? Au walikuwa na ilani nyingine ambayo haikupelekwa kwa wapiga kura? Ukosefu wa elimu ulichangia kwa namna yoyote kuwa na ilani kama hii?

Nielimisheni na wengine wanaotaka kujua pia, mnavutika na sera zipi za CDM kiuchumi ili tushawishike kuipigia kura badala ya CUF, TLP au NCCR?

Je ukosefu wa upembuzi yakinifu kwenye maswala ya msingi kama haya inathibitisha kwamba CDM bado haijawa tayari kushika hatamu za uongozi wa Tanzania?

Au unaweza ulisababishwa na ukosefu wa elimu wa viongozi wa CDM?

Note: Viongozi wakuu wa CDM wanaweza kuchangia na kuturekebisha pale ambapo tumekosea. Mnaweza kujifunza pia kama kuna lolote jipya katika haya.

Reference: Ilani ya uchaguzi ya CDM 2010 - 2015 imeambatanishwa hapo chini.Hii ni suppliment kwa wale wasioelewa zaid:

Watu wakisema Tanzania haina vyama mbadala vya Kisiasa, wengine wanapiga kelele kwa sababu fikra zao zimejazwa mapenzi na ushabiki wa kisiasa Kutokana na kuichoka CCM na hii imewafanya wasiushughulishe tena ubongo wao katika quantitative thinking.

Ninakubaliana na wewe, ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2010 ilikuwa na mapungufu mengi tu kwa mtu anayetumia macho mawili kusoma na kutafakali, pia ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka hivi huku ikilenga kundi moja tu wananchi kana kwamba nchi inajengwa na kundi hilo moja.

Hata bajeti mbadala ya mwaka wa fedha 2012/2013 nayo ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka na hata uchapaji nao ulifanywa haraka haraka mpaka kurasa zingine zikawa zimesahauliwa kuwekwa kitu ambacho ni makosa hasa unapotaka kuileza nchi na dunia kama "NIKO TAYARI".

Ukisoma DIBAJI YA ILANI YA UCHAGUZI utaona kuwa CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi mkuu na ajenda moja tu ambayo ni UFISADI. kitu ambacho ilikuwa ni makosa katika siasa kwa sababu wananchi walitegemea chama kiwe na macho yanayoona mbele beyond UFISADI. Kwa kuonyesha kama ni ajenda ilikuwa ni moja, ilani ya uchaguzi ilibainisha mambo matatu yanayosababisha nchi iwe maskini, ikayataja kuwa ni UFISADI, UFISADI, UFISADI. Rushwa na umaskini viliwekwa kama "sub-category" ya ufisadi wakati ambapo rushwa inaweza isiwe sababu ya ufisadi kama chama kilivyoainisha maana ya neno UFISADI katika ilani yake ya uchaguzi.

CHADEMA walitaka kuwaambia wananchi kuwa, hakuna changamoto zingine zilizo mbele yao zaidi ya UFISADI na kama wananchi wakiukataa ufisadi, kila kitu kitapatikana.

Kibaya zaidi, hawakutaka kujua kama uchaguzi ni endelevu pale walipopigilia msumari kwenye ilani ya uchaguzi na kusema, "Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015". Hawakutaka kufungua mlango kwa chaguzi zingine kuu zijazo kana kwamba huo ndiyo ulikuwa uchaguzi wa kufa na kupona. Sijui 2015 watalifunguaje tena hili jeneza la kisiasa.

Ni kitu cha kushangaza unapoona CCM jinsi inavyoendesha na kuchezea nchi na wananchi wake, na ishara zote zinaonyesha kama imechoka kutawala, lakini hakuna chama ambacho kinaitumia nafasi hii kuionyesha jamii kama kiko tayari kupewa madaraka badala ya kucheza mchezo ule ule ambao CCM wanaucheza huku CCM wakionekana kama ndiyo "disc jokey". 'Ng'wamapalala'
 
Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,974
Vp ndio unaamka au? Njoo upate gahawa hapa kabla ya kuendeleza majungu yako hayo hapa.
 
HUGO CHAVES

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
2,045
540
unaposema cdm ni wikileaks lazima uangalie nini maana ya wikileaks na nini maana ya cdm .hapa una kutana na vitu viwili tofauti na vyenye malengo tofauti .sijui umefikiria nini kulinganisha cdm na wikileaks pengine kuna nadharia iliyokusukuma kuandika ukizingatia ccm imekuwa ikifanya mambo yake kwa siri siri kwa hiyo sasa hivi hawawezi kwa kuwa siri zinavuja .sikuungi mkono kwa hoja yako kulinganisha cdm na wikileaks
 
Maundumula

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
7,503
2,938
Chadema ni jumuiya ya wapiga filimbi Tanzania ambayo ina watonyaji au wanyetishaji sehemu mbalimbali.:becky:
 
Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Vp ndio unaamka au? Njoo upate gahawa hapa kabla ya kuendeleza majungu yako hayo hapa.

Kama hapo tayari umeshaona majungu, basi hili jukwaa huenda ikawa si saizi yako. Nenda kwenye kamusi kwanza utafute tafsiri ya maneno magumu kama: mfumuko wa bei na thamani ya shilingi. Bila hivyo hapo utaona nyota tu na pengine hujui tunazungumzia kitu gani. Wewe unaona tu CDM, CUF, TLP na NCCR! Sio kila mtu anaweza kuchangia uzi huu, lazima kidogo uwe na akili ya kuzaliwa.
 
Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
Huijui chadema, tena huijui kabisa, ila umeandika kwa kufikirika tu na kufikirika huko ni kule kwa kiwango cha chini kabisa!

Ilani ya Chadema ya mwaka 2010-2015 ipo wazi ila wewe hujajikita kuichambua bali umekurupuka tu toka usingizini,

Nakushauri tumia mda mwingi kusoma ilani za vyama kisha njoo tukufunde kisiasa zaidi usije kuingingia kwenye mkondo wa wapiga kelele wa Lumumba.
 
Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Huijui chadema, tena huijui kabisa, ila umeandika kwa kufikirika tu na kufikirika huko ni kule kwa kiwango cha chini kabisa!
.

Inawezekana siijui CDM vizuri ila ilani si nimeiambatanisha hapo. Unaweza kuniambia page ya ngapi inazungumzia mfumuko wa bei na utashughulikiwaje? Thamani ya shilingi itashughulikiwaje? Ila unaonekana sasa wewe ndio mpiga kelele sijui wa wapi?
 
kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
492
huijui chadema, tena huijui kabisa, ila umeandika kwa kufikirika tu na kufikirika huko ni kule kwa kiwango cha chini kabisa!

Ilani ya chadema ya mwaka 2010-2015 ipo wazi ila wewe hujajikita kuichambua bali umekurupuka tu toka usingizini,

nakushauri tumia mda mwingi kusoma ilani za vyama kisha njoo tukufunde kisiasa zaidi usije kuingingia kwenye mkondo wa wapiga kelele wa lumumba.
Yericko huyu bayana ni kama vile mlevi wa ngwasuma-gongo unazungumzia ilani ya uchaguzi ya chadema ya 2010?. Ndio maana nasema nchi bado inawajinga wengi ingawa mwalimu alijenga shule nying za msingi.na muhimu kwako kubali uombewe la sivyo umekwisha aribikiwa.
 
Last edited by a moderator:

Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Yericko huyu bayana ni kama vile mlevi wa ngwasuma-gongo unazungumzia ilani ya uchaguzi ya chadema ya 2010?. Ndio maana nasema nchi bado inawajinga wengi ingawa mwalimu alijenga shule nying za msingi.na muhimu kwako kubali uombewe la sivyo umekwisha aribikiwa.
Sasa hiyo si ndio dira ya chama chako? Au unatwambia kwamba miaka miwili tu baada ya kuipendekeza haifai tena? Wasi wasi wangu mkubwa ni kwamba hamjawahi kuisoma wengine, ndio maana majibu yenu yanakuwa mepesi; Huijui CDM, unatoka kuamka, kaisome tena!!! Hakuna hata mmoja anayeiunga mkono kwa hoja. Tetee sera za chama chenu sio mnawababaisha wananchi wasiojua kusoma na kuandika.
 
sinshoo

Member
Oct 13, 2012
50
14
Unapokuwa na mfumuko wa bei pia thamani ya shilingi lazima ishuke ni kitu kimoja au viwili vinavyoenda sambamba na kuinua hali ya uchumi ni kuongeza Uzalishaji wa viwandani na kilimo na kubana matumizi CDM walishasema watapunguza matumizi ya Serikali kwa kuwa na Serikali yenye mawaziri wachache na kuondoa wakuu wa wilaya na mikoa kote uko ni kuongeza ukuwaji wa uchumi kwa kubana matumizi na kuongeza TIJA ina bidi utulie kusoma ilani ya uchaguzi na Ahadi ya viongozi then unalinganisha, Mikakati MENGINE ni policymaker wanafanya baada ya dondoo ya ktk Ilani,

Maswali yako ni mepesi na hayana Tija kwa wakati uliopo maana unaturudisha kujadili kitu ambacho kishajadiliwa 2010 na sasa CCM wanatekeleza sera za chadema elimu bure inawezekana na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi
 
Mimibaba

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
4,558
1,285
Note: Viongozi wakuu wa CDM wanaweza kuchangia na kuturekebisha pale ambapo tumekosea. Mnaweza kujifunza pia kama kuna lolote jipya katika haya.

Uharo unatokana na ugonjwa
attachment.php
 
chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,941
899
Msiojua Misingi ya nchi, kwa nini sisi ni masikini ,mtaendelea kufanya haya. Sera ya chadema imejikita kujenga nchi ya kizalendo na kuondokana na umasikini maana chanzo kimeishabainishwa
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,478
Watu wakisema Tanzania haina vyama mbadala vya Kisiasa, wengine wanapiga kelele kwa sababu fikra zao zimejazwa mapenzi na ushabiki wa kisiasa Kutokana na kuichoka CCM na hii imewafanya wasiushughulishe tena ubongo wao katika quantitative thinking.

Ninakubaliana na wewe, ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2010 ilikuwa na mapungufu mengi tu kwa mtu anayetumia macho mawili kusoma na kutafakali, pia ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka hivi huku ikilenga kundi moja tu wananchi kana kwamba nchi inajengwa na kundi hilo moja.

Hata bajeti mbadala ya mwaka wa fedha 2012/2013 nayo ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka na hata uchapaji nao ulifanywa haraka haraka mpaka kurasa zingine zikawa zimesahauliwa kuwekwa kitu ambacho ni makosa hasa unapotaka kuileza nchi na dunia kama "NIKO TAYARI".

Ukisoma DIBAJI YA ILANI YA UCHAGUZI utaona kuwa CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi mkuu na ajenda moja tu ambayo ni UFISADI. kitu ambacho ilikuwa ni makosa katika siasa kwa sababu wananchi walitegemea chama kiwe na macho yanayoona mbele beyond UFISADI. Kwa kuonyesha kama ni ajenda ilikuwa ni moja, ilani ya uchaguzi ilibainisha mambo matatu yanayosababisha nchi iwe maskini, ikayataja kuwa ni UFISADI, UFISADI, UFISADI. Rushwa na umaskini viliwekwa kama "sub-category" ya ufisadi wakati ambapo rushwa inaweza isiwe sababu ya ufisadi kama chama kilivyoainisha maana ya neno UFISADI katika ilani yake ya uchaguzi.

CHADEMA walitaka kuwaambia wananchi kuwa, hakuna changamoto zingine zilizo mbele yao zaidi ya UFISADI na kama wananchi wakiukataa ufisadi, kila kitu kitapatikana.

Kibaya zaidi, hawakutaka kujua kama uchaguzi ni endelevu pale walipopigilia msumari kwenye ilani ya uchaguzi na kusema, "Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015". Hawakutaka kufungua mlango kwa chaguzi zingine kuu zijazo kana kwamba huo ndiyo ulikuwa uchaguzi wa kufa na kupona. Sijui 2015 watalifunguaje tena hili jeneza la kisiasa.

Ni kitu cha kushangaza unapoona CCM jinsi inavyoendesha na kuchezea nchi na wananchi wake, na ishara zote zinaonyesha kama imechoka kutawala, lakini hakuna chama ambacho kinaitumia nafasi hii kuionyesha jamii kama kiko tayari kupewa madaraka badala ya kucheza mchezo ule ule ambao CCM wanaucheza huku CCM wakionekana kama ndiyo "disc jokey".
 
Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Watu wakisema Tanzania haina vyama mbadala vya Kisiasa, wengine wanapiga kelele kwa sababu fikra zao zimejazwa mapenzi na ushabiki wa kisiasa Kutokana na kuichoka CCM na hii imewafanya wasiushughulishe tena ubongo wao katika quantitative thinking.
.

Tatizo la CHADEMA ni kurejea makosa yale yale ambayo yameipeleka CCM na nchi yetu kufika hapa tulipo. Yaani dhana ya 'know it all' na tabia ya kujiona viungu vido vidogo ambavyo viko perfect. Hii si kweli. Critical thinking ni muhimu ili kufikia ufanisi. La sivyo itafikia kipindi CDM nayo itakuwa kama CCM; Ukisema CDM hakina dira, utaitwa makao makuu na kukolimbwa!
 
Bayana

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
433
69
Kwa hiyo kwa mawazo yako unataka kutuaminisha CDM nini kuhusiana na mada yako!

CHADEMA should have clear plans na ichanganue impact ya maamuzi mbalimbali ambayo inakusudia kuyachukua.

Watu wenye busara wanasema; 'hatupangi kushindwa ila tuna shindwa kupanga'.
 
Benaire

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
1,956
301
Haya ndio maneno ya watanzania waliochagua kutakufanya tafiti na kubuni tafiti wakitumia maneno ya kiingereza kama "quantitative thinking"......nadhani ungeanza kwa kuelewa nini maana ya kampeni na kuangalia kama ajenda kuu ilikuwa ni ufisadi....na kwa suala la bajeti,usiishie kusoma makosa kwani hata maprofesa hukosea katika machapisho bali ukisikiliza speech utaelewa vizuri (by zitto kabwe).
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom