GREAT THINKERS
Hebu wana jukwaa sasa tujadili sera za hivi vyama vya upinzani kwa umakini ili tuweze kujua kama vina uwezo wa kutuletea mabadiliko tunayoyataka.
Hapa tutajadiliana sera za chama kikuu cha upinzani CHADEMA muda ukiruhusu tunaweza kulinganisha na vyama vingine vya upinzani hasa CUF ambacho ni cha pili in rankings.
CHADEMA imejikita zaidi katika kufichua ufisadi ndani ya serikali kwakuwa inaamini kuwa hili ndilo tatizo la msingi. Hili lilithibitishwa na ilani ya uchaguzi ya chama ya 2010 – 2015. Nakubaliana na hilo kwamba ufisadi unaligharimu taifa kwa kiasi kikubwa hivyo kustahili kupigwa vita kama sera ya CDM inavyotaka.
Hata hivyo ukisoma ilani ya uchaguzi ya CDM, inaonekana iko too ‘generic' na kisiasa zaidi na imeshindwa kuonesha wapi mtanzania alipo na itampeleka wapi.
Ilani ya uchaguzi ya CDM haioneshi quantitatively ni kwa jinsi gani itashughulikia maswala ya kiuchumi mfano:
1) Mfumuko wa bei Tanzania
2) Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mtizamo wa CDM inataka kiweje?
3) Kuporomoka kwa thamani ya shilingi
4) Mgawanyo wa budget kwa sekta mbalimbali e.g Kilimo na elimu uweje
5) Makadirio ya mapato na matumizi ya kuendesha nchi kama ingeweza/ itapewa ridhaa ya kuongoza nchi.
Assumption niliyokuwa nayo hadi sasa ni kuwa CDM ni kama WikiLeaks ambayo kazi yake kubwa ni kufichua ufisadi. Lakini bado si chama cha Siasa ambacho kinaweza kupewa nchi kwa misingi y a kisera zinazoweza kuleta mabadiliko ya kweli ya kisiasa, kijamii na kiuchumi Tanzania.
Hivi ni kweli kwamba viongozi wa CDM walikurupuka tu kutaka uongozi bila kujiandaa? Au walikuwa na ilani nyingine ambayo haikupelekwa kwa wapiga kura? Ukosefu wa elimu ulichangia kwa namna yoyote kuwa na ilani kama hii?
Nielimisheni na wengine wanaotaka kujua pia, mnavutika na sera zipi za CDM kiuchumi ili tushawishike kuipigia kura badala ya CUF, TLP au NCCR?
Je ukosefu wa upembuzi yakinifu kwenye maswala ya msingi kama haya inathibitisha kwamba CDM bado haijawa tayari kushika hatamu za uongozi wa Tanzania?
Au unaweza ulisababishwa na ukosefu wa elimu wa viongozi wa CDM?
Note: Viongozi wakuu wa CDM wanaweza kuchangia na kuturekebisha pale ambapo tumekosea. Mnaweza kujifunza pia kama kuna lolote jipya katika haya.
Reference: Ilani ya uchaguzi ya CDM 2010 - 2015 imeambatanishwa hapo chini.
Hii ni suppliment kwa wale wasioelewa zaid:
Watu wakisema Tanzania haina vyama mbadala vya Kisiasa, wengine wanapiga kelele kwa sababu fikra zao zimejazwa mapenzi na ushabiki wa kisiasa Kutokana na kuichoka CCM na hii imewafanya wasiushughulishe tena ubongo wao katika quantitative thinking.
Ninakubaliana na wewe, ilani ya uchaguzi ya CHADEMA ya mwaka 2010 ilikuwa na mapungufu mengi tu kwa mtu anayetumia macho mawili kusoma na kutafakali, pia ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka hivi huku ikilenga kundi moja tu wananchi kana kwamba nchi inajengwa na kundi hilo moja.
Hata bajeti mbadala ya mwaka wa fedha 2012/2013 nayo ilikuwa kama imeandikwa kwa haraka haraka na hata uchapaji nao ulifanywa haraka haraka mpaka kurasa zingine zikawa zimesahauliwa kuwekwa kitu ambacho ni makosa hasa unapotaka kuileza nchi na dunia kama "NIKO TAYARI".
Ukisoma DIBAJI YA ILANI YA UCHAGUZI utaona kuwa CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi mkuu na ajenda moja tu ambayo ni UFISADI. kitu ambacho ilikuwa ni makosa katika siasa kwa sababu wananchi walitegemea chama kiwe na macho yanayoona mbele beyond UFISADI. Kwa kuonyesha kama ni ajenda ilikuwa ni moja, ilani ya uchaguzi ilibainisha mambo matatu yanayosababisha nchi iwe maskini, ikayataja kuwa ni UFISADI, UFISADI, UFISADI. Rushwa na umaskini viliwekwa kama "sub-category" ya ufisadi wakati ambapo rushwa inaweza isiwe sababu ya ufisadi kama chama kilivyoainisha maana ya neno UFISADI katika ilani yake ya uchaguzi.
CHADEMA walitaka kuwaambia wananchi kuwa, hakuna changamoto zingine zilizo mbele yao zaidi ya UFISADI na kama wananchi wakiukataa ufisadi, kila kitu kitapatikana.
Kibaya zaidi, hawakutaka kujua kama uchaguzi ni endelevu pale walipopigilia msumari kwenye ilani ya uchaguzi na kusema, "Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015". Hawakutaka kufungua mlango kwa chaguzi zingine kuu zijazo kana kwamba huo ndiyo ulikuwa uchaguzi wa kufa na kupona. Sijui 2015 watalifunguaje tena hili jeneza la kisiasa.
Ni kitu cha kushangaza unapoona CCM jinsi inavyoendesha na kuchezea nchi na wananchi wake, na ishara zote zinaonyesha kama imechoka kutawala, lakini hakuna chama ambacho kinaitumia nafasi hii kuionyesha jamii kama kiko tayari kupewa madaraka badala ya kucheza mchezo ule ule ambao CCM wanaucheza huku CCM wakionekana kama ndiyo "disc jokey". 'Ng'wamapalala'