CHADEMA imebadili sana aina ya uendeshaji wa siasa zake hivyo kuwapa shida wapinzani wao hata baadhi ya wanachama wake. Nakumbuka siku aliyouawa Mwangosi kama ingekuwa ni zama hizi inawezekana kabisa watu wasingeenda Nyololo na Mwangosi asingeuawa.
Enzi hizo zinazosifiwa kwa nderemo hivi sasa na CCM ni zile zama za Dk.Slaa akiwa anaamini kwenye kusukumana na Dola. Ilikuwa misisimko ndiyo siasa na nguvu nyingi sana zilitumika kushindana na watu wenye hamu ya kutoa "fundisho" kwa wapinzani wao kwa kutumia nguvu za dola.
Kwenye Uchaguzi wa Kalenga Dr.Slaa alisema "Hatutaki damu ya mtanzania hata mmoja imwagwe kwa lengo la CHADEMA kushinda" nikajua Dr.Slaa kaanza kuelewa kudili na wachochea vurugu wa CCM. Leo CHADEMA inayoitwa dhaifu na kuppoteza dira, ndiyo hiyo hiyo kila ikitaka kufanya jambo na kila lisemwalo na chama hicho, kinaleta kiwewe upande wa pili.