TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,559
Nimefanya uchunguzi Mdogo sana juu ya chama gani cha siasa chenye mawazo mazuri sana ya kuitoa nchi yetu ya Tanzania kutoka kwenye hali duni ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na Kuwa nchi ya ahadi,nikagundua kwamba CHADEMA ndio chama chenye mawazo bora kabisa kwa sasa.
Hiki chama kimeniingia sana moyoni na siku zote huwa natamani kichukue madaraka ya kuongoza nchi lakini navunjwa moyo na uongozi wa taifa wa chama hiki chini ya mwenyekiti wake Mheshimiwa Mbowe.Kwa kifupi Mheshimiwa Mbowe amefanya Kazi nzuri sana ya kudhohofisha harakati za Upinzani kuing'oa CCM madarakani,Sina maana kwamba Mheshimiwa Mbowe anatumiwa na CCM kufanya hivi,Lakini wakati mwingine nalazimika kuamini kwamba huenda Mheshimiwa huyu anatumika.
Nitakuachia vielelezo vifuatavyo hapa chini uamue kama uniunge mkono ama la:
1) Chini ya Dr Slaa CHADEMA ilikuwa moto mkali bungeni,Lakini akaja kushawashiwa aachane na Ubunge agombee urais wa nchi huku akipatiwa mgombea mwenza mwenye elimu ya darasa la saba kutoka Zanzibar, hii inaonyesha kwamba hawakuwa na dhamira ya kushinda uchaguzi.Tangu Dr Slaa aondoke Bungeni CHADEMA imepoteza makali yake.
2) Wakati wa mchakato wa katiba mpya Upinzani chini ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Mheshimiwa Tundu Lissu ulikata shauri la kugomea mchakato mzima lakini Mheshimiwa Mbowe akawaburuza wapinzani kuingia makubaliano na rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM ambapo imeishia kwa Wapinzani kukosa walichokitaka na CCM kupata walichokitaka ambacho ni hii katiba pendekezwa.
3) Hakika hili suala la ESCROW ilikuwa kete muhimu ya kisiasa kwa wapinzani hasa ukitilia maanani kwamba kuna uchaguzi wa serikali za mitaa unakuja mwezi huu,CHADEMA walipaswa kuingia ndani zaidi Kwenye suala kwa kuibua majina ya watuhumiwa wote bila kujali vyeo vyao ili wananchi wawajue na hatimaye wafanye maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi,lakini suala la ESCROW likazimwa chini ya msaada wa Mbowe kwa kile kinachoelezwa kama kukubaliana maazimio maalum na Waziri mkuu Mizengo Linda.
4) CHADEMA imeanza kupoteza wagombea wengi wa serikali za mitaa nchi nzima kutokana na makosa ya kizembe kabisa,Ajabu ni kwamba makosa ya namna hii yamekuwa yakifanywa mara kwa mara wakati wa chaguzi mbalimbali na uongozi wa chama taifa huonekani kutafuta suluhisho juu ya makosa hay a.Unaweza kudhani labda hizi ni hujuma za makusudi zinazofanywa dhidi ya chama huku viongozi wakuu wakifahamu.
5) Mgogoro wa viongozi wa CHADEMA uliopelekea baadhi ya viongozi Kufukuzwa ni dhahiri viongozi waliosimamia maamuzi haya walijua fika kwamba maamuzi haya yangekidhohofisha chama lakini wakaendelea nayo,Leo hii chama kimegundua athari za maamuzi yale na kufikiria na kufikiria kutaka kumrudisha mmoja wapo wa waathirika wa maamuzi yale ambaye ni Zitto Kabwe.Chama kingechukua njia mbadala ya kushughulikia mgogoro ule hali ya kusiasa ya chama isingifikia hapo ilipo,Simtetei Zitto however ila nasisitiza kuhusu busara na hekima vitawale Kwenye maamuzi ya viongozi wa chama ili CHADEMA iendelee kutawala katika anga za kisiasa hapa nchini na isiwe vinginevyo.
6) Kutofanyika kwa uchaguzi ulio huru na wa haki hususani kwenye nafasi za juu za uongozi (mwenyekiti) kunadhohofisha hoja za chama za kupigania demokrasia na uchuguzi huru,Nina uhakika kwamba uongozi wa CHADEMA unafahamu kuhusu madhara ya kisiasa juu ya ufanywaji wa siasa za namna hii ndani ya chama,Je wanafanya hivi makusudi kuhidhohofisha CHADEMA?
Mbaya zaidi ni kuona sura zile zile za watu wakirejea kwenye nafasi nyeti za uongozi (Katibu mkuu na Mwenyekiti) tena kutoka kanda moja.Nilidhani CHADEMA wangejirekebisha kupitia uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwa kuweka sura mpya za viongozi kwenye hizo nafasi muhimu lakini wapi,Ni kama vile wanawasaidia CCM kuhuisha propaganda zao za ukanda dhidi ya CHADEMA.