CHADEMA ni "professional"

tuko kwenye tatu ya marehemu chagadema, tunasubiri kuanua tanga
Waliojiandikisha ku pita Ukraine in 70,000,walloping a Jura 20,000.kura 50,000 zimenunuliwa na ccm sass mnashangilia mini Kama sio ujuha wenu 2015 kitaeleweka.
 
Ni aibu kijana kuwa hivyo.. Labda kama ni mzee..lkn km kijana ujipange uwe na uwezo wa kujenga hoja

Wewe nimekuuliza hoja gani hujibu ulifikiri mi mnuka shiki wa kukimbia kwetu na kurukia maisha ya kuitwa Nyani? Nipotezee tafadhali nusijeharibu thread ya watu
 
Kwa hili mimi najivinia kuwa mwanachadema kiukweli
 
ES

Kwa hiyo kila mwananchi anayetaka kurejeshwa kwa Tanganyika amekosa kura Zanzibar! What a simple inference Mkuu!

Vijana wa CCM ni waropokaji,Hawana hata hoja.Sasa huyu ES ni wale wale tu.Kwa taarifa yake,wanaotaka hasa kurudi kwa Tanganyika ni Wazanzibari-tena CUF ambao wanaidhibiti Pemba. chana na watu wenye ufinyu wa kufikiri kama huyo
 

Walimpinga kabla ya kufanya kazi lakini wameona kazi yake imefanyika kwa uadilifu na ndiyo maana wamempongeza.Lakini wale waliomuamini toka mwanzo leo wanamtolea macho ndicho kitu cha kujiuliza kulikoni?
 
Yaani wabongo kwa unafiki huyu jamaa kuna post amejidai hana chama lakini post zake ni kusifia chadema tu! watanzania wa kusifia sifia unajua wametucost sana (unafiki mbaya) hili bandiko lako kama hujui historia vile na mgeni wa JF. Wenzie walikuwa wanawaita wake wenza/ wameolewa na viongozi wako waliwatupilia mbali katika serikali kivuli sema wamesoma alama za nyakati na hakukuwa na option nyingine. Viongozi wa Chadema hawako tayari kuungana na ukawa imekaa kichuga chuga.

 

we shida yako nini?kwamba mimi sina timu,lakini eti ni dhambi kuipongeza timu shindi
 

Hakuna mfumo wa serikali ambao uko perfect 100%, hata huo wa serikali 3 utaibuka na changamoto zake,sasa itakapofikia hapo mtasema suluhisho lake ni serikali 4? kimsingi changamoto nyingi za muungano ni za kikatiba na hii ni nafasi nzuri ya kuzirekebisha bila kuuvunja muunganlo huo.

Muungano wa serikali 3 utaondoa kabisa utaifa , ni nani atakayekuwa na uchungu na hii serikali ya 3? ambayo kimsingi ni ya kiutawala tu , haina mahusiano ya moja kwa moja na wananchi,hivi katika umasikni na shida zote zinazowakabili wananchi wanyonge hivi sasa dawa yake ni kuwa na serikali 3? mimi bado nina imani na mfumo wa sserikali 2 na kama tumefikia hatua ya kubadili mfumo wetu wa kiutawala kwa nia ya kuwaletea wananchi wetu maendeleo basi jawabu ni serikali moja .
 

Mimi si mnafiki.Labda wewe mwenzangu.Narudia tena,mimi sina chama chochote cha siasa nchini Tanzania na kwingineko.Kumbuka uanachama ni kadi. Nasimamia ukweli daima.Kwa wanaonijua wanaweza kushuhudia hapa. Kama kuongea ukweli ni unafiki,somo la kidini na kiraia halikukuingia vyema.
 
Kumbe gamba sugu.. Ndo maana huwezi jenga hoja.. Ndo maana diaspora walikua wanapoteza muda wao kukufafanulia mambo madogo..ccm inaabishwa na ninyi ambao hamwezi kujenga hoja.. Ni kutukana tukana tu na kutoa mipasho..

wabeba box mna hali ngumu sana kiuchumi
 

chadema watanzania wameichoka .. ACT NDIO HABARI YA MUJINI
 
Walimpinga kabla ya kufanya kazi lakini wameona kazi yake imefanyika kwa uadilifu na ndiyo maana wamempongeza.Lakini wale waliomuamini toka mwanzo leo wanamtolea macho ndicho kitu cha kujiuliza kulikoni?

Mantiki gani iliyowaongoza kumpinga kabla ya kuona kazi yake ? ndio maana nikasema CDM wanafanya mchezo wa kuigiza ama wanataka kuhalalisha jina walinalo la wapinzani wakidhani kwamba kila jambo linalofanywa na CCM basi lazima lipingwe.ukitazama kwa umakini utagundua upinzani umempa support Warioba kwa sababu tu maoni yake yamekwenda kinyume na mtazamo wa CCM , laiti kama Warioba angetoa mapendekezo ya serikali 2 kama CCM wanavyotaka hakika leo hii sifa ya usomi na umakini wa Jaji warioba ungekuwa kituko kwa CDM.

Kimsingi nakubaliana na ukweli kwamba mazingira yamebadilika sana tangu muungano wetu uasisiwe, na hili ni jambo la kawaida,waasisi wa muungano wetu walikuwa sahihi kwa wakati wao kufanya yale waliyoona yanafaa kwa wakati wao, ni wajibu wetu sisi tuliopo sasa kuchukua hatua ya kuboresha mapungufu ya waasisi wetu wa muungano huu.kufikilia kwamba kuirudisha Tanganyika ndio kuuboresha muungano huu kwa maoni yangu sioni kma ni sawa, kwa sababu kuirejesha Tanganyika pia kutakaribisha changamoto zingine ambazo wakati tukiwa Tanzania bara hazikuwepo mf,sasa hivi tunasema sisi ni watanganyika kwa sababu tupo ndani ya muungano ndio maana tunataka au tunajitambulisha kama Tanganyika, lakini nje ya muungano sio watanganyika tu, bali kutakuwa na wabara na wapwani,mikoa iliyopiga hatua kimaendeleo na iliyonyuma, wasukuma , wachaga makabila makubwa na madogo.

Tanganyika itaibua tena utambulisho wa uchifu, umwinyi, lakini pia itarudisha nyuma harakati za kiuchumi za kikanda maana lazima mchakato mzima wa mashirikiano ya kiuchumi na mataifa mengine itasimama.

wakati tunajifunza kutoka katika mataifa mengine juu ya miundo na mifumo mbalimbali ya kiutawala, ni vyema pia tukajifunza yale mabaya yaliyokuta wengine, mf SUDAN kabla ya kujitoa kwa Sudan ya kusini walikuwa wamoja, ikaibuka hoja ya wakusini na kaskazini, matokeo yake Sudan ya kusini ikajitenga kutoka Sudan kaskazini wakati huo wanapambana na Sudan wajiita wao wasudan weusi wakusini wanaopigania maslahi ya weusi.

Kupitia azimio la umoja wa mataifa Sudan kusini ikawa nchi kamili miaka 3 iliyopita, sasa wale waliokuwa wanasema walikuwa wamoja kama Sudan ya kusini sio wamoja tena, kila mmoja ni shahidi kwa yale yanayotokea,tutakuwa ni watu wa ajabu tukidhani kwamba sisi ni watu wa pekee hatuwezi kupatwa na masaibu yanayowapata wengine kwa makosa yaleyale waliyowafanya wenzetu, ebu tujiulize ndugu zangu tunajifunza nini katika hilo?
 
Tatizo la chadema mnapenda sifa ili mjiongezee umaarufu mbona waisifia chadema pekee hali ukijua hoja hii na wapinzani wote hongereni nccr cuf na cdm
 
wabeba box mna hali ngumu sana kiuchumi

chadema watanzania wameichoka .. ACT NDIO HABARI YA MUJINI

Kaka huwa unazielewa kweli topic za humu?,maana huwa sioni cha maana unachochangia zaidi ya ACT chama "makini,braa,braa".hao kina ACT walikupa maneno ya kuandika na kukukataza mengine ya "kitimamu zaidi"?
 
Hivi umesahau kuwa hivyo vyama mnavyo jiunga navyo mlisema viliolewa na ccm?
 

Wajua kaka yangu tatizo walilonalo wawakilishi wa Muungano wa serikali mbili wamegubikwa na uwoga wa kutotaka kuzungumza na kuargue.Hakika hakuna kitu kizuri kama maelewano,lakini kwa kulazimisha hatufiki kokote,mwisho wa sikuwajiuliza hivi hwa kwa nini wanatulazimisha?Na hapo ni moja muungano utavunjika kwa vurugu,mauaji ambapo haya yote yangeweza kuepukika.

Hebu jiulize kwa nini tusikubaliane katika kutokubaliana?Watoa hoja wachache na wengi wakubaliane kwenye hoja za msingi.Tatizo litatuliwe kwa hoja?Hivi katika hiyo Katiba hata UWAJIBIKAJI,UADILIFU na UWAZI nao ni unafiki wa Tume ya Warioba kuyaweka?Hivi kwenye hiyo Katiba hakuna mzuri ya kuyafikiria zaidi ya Muungano wa serikali mbili.tatu,moja nne nk.

Mwisho woga wa CDM ulikuwa valid sababu wateuliwa wengi wa Rais hawatendi haki na uajibikaji ipasavyo.Waangali Wenyeviti wa Tume ya Uchaguzi,ya Vyama vya siasa nk,hawatendi haki kwa vyama vya upinzani ndiyo maana wakawa na uwoga huo.Wanasema mtu akiumwa na nyoka basi hata unyasi ukimgusa lazima apige mayowe na kutoa mbio,sawa ndugu.

Tushindane kwa hoja tupate Katiba ya watanzania na siyo Katiba ya CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…